Verossa

Naridhika hata kwa mbilimbi usinisemee asee

Unajua nakuthamini zaidi ya nyota na gwaride

Bila ya wewe mimi siwezi kuishi, ni sawa na kukosa posho na mshahara

Nakuheshimu kama ninavyoheshimu gwanda langu

Wewe ndio IGP wa moyo wangu...CDF wa maisha yangu

Moyo wangu ulikuwa umevunjwa kama kota za polisi

ila umeupendezesha zaidi ya kambi ya Lugalo!
 
Mie sikulichukia ila kutoka moyoni sikuamua kulielewa tu na wala sikuhangaika kabisa, na kwenye papers swali lake nilikuwa kama silionagi vile, naselect tu mengine. Khaaa hapana tu. Kwa hiyo ningeamua kuelewa, ningelielewa tu by hook or by crook
 
Nakuomba utulie na mie huko kwingine watakuvuruga vuruga kama elimu bure, na wakutelekeze kama shule za kata
 
Umeanza pesa umekuja mandingo....nimebarikiwa sekta zote aisee.

Ulichezea bahati kwa Mjeda yule, ukachezea bahati kwa Kipaji Halisi, Mtambuzi alitaka kukufanya nyumba ndogo sijui mke mdogo ukaringa, sasa umebaki unalilia celica!!!!
Usiwaambie kama una mandingo please nna moyo wa kuvumilia kuona wallet yako inagombaniwa sio mandingo
 
Nakuomba utulie na mie huko kwingine watakuvuruga vuruga kama elimu bure, na wakutelekeze kama shule za kata

Napenda unavyopenda hesabu hasa ile ya: 1 + 6 😛

Kwako nimetulia tuli kama niko kwenye ukaguzi wa gwaride la Rais

Au zaidi ya yule kanali nyuma ya raisi🙂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…