Wakuu hii mboga nilishawahi kulaga ni MIRUNGI au kwajina lingine wanaiiita Gati! Nilishawahi kulaga lakini ulevi wake ni balaa au unaweza kuita Handasi kwa wale wataalamu wanavyoita. Siku nilikula huo ulevi wake bwana hupati usingizi unatafuna tu wakuu, basi nilitafuna wenyewe wanasema unasaga mpaka kunakucha ilivyofika milango ya saa tatu asubuhi jua linawaka nikaenda chooni na tochi yaani wewe unahisi bado ni usiku, halafu kwenye kujisaidia haja kubwa nikajisaidia haja kubwa kama mbuzi! Jamani ulevi mwingine nyie wacheni tu.