Vatican kujieleza kuhusu kashfa za ngono

Vatican kujieleza kuhusu kashfa za ngono

Status
Not open for further replies.

kahtaan

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2009
Posts
19,174
Reaction score
11,628
Vatican kujieleza kuhusu kashfa za ngono - BBC Swahili - Habari
131224212954_vatican_pope_christmas_304x171_getty.jpg





Maafisa katika Vatican makao makuu ya kanisa katoliki, wanatarajariwa kuhojiwa na maafisa wa Umoja wa Mataifa kuhusu dhuluma za kingono ambazo makasisi wa kanisa hilo waliwatendea maelfu ya watoto.
Maafisa hao walikataa ombi la awali ambapo Umoja wa Mataifa ulikuwa unataka taarifa za kina kuhusu dhuluma za kingono wakisema kuwa visa hivyo vinapaswa kushughulikiwa na idara ya mahakama katika mataifa ambako visa hivyo vilitokea.
[h=3]Kashfa katika kanisa katoliki[/h]Ujerumani-Kasisi aliyejulikana akama Andreas L, alikiri mwaka 2012 kuwa aliwalawiti, watoto watatu wa kiume.
Marekani – ufichuzi kuhusu makasisi wawili Paul Shanley na John Geoghan waliowalawiti watoto mapema miaka ya tisini ,iliwaghadhabisha watu wengi sana.
Ubelgiji - Askofu Bruges, Roger Vangheluwe, alijiuzulu Aprili mwaka 2010 baada ya kukiri kuwalawiti watoto wavulana kwa miaka mingi
Italy – Kanisa katoliki mnamo mwaka 2010 ilikiri kuwa visa 100 vya makasisi kuwalawiti watoto viliripotiwa kwa zaidi ya miaka kumi
Ireland – Ripoti iliyotolewa mwaka 2009 iligundua kuwa visa vya makasisi kuwalawiti watoto vilitokea sana mapema karne ya ishirini.




[h=2]Taarifa zinazohusiana[/h]



Papa Francis amesema kuwa ni jambo muhimu kukabiliana na visa kama hivyo ili kanisa liweze kupata sifa yake nzuri.
Kanisa hilo limekosolewa kwa kukosa kuchukua hatua za kutosha kuhusiana na madai ya dhuluma za kingono kanisani.
Mwezi jana, Papa Francis alitangaza kubuni kamati ya kukabiliana na visa vya dhuluma za kingono dhidi ya watoto kanisani pamoja na kutoa ushauri nasaha kwa waathiriwa.
Pia alitilia mkazo sheria kadhaa za kukabiliana na watuhumiwa wa dhuluma za kingono na kupanua zaidi maana ya uhalifu.




[h=2]Taarifa zinazohusiana[/h]

 
Si wanasema kwenye mafundisho yao ya biblia new version ngono na vitoto vidogo na kuwalawiti pia watoto wa kiume ni halali? Wanataka kujieleza nini sasa wakati kwao ni halali? Dini za watu ni majanga matupu.
 
Msiangalie mwili,angalieni roho,uliotenda ni mwili,kwa roho bado ina uzima wa milele.Hawa wa
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom