Vatican haijawahi kuwa na balozi Tanzania, tatizo ni uelewa wa "Sovereignty"

Paschal Matubi

Verified Member
Sep 15, 2008
212
500
- - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - -
Nimekuwa nikiamini kwamba Vatican ina ubalozi hapa nchini, lakini nimeshangazwa na makala hii ya RAIA MWEMA ya last week inasema tofauti. Sijui wanaodi mnasemaje!!!!!!!!!
- - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - -
SOURCE: MAKALA
GAZETI: RAIA MWEMA, JUNE 15, 2017
AUTOHR: JOSEPH
HEADLINE: (Vatican haijawahi kuwa na balozi Tanzania, tatizo ni uelewa wa "Sovereignty")
WEBSITE: www.raiamwema.co.tz/vatican-haijawahi-kuwa-na-balozi-tanzania-tatizo-ni-uelewa-wa-sovereignty
- - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - -

WAMISIONARI wa “Order of Malta” wanamiliki jengo “Palazzo di Malta” jijini Roma. Ukiingia unakuwa umeondoka nchini Italy. Je, humo “Palazzo di Malta” ni “nchi” gani?

Tanzania imeletewa balozi mpya, mpoland, anaitwa askofu Marek Solczyński. Je, anakuja kuwa balozi wa nchi gani? Msomaji, usipoelewa neno “sovereignty” hutajibu maswali haya mawili.

Bado wapo wanaojibu swali la pili kwamba nchi huhusiana na nchi, hakuna nchi inayoitwa “Holy See” lakini ipo iitwayo “Vatican”. Hivyo, “Vatican” ndiyo inayoleta mabalozi. Lakini ukiwabana kwa hoja hiyohiyo, ni bahati sana wakikujibu swali la kwanza.

Hivyo nitaeleza sana neno “sovereignty”. Binadamu wa mwanzo aliishi, jangwani, visiwani, mapangoni au porini. Hivyo alitumia haki zake kwa uhuru wa kutodhibitiwa na sheria za wenzake duniani.

Unapoishi bila kudhibitiwa hivi, maisha ya uhuru wa namna hiyo yanaitwa “sovereignty” na unaeyaishi unaitwa “sovereign”.

Mimi na wewe tuliipoteza “sovereignty” tulipoogopa upweke na pori, tukaungana kwenye jamii, maisha yetu yakadhibitiwa na “sheria” za jamii. Hivyo, kujitenga na sheria za jamii ni njia ya binadamu kurudisha “sovereignty” yake.

Jamii zilishazoea kumuamini mtu mmoja atumie “sovereignty” yake kuongoza jamii. Ingawa neno “sovereign” halikuwepo walimwita majina kama “farao”, “mfalme”, “malkia”, “czar”, “emperor”, “sultani”, “omukulu”, “mangi”, “chifu”, “mtemi”, “mukwavinyika”, “kabaka”.

Kufikia mwaka 313, mtawala “Constantine” wa Roma aliuruhusu ukristo Ulaya. Kiongozi wa wakristo akajikuta anaheshimiwa na hadhibitiwi tena na sheria za Ulaya. Akapata “sovereignty” bila kuwa mtawala.

Roma ilipoanguka mwaka 476, wafalme wakarithi nidhamu ya kutomdhibiti kwa sheria za makabila yao. Waliomshambulia walipatwa msukosuko.

Jina lake rasmi ni “Askofu wa Roma” lakini akajikuta anaitwa majina kadhaa, mengine yanaonyesha heshima kwake, mfano “Papa” na mengine yanatambulisha mamlaka ya kiti chake cha uongozi, kama vile “Holy See”.

Mfumo uitwao “feudalism” ulianzia kabila la “Frank” mwaka 750: {Children's Encyclopedia of British History, 1996, uk. 26}. Humo mtu alipata hadhi kulingana na ardhi anayomiliki, akaitwa “baron”.

Ardhi iliyomilikiwa iliitwa “fief” na ulipewa na mfalme. “Askofu wa Jimbo” naye alitengewa ardhi yake.

Mwaka 754, mfalme Pippin III wa “Frank” alimpa Papa Stephano ardhi aimiliki. Watu waligombana wakijiuliza, nani hasa ndiye mmiliki mkuu wa ardhi yaani “état” au “state”? Je, ni “baron”, “mfalme” au “Papa”?

Lakini hadhi (status) ya “Papa” ilizidi wote Ulaya, ardhi aliyopewa ikaitwa “Papal states. Wafalme wakawa “vassal state”, yaani ni “state” lakini mahusiano yao anayadhibiti “suzerainty” yaani “Papa”, akitangaza vita wafalme wanamtii.

Kufikia mwaka 1544 jamii zilishajiona ni “taifa” si “kabila” na ukatoliki siyo dini ya wote. Ndipo mwaka 1576, Profesa Jean Bodin alishauri kwamba mkuu wa taifa yaani “state”, asidhibitiwe. Prof. Bodin alitumia neno “sovereignty” lililozaa neno “sovereign state”.

Mei 15, 1648 mataifa Ulaya yaliingia mkataba wa “Westphalia”, neno “sovereign state” likavuma hadi leo likimaanisha huyo “state” ni yule mwenye “sovereignty”. Kuna uvumi kwamba kipindi hiki mfalme Louis XIV wa France alitamka “mimi ndiye state”.

Huko nyuma, Februari 15, 1113 Papa Paschal II aliamuru watawa waitwao “Order of Jerusalem” wasidhibitiwe na jamii yoyote na mwaka 1530 wakahamia Malta wakaitwa “Order of Malta”.

Mwaka 1798, Napoleon Bonaparte wa France aliwafukuza “Order of Malta” kutoka Malta. Walipohamia Roma, mwaka 1868 Papa Pius IX akazipa nyumba zao “Palazzo di Malta” na “Villa di Malta” kinga iitwayo “extra-territorial”, zisiguswe na sheria yoyote.

Septemba 20, 1870 mfalme Victor Emmanuel II aliipora ardhi ya “Papal states” ikawa sehemu Italy.

Mjadala ukaibuka, “Papa” sasa amekuwa nani katika Italy? Mabalozi pale Roma, wametumwa na nchi zao kufanya nini? Mabalozi anaoendelea kuwateua “Papa”, wanakopokelewa wanawakilisha nini wakati “Papal States” ilishafutika?

Maswali haya yaliitwa “Roman Question”. Papa Pius IX hakujishughulisha na mjadala, alijiita “Prisoner in the Vatican” yaani “mfungwa ndani ya Vatican”.

Mwaka 1929, Mfalme Victor Emmanuel III wa Italy na Papa Pius XI waliingia mkataba iitwayo “Lateran Pacts”, Italy ikarudisha maeneo kadhaa iliyopora ikiwemo ardhi ya “Vatican”.

Wanaochambua suala la “Vatican” hujitahidi huonyesha kama ina serikali au la. Papa” hutoa taarifa ziitwazo “Annuario Pontificio” na humo amejitaja kwamba pale Vatican” anaitwa “Sovereign wa Vatican”.

Hivyo, Vatican” ni ardhi anayoimiliki binadamu mmoja tu, askofu wa Roma” tangu mwaka 754 miaka minne tangu kuanza “feudalism” tuliyoiita “ukabaila”.

Je, kanisa linajisemaje kuhusu kuwa na “serikali” yoyote, kama kweli linayo? Kanisa Katoliki lina uongozi na unathibitishwa na maandiko yafuatayo, (1: Katekism ya Kanisa Katoliki”) na (2: Sheria za Kanisa”).

Ibara ya 880 hadi 896 ya “Katekism ya Kanisa Katoliki” inautaja uongozi kuwa ni ule wa “askofu wa Roma” kwa kushirikiana na “maaskofu wa majimbo” walioenea duniani kote.

Uongozi huo unaoitwa “magisterium” ndiyo unayostahili kufananishwa na “Serikali ya Kanisa Katoliki”. Lipo kundi linalosaidia “magisterium” linaitwa “ministerium”.

Lakini “ministerium” ni pana mno imeelezwa kwenye ibara ya 334 ya “Sheria za Kanisa” (Can. 334) ambayo Askofu Severine Niwe Mugizi aliitafsiri hivi, “Katika kutenda wajibu wa ofisi yake Baba Mtakatifu, anasaidiwa na maaskofu wanaoshirikiana naye kwa njia mbalimbali, kati ya hizo ni sinodi ya maaskofu. Anasaidiwa pia na makardinali kama wafanyavyo watu wengine pia na taasisi nyingine kulingana na mahitaji ya wakati. Watu wote hao na taasisi hizo hufanya kazi walizokabidhiwa kwa mema ya makanisa yote kwa niaba na mamlaka yake, kwa mujibu uliowekwa na sheria.{Severine Niwe Mugizi, Zijue Sheria za Kanisa, 1996, uk. 46}.

Hivyo, sehemu za “ministerium” zinazomsaidia “Papa”, baadhi nazitaja huku ibara zinazoelekeza usaidizi zikiwa kwenye mabano.

Taarifa ya askofu kwa “Papa” ya kila miaka mitano “ad limina” imo katika ibara ya (Can. 399-400), Sinodi za maaskofu (Can. 342- 348), makardinali (Can. 349-359), “Roman Curia” (Can. 360-361), wanaomwakilisha kwenye mataifa kama Tanzania (balozi) wamo kwenye (Can. 362-367).

Muumini wa kawaida, yaani mlei, usaidizi wake umeelezwa kwenye ibara ya 897 hadi 913 ya “Katekism ya Kanisa Katoliki”.

Hivyo, “Roman Curia” si serikali, ni kundi mojawapo tu la usaidizi yaani “ministerium” kama mengine, na yotea yanapomsaidia “Papa” hufanya “kwa niaba na mamlaka yake”.

Tuone ibara mahsusi kuhusu mabalozi leo yaani (Can. 363(1)) inayosema, “Wawakilishi wa Baba Mtakatifu wanapewa wajibu wa kumwakilisha yeye kwa hali imara katika makanisa ya mahali na pia kwa mataifa na wenye mamlaka ambako wanatumwa”: {Severine Niwe Mugizi, uk. 46}.

Askofu Severine wa Rulenge-Ngara, ametafsiri kiingereza kinachosomeka “representing in a stable manner the person of the Roman Pontiff”. Hivyo, wawakilishi wanaoitwa “mabalozi”, wanamwakilisha binadamu mmoja tu (the person) anayeitwa “Askofu wa Roma”.

Hivyo, Rais wa Tanzania, atampokea askofu Marek Solczyński kama “mwakilishi wa Papa”, anayekuja kumwakilisha binadamu anayeitwa “Askofu wa Roma”, wakatoliki tunamwita “legate” au “Nuncio”.

Hakuna tamko linalosema hawa ni mabalozi wa “Vatican”, wala “Mkataba wa Lateran” hauna ibara inayotamka hivyo.

Hivyo, ukilipenda jina “balozi” bora umwite “Balozi wa askofu wa Roma” au “Balozi wa Papa” kuliko kosa sugu la kumuita “Balozi wa Vatican”. Siyo tu haji kuwa “Balozi wa Vatican”, bali pia hiyo “Vatican” haijawahi kuwa na ubalozi kokote duniani.

Tumeona hoja za Kanisa Katoliki linavyojisema. Sasa tuone hoja za wataalamu, Prof. Lassa Oppenheim ambaye mwaka 1911 aliandika mada nitakayoijadili iitwayo {International Law. A Treatise. Volume I (of 2)} na Dk. Robert Graham ambaye mwaka 1959 aliandika kitabu {Vatican Diplomacy. A Study of Church and State on the International Plane, 1959}.

Ninaweza kujieleza bila kuwataja hawa, lakini mada zao katika fani ya kimataifa hurejewa kote hata na mahakama za dunia.

Kuhusu matokeo ya “Papa” kuporwa ardhi, Prof. Oppenheim anasema “It seemed impossible that the Pope should become an ordinary Italian subject and that the Holy See should be an institution under the territorial supremacy of Italy”: {Oppenheim, §105}.

Hapa Prof. Oppenheim anasema, ilishindikana “Papa” kudhibitiwa na sheria za Italy. Hivyo anathibitisha “sovereignty” ya “Papa” haikupotezwa na uporaji wa ardhi.

Lakini sentensi za Prof. Oppenheim zinaonyesha naye alidhani “Holy See” na “Papa” ni vitu viwili tofauti.

Watafiti hata wa leo, wangesoma mafundisho ya kanisa, neno “Holy See” lisingechawanganya kwani wasingeliona katika ibara zote 2865 za “Katekism ya Kanisa Katoliki”.

Katekism imeeleza vizuri uongozi, ambao ni “Askofu wa Jimbo” na “Askofu wa Jimbo” yaani “magisterium” na usaidizi ambao ni “ministerium”.

Mei 13, 1871, Italy iliweka sheria kumlinda Papa iliyoitwa “Law of Guaranty” lakini Papa Pius IX aliipuuza.

Prof. Oppenheim anasema, “The Law of Guaranty is not International but Italian Municipal Law”: {Oppenheim, §106}. Hapa anakiri hoja ya Pius IX kwamba Italy inatunga sheria kwa waitalia tu, “Papa” hakugeuka kuwa muitalia.

Mwaka 1959, Dk. Robert Graham alisema hivi, “it is common error to suppose that the Lateran Treaty of 1929 finally re-established the papacy as a subject of international laws. This misapprehension ignores the evolution of legal thinking during the preceding decades”: {Vatican Diplomacy, uk. 201, aya ya mwisho}.

Hapa anasema, kuna kosa sugu la kudhani kwamba “Mkataba wa Lateran” ndiyo ulimfanya “Papa” atambuliwe na sheria za kimataifa, akapata “sovereignty”. Anasema, wanaosema hivi hawajui hoja za kisheria za miaka iliyotangulia.

Msomaji, hapa anaowakosoa Dk. Graham ni pamoja na wale wenye kuuliza, je, “Vatican” ni “state”? Je, ina bendera? Je, ina sarafu? Je, ina jeshi? Je, ina serikali? Je, ina gavana? Je, ina mahakama? Je, ina magereza? Je, ina bunge? Je, ina polisi? Je, ina katiba na sheria? Je, ina utaifa? Je, ina ardhi yenye mipaka? Je, ina wimbo wa taifa? Je, ina nembo ya taifa? Je, ina lugha ya taifa? Je, inapigiwa saluti ya mizinga? Je, ina “stempu”? Je, ina redio? Je, ina namba za simu (country code)?

Msomaji, “sovereignty” ya “Papa” inayompa uwezo wa kuwakilishwa, haithibiki kwa maswali haya, hata kama majibu yote 22 yangekuwa ni “NDIYO”, tena mengi ni “SIYO” nataja mifano miwili tu ifuatayo ya “utaifa” na “wimbo wa taifa”.

Mfano wa kwanza ni ibara ya 9 ya “Mkataba wa Lateran” (art. 9) inasema hivi, “In accordance with the provisions of International Law, all persons having permanent residence within Vatican City are subject to the sovereignty of the Holy See”.

Msomaji, kwenye ibara hii umeona neno “subject”. Linalitafsiriwa hivi, “-sio huru, liotawaliwa na serikali ya kigeni”: {English-Swahili Dictionary-TUKI, ISBN: 9976911297, uk. 860}.

Mfano mzuri wa “subject” ni kwamba mtu wa Oman, Qatar, Saudi Arabia, Falme za Kiarabu, huko anaitwa “subject” wa sultani au mfalme. Kwa lugha rahisi ni “mtu wa sultani” au “mtu wa mfalme”. Utii unaoitwa “allegiance” ni kwa “mfalme” au “sultani”.

Tumeona ile ibara(art. 9) penye neno “subject” ikisema mkazi wa “Vatican” ni “mtu wa Holy See” na kiusahihi zaidi ni “mtu wa askofu wa Roma”.

Kwa msingi huo, “Sovereign wa Vatican” hana watu anaoweza kuwaita taifa lake kama mwenzake “Sultan wa Oman”. Tumeona walioko pale, ule utii wao (subject) ni kwa amri na matakwa ya “Askofu wa Roma”.

Mfano wa pili, ule wimbo. Umemtaja “Askofu wa Roma” anayeombewa kuliongoza kanisa na umetaja eneo moja tu “Roma”. Hauitwi “anthem”, unaitwa “hymn”.

Hivyo, “Vatican” haina wimbo uuite “wa taifa”, ule unaitwa“Pontifical Hymn” yaani wimbo kwa “askofu wa Roma”.

Mifano hii miwili, inatosha kuonyesha urahisi wa kutikisa hoja zinazobebwa na yale maswali 22, hivyo tuendelee na mada yangu.

Dk. Graham, anasema “The fact that the Holy See is a non-territorial institution is no longer regarded as a reason for denying it international personality. The papacy on its own can act in the name of international community: {Vatican Diplomacy, uk. 201, sentensi ya kwanza}.

Msomaji, Dk. Graham hapa anasema, dunia ilishakiri kwamba kutomiliki ardhi hakumuondolei “Papa” uhusiano na mataifa. Ule uaskofu wake wa Roma, ni kigezo kinachojitosheleza kumuingiza katika jumuiya ya kimataifa.

Dk. Graham anaendelea hivi, “Had the Vatican State never come into being in 1929, international law would have increasingly recognised the non- territorial sovereignty of the papacy”: {Vatican Diplomacy, uk. 202, sentensi ya kwanza}.

Hapa anasema, hata Italy isingemrudishia “Papa” ardhi ya “Vatican”, bado jumuiya ya kimataifa, iliyoshindwa kumkataa mwaka 1870 hadi 1929 wakati hamiliki ardhi, ingeendeleza zaidi kuitambua “sovereignty” yake.

Hoja hii siyo ngeni. Mwaka 1911 kabla “Vatican” haijarudishwa, Prof.Oppenheim alisema, hivi “although the Pope is no longer the head of a State, the privileges due to the head of a monarchical State are still granted to him by foreign States”: {Oppenheim, §106}.

Hapa Prof. Oppenheim alisema, mataifa yaliendelea kumpa “Papa” hadhi kama mkuu wa nchi japo hakuwa na ardhi tangu mwaka 1870.

Hivyo, kumrudishia “Papa” ardhi ya “Vatican”, hakukumuongezea chochote mwaka 1929, kwani “sovereignty” yake haikupotea alipoporwa ardhi hiyo mwaka 1870.

“Sovereignty” ya “Papa” haikutengenezwa na umiliki ardhi, ilitokana na Ulaya kumheshimu, kumuamini, kumpenda, kumhusudu, kumlinda na hivyo kutomdhibiti na sheria zao tangu mwaka 313.

Hii ikaitwa “spiritual sovereignty”, Dk. Robert Graham anaiainisha hivi, “as states claim a territorial sovereignty, the Universal church claims its own kind of sovereignty, of a spiritual nature”: {Vatican Diplomacy, uk. 218, aya ya kwanza, sentensi ya nne}.

Hii “spiritual sovereignty” wasomi walizembea kuitafiti mwaka 754 hadi 1870, ikajidhihirisha rasmi ilivyotumika mwaka 1870 hadi 1929 ambapo sasa “Papa” hakuwa na ardhi.

Ingawa Prof. Oppenheim, hakutaja neno “spiritual sovereignty”, anathibitisha ilivyojificha anaposema hivi, “Even formerly, when the Pope was the head of a State, such Concordats were not concluded with the Papal States, but with the Holy See and the Pope as representatives of the Roman Catholic Church”: {Oppenheim, §106}.

Hapa Prof. Oppenheim anasema, hata mikataba ya kimataifa ya mwaka 754 hadi 1870, “Papa” hakuisaini kama “Sovereign wa Papal states” bali alisaini kama “Askofu wa Roma”.

Hivyo, Prof. Oppenheim na Dk. Graham, walishathibitisha kwamba “mahusiano ya kimataifa” si lazima yawe “nchi” na “nchi” tu.

Wameonyesha hata zamani mahusiano yalikuwa ni kati ya taifa na binadamu mmoja aitwaye “askofu wa Roma”, hayageuka kuwa mahusiano na “Vatican” ya sasa.

Siyo ajabu mataifa kuhusiana na binadamu mmoja. Mkutano wa kuigawa Afrika pale Berlin mwaka 1885, mataifa ulimhusisha “binadamu mmoja” aliyeitwa “Leopold Lodewijk”, tena akapewa eneo kubwa yaani “fief”, akaliita “Congo Free State” naye pale akaitwa “Sovereign wa Congo”.

Tumeona “Order of Malta” nao walivyoporwa ardhi ya Malta. Dk. Scarfo wa Italy aliishitaki “Order of Malta”. Kesi hiyo huitwa (Scarfo v. Sovereign Order of Malta, 24ILR (1957), Tribunal of Rome, Italy).

Mahakama ya Italy ilihukumu hivi, “Thus the status of the Order as a subject of international laws, at any rate, cannot be doubted because the Italian State, by establishing legation, has recognised the sovereignty of the Order within its own territory”: {Cases and Materials on International Law: ISBN: 0199562717, uk. 155}.

Nimetafsiri hivi, “hadhi ya “Order of Malta” kutambulika na sheria za kimataifa, kwa namna yoyote haina ubishi kwani kitendo cha Italy kuwa ubalozi wao, tayari imeitambua “sovereignty” yao”.

Msomaji, kipimo cha “sovereignty” ni kutoshitakika. Kiongozi wa “Order of Malta” hashitakiki kama alivyokataza Papa Paschal II mwaka 1113 na kama “Papa” mwenyewe asivyoshitakika tangu takriban mwaka 313.

Ubalozi wa “Order of Malta” jijini Roma jengoni “Villa di Malta” ni moja ya balozi zake 106 duniani, ingawa haina ardhi kwa miaka 219 sasa, tena walau “Papa” alirudishiwa ardhi ndogo ya “Vatican”.

Ukiingia “Palazzo di Malta” ambamo ni ekari tatu, “Order of Malta” hujisema umeingia nchi ndogo kuliko zote duniani.

Navijua vigezo vya Umoja wa Mataifa kuhusu “sovereignty”. Lakini umoja wowote siyo ofisi ya kugawa “sovereignty” kwani hata kujiunga ni utashi wako. Vigezo vya umoja wowote hukomea kwa wanachama wake, tena napo toka siku ulipoundwa hadi siku utakapovunjika au siku ya mwanachama kujitoa.

Kujitoa kama Britain inavyojitoa kwenye “EU”, au kuwepo kwa balozi 19 za Taiwan na 75 za Palestina, kunatokana na kujiamini kwamba “sovereignty” yako haipangiwi vigezo vya mahusiano, unajipangia..

Vivyohivyo mwaka 1870 hadi 1929 mataifa yaliendeleza mahusiano na “askofu wa Roma” huku yakijua hana ardhi. Natumaini nimeeleweka kwamba “Vatican City State” haijawahi kuwa na ubalozi kokote duniani.
- - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - -
 

nyabhingi

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
14,260
2,000
long story short,mfalme costantine ndiye aliyeleta duniani ujinga wa ukristo na uislam duniani hadi watu weusi nao wamedakia upu.uzi eti wataokolewa na kwenda peponi kupitia hawa waarabu na wazungu...ujinga mtupu.
 

nyabhingi

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
14,260
2,000
Kwa ufupi mleta Mada bwege ubalozi wa Vatican upo aende kwenye jumuiya Kama ni mkatololiki aulize Kama upo au haupo ila Kama ni bwege aendelee na msimamo wake kuwa ubalozi wa Vatican haupo Tanzania
kwa hiyo ubalozi unapatikana kwenye jumuiya!!!!si utuambie ulipo......
When your god and savior looks like your master and enslaver, you become the principal agent in your destruction-Dr. Yosef Ben- Jochannan
 

Paschal Matubi

Verified Member
Sep 15, 2008
212
500
Kwa ufupi mleta Mada bwege ubalozi wa Vatican upo aende kwenye jumuiya Kama ni mkatololiki aulize Kama upo au haupo ila Kama ni bwege aendelee na msimamo wake kuwa ubalozi wa Vatican haupo Tanzania
Changia hoja,

Hapa hakuna mleta mada, hii ni makala tumeiona gazetini, kama unadhani ni uongo lete ukweli unaoujua.
 

Mdanganywa

JF-Expert Member
Jun 15, 2009
584
250
long story short,mfalme costantine ndiye aliyeleta duniani ujinga wa ukristo na uislam duniani hadi watu weusi nao wamedakia upu.uzi eti wataokolewa na kwenda peponi kupitia hawa waarabu na wazungu...ujinga mtupu.
Constantine hakuleta ukristo. Aliukuta na ulimshinda kuutekekeza akaamua kuupenda akaachana na dini za kijinga.
 

Ticktock dork

JF-Expert Member
Dec 23, 2015
435
250
Kwa ufupi mleta Mada bwege ubalozi wa Vatican upo aende kwenye jumuiya Kama ni mkatololiki aulize Kama upo au haupo ila Kama ni bwege aendelee na msimamo wake kuwa ubalozi wa Vatican haupo Tanzania
ss jumuiya ni inahusika na balozi za nchi
taja ofisi za ubalozi wao zpo wapi
 

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
28,786
2,000
Haya mambo ya imani za kidini huwa sipendi sana kujishirikisha nayo maana naamini mimi ni akili kubwa ya sayansi na teknolojia
 

Zanzibar-Nyamwezi

JF-Expert Member
Jun 11, 2013
808
500
Pia kuna watanzania ni mabalozi wanaowakilisha Vatican duniani wakiwa kama Raia na viongozi wa Vatican duniani. Ubalozi wa hapa upo nyuma ya kanisa la mtakatifu Petro, Namanga
 

Kibehe

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
883
1,000
Acha uongo. Nyuma ya st peters au mkabala na st peters nyumba inayotizamana na ya Bakhresa no kwako ?
 

nyabhingi

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
14,260
2,000
Constantine hakuleta ukristo. Aliukuta na ulimshinda kuutekekeza akaamua kuupenda akaachana na dini za kijinga.
constantine ndiye muasisi wa ukristo unaomuabudu yesu mwaka 325 AD kwenye mkutano maarufu alioutisha kule NICEA,na wale wajumbe walikuwa na machaguo mawili,wakubaliane naye au wauawe!
 

A k A

JF-Expert Member
Jan 9, 2016
210
500
Acha uongo. Nyuma ya st peters au mkabala na st peters nyumba inayotizamana na ya Bakhresa no kwako ?
Ubalozi upo nyuma ya kanisa LA st Peters huku geti lao lipo mkabala na ofisi kuu za suti nyeusi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom