Vasectomy imeniponza: Mke wangu ana mimba ya wajanja, nifanyeje!

ndyoko

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,971
1,650
Miezi 10 iliyopita niliamua kufanyiwa uzazi wa mpango kwa kutumia ile njia ijulikanayo kwa jina la VASECTOMY. Hii ni baada ya kuona mwenzangu 'hesabu' zimemshinda kabisa. Nikaona ili kuepuka uwezekanao wa kuwa na familia yenye idadi ya timu ya mpira-maana watoto 8 ktk ndoa ya miaka10 sio mchezo-nikaona acha jukumu la uzazi wa mpango nilichukue mwenyewe. Nikaamua kufanyiwa vasectomy.

Miezi miwili imepita sasa, nimegundua mke wangu ni mjamzito, tena wa miezi 3. Hii ni baada ya kuona dalili zile zinazoambatana na mimba changa. Nilipohisi nikaamua kumpeleka hosp lakini bila yeye kujua, nikaongea na daktari ampime mimba na anipe majibu privately. Mungu si Athumani, vipimo vikaonyesha mke wangu ana mimba ya miezi miwili. Sikuonyesha kushangaa mbele ya dr kwani sikutaka ajue mshangao wangu ktk hilo. Hata hivyo wife ameshaanza kuhisi kuwa amenasa, na amekosa amani ghafla.

Awali nilidhani huenda hiyo operesheni haikufanywa vizuri, lakini nilipoenda kuangaliwa upya mtaalamu iko sawa na nisingeweza kumtia ujauzito my wife. Hivyo ni wazi mimba hii ni ya mwanaume mwingine.

Wajemeni naomba mnishauri nifanyeje. Na kama ni adhabu, nimpatie adhabu gani..........nimchinje, nimpe talaka, au niendelee kulea 'kiumbe cha mwanaume mwingine?
 
Pole mkuu.

Ila sheria ya Ndoa ya Tanzania inamlinda mkeo. Hata kama ukichukua vipimo vya DNA na kugundua kuwa mimba si yako kabisa, KITANDA HAKIZAI HARAMU (kwa sheria ya Tanzania). Unaweza kuuchuna na kumwonya, for the best interest of your other children.

Jikaze mzee.
 
Mna watoto wangapi na mkeo kabla ya hiki kipya?
Kama ni above 5 watoto
bora na hiki kipya changanya na wako ulee tu

Tahadhari
mkeo kimeo, anweza leta gonjwa ndani
hao watoto mlionao wangapi mamluki?

Duh ndoa ngumu poleni
matatizo ni kipimo cha akili
 
Pole mkuu.

Ila sheria ya Ndoa ya Tanzania inamlinda mkeo. Hata kama ukichukua vipimo vya DNA na kugundua kuwa mimba si yako kabisa, KITANDA HAKIZAI HARAMU (kwa sheria ya Tanzania). Unaweza kuuchuna na kumwonya, for the best interest of your other children.

Jikaze mzee.

kwa hiyo unanishauri na shule nimpeleke na gharama nyingine nitoe as if ni mwanangu huku nikijua sio wangu? Hata kama limbwata hii sasa itakuwa imezidi, loooooooh!
 
Hapa chukua watoto wote pima DNA unaweza kukuta kwamba hata
kwenye aho waliobaki wapo ambao sio wa kwako kisha timua na mama
yao acha uzandiki

hata simba wa porini hatunzi watoto wa mume mwenzie kama ni wadogo
sana huua ili aweze kupata uzao wake............kwa heri
 
Ndo na iheshimiwe na watu wote . Tafakari chukua hatua .

ushindwe wewe na ukakamae kabisa! kuna haja gani sasa ya kulaumiana inapotokea unasalitiwa? si ukae kimya tu maana haileti tofauti kama hupendi kusalitiwa lakini unapenda watoto wa 'wenzio' unaopewa kupitia kwa mkeo!
 
Hapa chukua watoto wote pima DNA unaweza kukuta kwamba hata
kwenye aho waliobaki wapo ambao sio wa kwako kisha timua na mama
yao acha uzandiki

hata simba wa porini hatunzi watoto wa mume mwenzie kama ni wadogo
sana huua ili aweze kupata uzao wake............kwa heri

asante sana mkuu. nadhani hii ni moja ya suluhu ya hii kadhia iliyopo mbele yangu
 
Kaka ndoa inahitaji hekima na busara,vumilia.Maana ukufanya maamuzi ya hatari hata wewe hautakuwa salama
 
Kinachoniuma ni kwamba nilipochukua uamuzi wa kufanya vasectomy, alifurahi sana na kuwaeleza watu jinsi alivyoona kuwa mimi ni responsible husaband. manesi pia walinisifia sana. sasa ghafla wife ana mimba, ntauweka wapi mimi uso wangu jamaniiiiiiiiiiiiiiiiiii! si afadhali angetumia kinga, walau angenisitiri utu wangu?
 
ntaanza kufanya DNA test very soon ili niweze kujua 'gravity' ya hii kitu, nahisi nimedhalilishwa sana mbele ya jamii. afadhali ingekuwa sijafanya hiyo operation ingekuwa rahisi kupotezea lakini ni ngumu ktk hali yangu ya sasa.
 
Hakuna binadamu asie kusea,hata wewe inawezekana ulimkosea japo mara moja na akakusamehe,mpe nafasi nyengine kwani usikumbuke mabaya yake tuu ana mema pia alokutendea,kaanae chini mzungumze kama bado unaitaka ndoa yako na unapenda watoto wako. simanishi kwasababu ya watoto ndio uteseke moyo laa hashaa! uamuzi uko kwako sie wapiga chapuo tuu.
 
ina maana wewe sio mjanja?pole sana mwisho wa siku wewe ndio mwenye maamuzi ya mwisho!
 
Kati ya hao watoto mlio nao kuna uwezekano zaidi ya nusu sio wako.....

ndo maana sasa naona hata kupima DNA inaweza ikaja kuwa yaleyale ya kujimaliza kabla ya wakati..............sijui itakuwaje ntapojua kuwa hata hawa wengine kati yao sio wangu. presha inaweza kuniondoa duniani
 
Back
Top Bottom