Mke wangu kasema nafeli; je, nafeli wapi?

profesawaaganojipya

JF-Expert Member
Apr 21, 2015
1,485
3,134
Wakuu,

Nilikatiwa kipande cha ardhi na kanisa, kwa makubaliano kwamba nijenge fremu halafu tutakatana kwenye kodi na makato yakiisha fremu itakuwa mali ya kanisa.

Unapewa miezi 3 ya kujenga, hata kama hujamaliza fremu inaanza kusoma. Nilimaliza ujenzi ndani ya miezi tisa, nikaweka vifaa vya umeme wa majumbani.

Kwa kuwa mimi ni muajiriwa wa serikali, nikaona bora mke wangu akae maana alikuwa hana shughuli analala tu nyumbani.

Ni miaka miwili imepita bado mwaka mkataba uishe, hela anazouza mimi sizioni wala sijui ziko wapi, vifaa anaenda kujumua yeye, mambo yote ni yeye.

Sasa kuna wakati nakuwa sina hata hela ya kula, ilibidi leo nimuulize, inakuwaje fremu ni ya kwangu nimejenga mimi na mtaji ni wangu kwa nini hela anazificha na mimi sina hela.

Amenijibu kuwa nikiona hivyo, KUNA MAHALI NAFELI akanyamaza.

Sasa wakuu hivi nafeli wapi?
 
kimsingi umeona msanii.

ukiishaona mwanamke anashindwa kutambua ipi ni mali yako,ipi ya kwake na ipi ni ya familia,ujue huyo ni ng`ombe.

angeweza asikuonyeshe zilipo ila asikuombe hela ya chakula,au ada na mavazi ya watoto.tungempa cheo cha mke bora kabisa.

muhimu,acha kuiendeleza hiyo frem,mwambie huoni tija yake,kama ana akili atakataa na kukusitiza kwamaba yeye anaweza kuisimamia.
 
Mahali unapofeli;

1. Unashindwa kumdhibiti mkeo ndio maana mkeo naye anashindwa kudhibiti biashara.
Ili uwe na uwezo wa kumdhibiti yeyote lazima ajue kuwa unauwezo wa kumfukuza muda wowote utakao. Hapo lazima awe na heshima.

2. Mkeo sio mfanyabiashara ndio kwanza anahitaji uzoefu wa biashara alafu wewe unamdai Pesa.
Baada ya kumfungulia hiyo biashara ulitakiwa umsimamie mpaka apate uzoefu.

3. Jitahidi uishi kama Mwanaume ndani ya familia. Yaani kichwa. Kichwa ndio kinatawala kila jambo kwenye Mwili.
Ukiona Mkeo anashida basi jua shida yake imeanzia kwako(kichwani)
 
kimsingi umeona msanii.

ukiishaona mwanamke anashindwa kutambua ipi ni mali yako,ipi ya kwake na ipi ni ya familia,ujue huyo ni ng`ombe.

angeweza asikuonyeshe zilipo ila asikuombe hela ya chakula,au ada na mavazi ya watoto.tungempa cheo cha mke bora kabisa.

muhimu,acha kuiendeleza hiyo frem,mwambie huoni tija yake,kama ana akili atakataa na kukusitiza kwamaba yeye anaweza kuisimamia.
Baba au mme amepewa uwezo mkubwa hila wengi wetu hatuhutumii hata kwa asilimia moja!
 
Back
Top Bottom