Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,487
NJEMBA mmoja ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja, juzikati aliwashangaza watu baada ya kulazimisha kudendeka jukwaani na msanii wa Muziki wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee ‘V-Money’.
Tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita ndani ya Ukumbi wa Bilicanas uliopo Posta jijini Dar ambapo msanii huyo alikuwa akitumbuiza huku akipita kwa mashabiki na kutaka kuwapa mikono.
Katika hali ya kushangaza, Vanessa alipofika kwa mwanaume huyo alimpelekea mkono akitaka kumshika kidevu, ndipo njemba huyo alipomshika mwanadada huyo na kumvutia mdomoni mwake.
Hali hiyo ilimfanya Vanessa afurukute kujichomoa mikononi mwa mwanaume huyo na kuendelea na shoo huku akimuacha mshikaji akiwa kamtolea macho
Source: Bongo Movie