Value Renention Fees ni wizi wa dhahiri wa Bodi ya Mikopo

habari ya kuweka hela bank na kupata riba ni endapo ulifungua account maalum ya muda fulani! mkopo wowote usipourudisha kama makubaliano penati ni lazima.
 
Tofautisha fixed account na saving account.

Kwa wanaotumia saving account, kila mwisho wa mwaka wakati wa kufunga hesabu CRDB huwa wanatoa faida ya 3% ya kiwango kilichokua kwenye akaunti yako kwa muda fulani.

Ni ama hujawahi kuangalia akaunti yako au wakati wa kuweka riba basi akaunti yako inakua ipo chini ya kiwango cha chini hivyo haipewi faida.

Kuhusu HESLB, unapochelewa kulipa wanatoza penati ya 10% ya deni lote.

Kinacholalamikiwa kwenye uzi huu ni hiyo value retention fee ambayo haikuwepo kwenye mkataba wowote kabla ya mwaka 2011.

Mwaka 2011 walisema itahusu mikopo yote itakayotolewa kuanzia 2011.

Mwaka 2014 wakasema itahusu wadaiwa wote kuanzia 1994.

Kwa lugha rahisi, wewe ulikopa benki mwaka 2000 na hakukua na riba yeyote (faini ilikuwepo).

Mwaka 2014 benki inakuambia wanaanza kukutoza riba ya 6% ya deni lako lote kuanzia mwaka 2000.

mashart ya mkataba ni kuanza kulipa 8% ya kipato chako baada ya mwaka mmoja unapomaliza chuo kama sijakosea. Wote wanaolalamika deni limeongezeka ina maana wameanza kukatwa ndipo wakaona! je walipoanza kazi waliripot ili waanze kulipa?? ama walijua wengine watakopeshwa nini? watu wafwate taratibu sio tulalamike kila kitu.

Wengine wamefanya kazi miaka 10 wamejikausha kama hawajakopeshwa bado utawaona wakilalamika serikali haitoi mikopo kwa wanafunzi wote.
 
Leo nimeona form ya mfanyakazi mwenzangu ambae ameenda Ofisi ya Bodi ya mikopo na kuomba deni lake na kukuta anadaiwa 8,500,000/ km deni halisi cha ajabu ni kukuta kuna Penalty ya 10% ya deni husika ambapo ni 850,000/

Kilichonisikitisha zaidi kukuta kitu kinacho itwa VALUE RETENTION FEES ambapo ameandikiwa deni zaid la 3,519,000/ na alipojaribu kuuliza akasema hiyo VRE ni nini akaambiwa ni thamani halisi ya fedha ya wakati huu na ule kulinganisha na dola.

Sasa kama dola ilikuwa ni kiasi kadhaa kwa wakati ule na sasa hivi shilingi yetu inazidi kushuka thamani ndio hiyo kitu ina take place hapo?

Sasa nikajiuliza hivi serikal inafanya biashara kwa RAIA wake hadi iwaongezee gharama nusu ya deni husika?

Hivi watumishi wa Umma wanaoidai serikali miaka hata mitano mbona hiyo VRF hua haipigiwi wanapolipwa? Sasa kama unadai 2M basis na VRF na penalty ya 10% basi iwepo.

Huu ni wizi kama wizi mwingine unaofanywa na serikali hii ya awamu ya 5.
 
... Hivi watumishi wa Umma wanaoidai serikali miaka hata mitano mbona hiyo VRF hua haipigiwi wanapolipwa? Sasa kama unadai 2M basis na VRF na penalty ya 10% basi iwepo...
Thubutu, serikali ikupe bingo badala ya kukunyonya!!
 
Tunaumia jamani, jpm tusaidie
Si ndio hivyo anawasaidia kuwaondoa wapiga dili ili nyinyi mpate hela zile za kudondoka juu kama walivyokuwa wana wa Israel kipindi cha wanateremshiwa manna kule jangwani.

Malaika huwa anawapenda watu wake so after a certain time wote mtakuwa sawa na mashetani wengine ambao ni wapiga dili ila malaika wataruka naye.
 
Ndio maana sina hata hamu ya kulipa hilo deni, unalinganganisha thamani kwa hela ya bodi ila hela hiyohiyo mnayonikata nssf inakua haina hiyo thamani, endeleeni kutufanyia huo ujinga na sisi hatutoacha kuwafanyia upumbavu wa kutokulipa, hadi twende sawa.
 
Kwenye Ule mkataba au form za mkopo zilikuwa na hicho kipengele vinginevyo wanatuibia.
Au vitu vya kiserikali vinabadilika badilika tu Bila utaratibu
 
kuwa na penalty ya 10% na value retention fees ni wizi tu kama kukomoana, commercial banks ndo zinafanya hivyo ila sio kwa serikali yetu ambayo inaendeshwa kawa kodi zetu na ipo kutoa huduma na si kufanya biashara
 
Mi nadhani kuna haja ya kurenew ule mkataba.
Mfano umekopesha na serikali ukasoma ualimu kisha ukarudi ofisini kwako kufundisha kama awali. Unapigwa deni lile lile la alienda kufundisha shule za private ambako manufaa ni ya bwana yule mwenye shule au chuo.
Nilidhani deni lingekuwa na unafuu kwa public servants since they offer their skills and professionalism to the same tanzanians.
Hili swala limetufanya sisi tunaojiendeleza kulipwa mishahara midogo ukilinganisha na walimu wa diploma au mwenye uzoefu wa kutosha katika ualimu wa cheti ambao wao wapo chini yetu kidogo kwenye elimu.
Nijuavyo mimi kama vile jeshini yanatawala mapega na kwwnyevualimu inatakiwa kichwa (ubongo) uliowekezwa vizuri utawale kitu ambacho hakipo kabisa. Yaani unakuta mtu ana cheti anavuka mshahara wa mtu mwenye degree.
Mimi nilikuta deni hilo sijui nalilipa for 9yrs mfululizo. Thamani yake ni gari mpya kabisa.
Yaani ninaposikia mwingine anatoa matamko wakati huko kwa walimu ameuchuna tu namshangaaga halafu namwona wa ajabu sana
 
Habarini wana jamvi wa Jamii Forum…

Bodi ya Mikopo imekuwa ikijinasibu kuwa inatoa mikopo isiyo na interest kwa ajili ya kusomesha watoto wa maskini. Lakini kwa utafiti mdogo nilioufanya, nimegundua kuwa mikopo inayotolewa na bodi ya mikopo ina riba iliyofichwa kwenye jina la value retention fees (6% annually). Kiasi hiki sio penalty ya waliochelewa kulipa, bali ni rate inayodhaniwa kuwa ni inflation ya Tanzania. Vilevile, kiasi hiko huchajiwa kuanzia wakati bado mwanafunzi yuko chuoni akiwa anaendelea na masomo yake

Kwa mfano:

· Kwa mwanafunzi anayesoma miaka minne (let say; 2001, 2002, 2003 na 2004)

· Ambaye kila mwaka anakopeshwa Shs. 2,500,000 (ada, malazi na kula). Miaka minne atapewa 10M.

Deni atakalodaiwa mara baada ya kumaliza chuo (i.e. mwaka 2005) ni Shs. 11,500,000. Ambapo Shs. 1,500,000 ni value retention fee, sawa na ongezeko la asilimia 15 (15%) ya mkopo aliokopeshwa.

a) Je, bodi ya mikopo hawajinasibu kuwa mikopo wanayotoa inarudishwa kama ilivyo?

b) Je retention fees ina tofauti yoyote na interest inayochajiwa na taasisi za fedha ambao wao wamezika humo ‘effect of inflation’?

c) Je ni sahihi kuanza kumtoza value retention fees kijana ambaye bado anaendelea na masomo? - Mkopo ulitakiwa kuanza kuwa deni baada ya kumaliza masomo, ama wakati bado masomo yanaendelea?

Kwa mfano tulioutaja hapo juu, ikiwa huyo mwanafunzi atachelewa kuajiriwa kwa kipindi cha miaka miwili tu; retention fee ya mkopo wake wa mwaka wa kwanza peke yake itafikia Shs. 900,000 (sawa na 36% ya 2,500,000).

Jumla ya pesa yote atayokuwa anadaiwa ni Shs. 12,700,000 ambapo retention fee ni Shs. 2,700,000 ongezeko sawa na asilimia 27 (27%).

SWALI:

Je, wakopeshwaji waliwekwa wazi kwenye mikataba kuhusu mfumo huo wa kupanda kwa madeni yao hata kabla hawajamaliza masomo na kupata ajira?

o Waliokopeshwa waje humu kutujuza undani wa mikataba yao.

o Wataalamu wa sheria, fedha, huduma za jamii na siasa waweke michango yao pia.

HITIMISHO:

Wanaodaiwa walipe pesa walizokopeshwa; vile vile Serikali nayo (kupitia Bodi) wahakikishe wanakuwa fair, ili mfumo uliowekwa kwa ajili ya kuinua maskini usije ukawa unawakandamiza. Tunaamini, bodi ya mikopo haipo pale kibiashara, ipo kihuduma zaidi ili kusaidia kupunguza gepu kati ya maskini na matajiri. Mikataba wanayopewa wanafunzi ijieleze kinagaubaga.

Nawasilisha!
 
Tupo tunafanya maandalizi ya kuwaburuza hao bodi mahakamani, maana mikataba imekiukwa kwa kiwango cha kutisha. Bado tunakusanya ushahidi soon wataisoma namba na wengine wajiandae kupoteza kazi zao. You have been warned!!!!
 
Back
Top Bottom