Value Renention Fees ni wizi wa dhahiri wa Bodi ya Mikopo

Kudadadeki!!!! Kama hatujapata ajira tunalipaje sasa????au siku tukipata ajira ndio mkopo utakuwa umeshakuwa na penalty ya 90%!!!! Noma sanaaa

Jambo hili la mikopo ya elimu ni kama mchezo wa pata potea. Mtu kakopa, kazi hajapata na hana namna ya kuingiza kipato kiasi cha kuwa na ziada ya kulipa mkopo, na maisha yanazidi kuwa ya ghali. Halafu, serikali itegemee mikopo ya watu kama hao kulipwa! Watawakamata tu wale walioajiriwa na serikali yenyewe. Hapa ndipo ninapoona logic ya elimu bure. Mchango wa serikali katika maisha ya mtu iwe ni elimu bure.
 
nadhani ukienda kujisalimisha kwao after a year,hutakuwa na mapenati makubwa namna hiyo
muda wa kulipa ukifika wafuate,waeleze huna kazi ila unawwza jichanga hata 30per month wanakukubalia unaanza lipa
na kwasbb huna kazi sometimes unaweza usiwape chochote coz hujapata na still usilipe hayo mariba
yamewekwa kuwabana wanaotaka kukimbia kulipa tu
 
kuna madogo ndo wame graduate mwaka jana wanaingia tu kwenye market wanakutana na huu umzigo. yaani ni ful kulia lia ofisini pesa haitosh. yaani malengo yamevurugika gafla. waende na kwa mizee ilo someshwa na pesa ya serikali nayo ikatwe maana hakuna namna! Isiwe sisi tu. Kila mtu anastahili hiki kikombe
 
Kuna kipindi cha rehema ambacho ni mwaka mmoja tangu umalize chuo (masomo).

Baada ya hapo, utatozwa asilimia kumi ya jumla ya deni unalodaiwa kama adhabu (penalty).

Kwa kila mwaka unaoendelea kuchelewa kutorejesha, utatozwa asilimia sita ya pesa ulizokopeshwa (value retention fee) kwa kila mwaka wa masomo wa shahada uliyosomea. Kama ni miaka kumi imepita tangu umalize chuo na hujaanza kurejesha, basi tozo yako itakuwa asilimia sita ya kila pesa uliyokopeshwa kwa kila mwaka wa masomo zidisha mara tisa (ukitoa ule mwaka mmoja wa rehema).

Gharama zote hapo juu zitajumlishwa na kuwa deni 'halisi' unalodaiwa.

Pia kuna tozo ya asilimia moja (nadhani kama sikosei) ambayo wanaiita 'administration fee'. Hii wanaikata kwenye jumla ya deni lako (kwenye pesa halisi walizokukopesha/kabla hawajatoza tozo zao).

Angalizo: kama kuna sehemu nimenukuu kwa makosa naomba mniwie radhi, mwenye kufahamu kwa usahihi zaidi anisaidie kurekebisha.
Pia kabla ya hayo unatozwa asilimia 6 ya deni lote kwaajili ya kulinda thamani ya fedha.
 
kuna jamaa yangu yeye alipofika mwaka wa pili ali disco akaamua kuaaply diploma ya ualim na amemalza mwaka jana.je na yeye anatakiwa kurudisha mkopo ?
 
Hiyo value retention fee ilikuwa kwenye mkataba? wasisahau kuwa mkopo unalindwa na masharti ya mkataba. Pili nani kapitisha hiyo value retention fee, bunge au nani?
Yan hii system ilishafeli kabisa, iko ICU, Kila wanachofanya ni utumbo tu.
 
si waweke orodha ya hao wadaiwa tuione sasa,si ajabu wale wakopaji wa mwanzoni hawana kumbukumbu zao hapa wanatafuta taarifa zao kijanja tu
 
Naomba mnielimishe namna ya kukokotoa hiyo Value Retention Fee (VRF), naona inanichanganya kabisa.
mkuu, kama upo Dar ungeenda pale bodi ya mikopo ni kitu cha dakika 10 tu wanakupa deni lako lote.

Jinsi ya kukokotoa kidogo ni changamoto ila unaweza jikadiria kwa position yangu:

Nimemaliza chuo mwaka 2013: Nimesomeshwa na bodi 100%.

>Jumla ya hela walizonipia: Mil 11.3 hivi
>Mwezi wa tano mwaka huu 2016 wameleta list kwa HR nadaiwa mil. 13

Ila nina karatasi yao inaomesha hesabu zote hadi hela kufika hapo. Nashauri ungeenda bodi sio kwamba ukienda wanaanza kukukata. No. just unachukua total deni
 
Hiyo value retention fee iko kabisa kwenye makubaliano ya mkopo ambayo ulisaini kisha kuyatuma loan board via EMS kwaajili ya kujadili maombi yako. Mie nilitoa copy ya mkataba wenyewe nkabaki nao sikuona hicho kipengele lakini siku niliposikia hilo jambo niliamua kuurejea mkataba kwa kusoma all its content nkakuta hicho kipengele. That is a contract in a standard form you can either reject it or take it. Haukupi nafasi ya kunegotiate. Nadhani mtoa mada hukuupitia mkataba wakati wa kuutuma kama mie, thats why you seem to be surprised.
ni kipengele kipi katika mkataba kimetaja hiyo Value Retention Fee? kwenye mkataba wangu, sehemu ya 2.0 Kanuni na Masharti, kuanzia kipengele 2.1 hadi 2.16 (ambacho ndo cha mwisho) sijaona, embu nifungue macho tafadhali, kipo wapi hicho?
 
mkuu, kama upo Dar ungeenda pale bodi ya mikopo ni kitu cha dakika 10 tu wanakupa deni lako lote.

Jinsi ya kukokotoa kidogo ni changamoto ila unaweza jikadiria kwa position yangu:

Nimemaliza chuo mwaka 2013: Nimesomeshwa na bodi 100%.

>Jumla ya hela walizonipia: Mil 11.3 hivi
>Mwezi wa tano mwaka huu 2016 wameleta list kwa HR nadaiwa mil. 13

Ila nina karatasi yao inaomesha hesabu zote hadi hela kufika hapo. Nashauri ungeenda bodi sio kwamba ukienda wanaanza kukukata. No. just unachukua total deni
Asante Mkuu, tatizo nipo mkoani. Sio rahisi kufika, ila ikibidi nitafika. Deni langu nimeshapata kutoka Chuo nilichosoma, tatizo sijaelewa namna ya ukokotoaji wa hiyo Ada.
 
tatizo watu wanapeleka form kwa watendaji kusainiwa tu yale maandishi mengi nyuma ya form ya sheria za mkopo huo hawasomi wakaelewa ukoje baadae nikulalamika tu kumbe mwenyewe ulisaign umekubali mashart
 
mkuu, kama upo Dar ungeenda pale bodi ya mikopo ni kitu cha dakika 10 tu wanakupa deni lako lote.

Jinsi ya kukokotoa kidogo ni changamoto ila unaweza jikadiria kwa position yangu:

Nimemaliza chuo mwaka 2013: Nimesomeshwa na bodi 100%.

>Jumla ya hela walizonipia: Mil 11.3 hivi
>Mwezi wa tano mwaka huu 2016 wameleta list kwa HR nadaiwa mil. 13

Ila nina karatasi yao inaomesha hesabu zote hadi hela kufika hapo. Nashauri ungeenda bodi sio kwamba ukienda wanaanza kukukata. No. just unachukua total deni
mkuu walileta wenyewe kwa HR au ulienda kuwauliza deni lako ndo wakakuletea
 
tatizo watu wanapeleka form kwa watendaji kusainiwa tu yale maandishi mengi nyuma ya form ya sheria za mkopo huo hawasomi wakaelewa ukoje baadae nikulalamika tu kumbe mwenyewe ulisaign umekubali mashart
please madam, yawezekana tumesoma miaka tofauti na mikataba ipo tofauti, kama kwenye mkataba wako hicho kipengele chako kipo, naomba unijulishe ni kipi? yawezekana kwenye mikataba ya walioomba mikopo 2012/2013 haikuwepo. Nimesoma vizuri hayo masharti, sikuona.
 
Tufanye hivi. Wewe ulikopeshwa jumla ya shilingi laki moja (kwa miaka yote uliyosoma chuo).

Umemaliza chuo mwaka 2014 na mpaka leo hujaanza kulipa deni lako.

Kwahiyo, ukiongeza mwaka mmoja wa rehema, hautokuwa na tozo mpaka mwishoni mwa mwaka 2015.

Yaani, mpaka mwishoni mwa mwaka 2015, deni lako ni 100,000/= (bila tozo).

Kuanzia mwaka huu (2016), deni lako litakuwa hivi.....

Deni lako 100,000 + (value retention fee 100,000×6/100)+ (penalty 100,000×10/100)+(administration fee 100,000×1/100) = jumla 117,000/=

Tufanye mwaka huu ukaisha mpaka mwakani (2017) bila wewe kuanza kulipa deni, deni lako kwa mwaka 2017 litakuwa hivi...

Deni lako 117,000 + (value retention fee 100,000×6/100) = 123,000/=

"Value retention fee" itaendelea kuongezwa kwa mwaka mpaka pale utakapoanza kurejesha mkopo ndiyo wataacha kuiongeza!

Yaani, ukianza tu kurejesha deni lako, na tozo ya kutunza thamani inakoma!

Hivyo ndivyo ninavyoelewa mimi (inawezekana nakosea).

Jitahidi uende ofisi za HESLB watakupa maelezo ya kina pamoja na deni lako lote.
mimi nilihitimu 2014/2015. Grace period inaishia 1 DEC 2016. Nilichukua Customer Statement ya HESLB chuo niliposoma, nimekuta wameniwekea hiyo VRF kuanzia mwaka wa kwanza hadi wa pili wa masomo.

Sasa ukiangalia, 1st year, jumla ya fedha ilikuwa 3,832,500/= Value Retention Fee wamejaza 459,900/= sielewi walivyokokotoa.
 
Back
Top Bottom