Valentine Story! Guess Who Is Getting Married? Marriage games

Valentine Story! Guess Who Is Getting Married? Marriage games

Eiiiishhhh @lara1 [emoji19] [emoji19] [emoji19] [emoji19] , nimesikitika, nimecheka, nimefurahi, nimesmile, nimesonya , mwisho nikachelewa kumpikia baba mwenye nyumba. Itabidi leo tukale huko duniani aaaiii[emoji27] .
 
lara 1 njooooooo, yani nimekaa nasubiri, hadi baba chanja huku anauliza nasubiri nn, mbona silali uwiiiiii
 
THE END OF ONE THING IS THE BEGGINING OF ANOTHER!!

Basi Sisca akamwambia, i am pregnant tooo! Anny akamwambia i am happy for you. Harusi lini? Sisca akmwambia shogaaaa hamna harusi, we just gonna have a baby! Isnt it wonderful! Anny akamwambia it is not! You deserve better, you saved yourself so much to deserve this! Atleast i got to wear the white dress once. Not that ina cha maana, just that every ladies dream is to wear it atlest ones.

Sikia Sisca usikubali, tufosi kingi, yeye si hataki harusi? Si tunakufanyia bridal shower, na sendoff afu kama mbabe asifanye harusii. Tunaalika mji mzimaa. Hahahaaaaa! Dont let him destroy your dreams easily, put up a fight unamlelea lea sanaaa. Ashakugeuzaaa godorooo kukulala kichwani. Its is not fare.

Sisca akmwambia umri wenyewe huu, bora hata nina huyo mwanaume, atleast im not gonna be a single mother on the bright side. Ill have a family! Not quite as i planned but it is something better than nothing. Anny aksemaa hapo kwenye usinhle mother ndo kutaponihusuuuu. Hahaaaaaa! Wakachekaaaa.

Anny akaja kumwambia Mangi, bwana kuna blander tulifanyaa, imejibuuuu. Mangi kafurahiiii, akamwambia nataka kuja kukuoa. Anny akamwambia sina uhakika, ujue nishaolewaga nikashindwa, mara pili ikawa nusra, nusra almanusraaa, niolewe tenaaa. Sasa hivi im not so sureee. Cant we just have this baby! Out of wedlock!

Akamwambia sikia najua unasitaaa, ila kuna leo na keshooo, sis wachaga bwanaa. Siku sipo, watakunyanganya mali na mtoto ubakie unashangaaa. Mi sitaki mwanangu aende kuomba jasho langu kwa nguvu zangu mburaaaaaahhhhhh! Hapa harusi lazimaaa.

Anny anamwambia mimi im not comfortable, wewe hujawahi kuoa and all, watu wataongea sanaaa, anamuoa mtalaka, mara alichumbiwa na babu. I am not suree i can handle all that pressure na mimba hii. !Mangi akamwambia basi tufunge ndoa ya wawili tu bomaniiii.

Anny akamwambia Mangi, tuishiii tu baby, kama Mungu kapanga kuishi tutabariki ndoa mbele kwa mbele but another wedding no baby! Not me again. Najua hapa wataongea kaoa ila kuja kunitoa ndani kwako hawaweziii. Hahahaaaa! Mangi akakubali kishingo upandeeee.

Basi wakawa close na Sisca wote na vitumbooo. Angy anawacheka tu, hapo anakaa na captain karelax, ashafunga ndoa yake ya beach kwa ushawishi wa Anny ile idea yake. The vows are just wow! Kila mtu kamuandikia mwenzie vows zake! So magnificient. Wakaenda na bomaniiii. Akawa ana rahaaaa.

Captain mstaarabu, na wanae wawili, na yule Ty kamlea vizuri, yaniii akajutia mda aliopoteza na yule boyaaa. Captain anarudi kula mchanaaa, wanafanya home work wote na watoto wao, anawasimilia story, wanasali wote siku ingine anapikaaa. They were homeee.

Mpaka akawa anaboa Angy, akienda meeting na mashosti kidogooo nawahi kumuandalia mume wanguuu! Shogaaaaa! Mumeo huyo mume wa kwanzaaa! Tufanye hiki siku flani, nina plans na mume wanguu. Loooo! Mume huyo vepeeeeeeeee! Ndo kapata mtu wa kumpenda akapendekaaa, basi ndo inakuwa addiction ya penziii.

Akaanza kuumwa umwaaa, kwenda hospital mimbaaa, ya twinsss. Akafurahii watoto wao na shoga zake watalinganaaa. Akawaambia wakawa wanakula wote embeee. Kila mtu kamimbikaaaa. Ikatokea complication kwa Anny, akaambiwa mimba ya mapacha , ila kutokana na kizazi hakina nguvuuuu, kwa mambo yake yaleee, itabidi ashonweee huko kw bibi, miezi tisaaa. Kuzaa operation, afu ndo atafumuliwa, na mda wote bedrest.

Akawa anaogopaaaa anawazaa, isije kutoka jamani twins wake. Ila captain was so supportive, mda wote yupo bega kwa bega, anamtia moyo hawawezi kutoka, usiji stress Mungu mkubwaaaaa.

Ikawa wakikaa wanagombania majinaaa. Jina hili nimeliwahi. Anny nikizaa wa kiume nachukua hilo la Tyron, nikizaa wa kike nachukua Melissa. Angy na mimi Tyron nalitaka, nikipata wote wakiume inakuwa Tyron na Tyrese. Hahaaaa! Sisca yupo mimi hata sichagui jina, asipopewa jina la mama mkwe sijuiii. Akitoka wa kike lazima amuite jina mama yake Tatu Shabani! Hahaaaa! Anny yupo hio si namba jamaniii! Hahaaaaa!

Wakawa wanamstress Sisca wafanye ile bridal shower bila hata harusiii. Akawazaa akana kwa KLM sio sehemu ya kubeep anaweza hata kumsusa mtoto kisa bridal shower. Hahaaaa! Akawa ashakubai harusibtena maisha haya yeye basi tenaaa.

Siku ya siku mimba ina miezi 3, KLM anamwambia nataka niletemshenga kwenu nilipe mahari, hii safari ndefu, mzee wako hashindwi kunisusia maiti. Uzuri wa mahari, ukinitibua nadai changu choote! Hahahaaaa! Na faini juu.

Kina Anny wakasema sasa ile bridal shower ndo mwakeee. !Mila zitaturuhusuuuu, si ushaolewa kimilaaa. Loooooh! Hahahaaaa! Wakaenda kuposa, posa ikapokelewa mahari Milioni 6. Tobaaaaa! Sisca akasemambasi tena KLM hatoi. Wakaaga akawalaumu sanaa wazazi wake si kwa mahari ileee! Akaambiwa ashakutia mimba katuchafulia ukoo, faini tu mil 2, bado mkaja wa mama, mwenyewe ulizaliwa njiti kwa hio mkaja haushuki milioni, mama yako alikandwa maji mengi sanaaa. Za kukusomeshaaa, bado faini ya wajombaaa. Milioni 6 halali kabisaaa.

Akajuuta kuwafahamuu. Hawezi basiiiii apunguze tumkopeshe mke, kama mke anakopeshwaaa. Atatumalizia kidogo kidogo. Washenga wenyewe wakawa wanalalamika si kwa milioni 6. Mke mwenyewe bibi. Hahahaaaa!

Basi anamwambia walipe 1 million tu, zingine potezea, KLM akamuuliza kwa hio nikukopeee? Hahahaaa! Sisca ananyamaza. Basi nikuchangie Milion 3. KLM akamjibu ili uje seme ulijioa kwa hela zako. Siku waliopangiwa kimyaaa hawakurudi. Sisca akajua basi tenaaa. Akawa anataka arudi zake kwake kwa KLM jumapili baada ya jmosi kuchomeshwa mahindi.

Asubuhi akamwambia usirudi nakuja hukoo na bi mkubwa na mjombaa. Akawa anawaza KLM kwa ujeuri wake atatoa hata laki 5 azingue. Tumbo jotooo. Sababu jana walipika afu hawakuja, baba ake akaema hamna kazi mara mbili, hatupiki chochote leo. Wala bia sinunui. Waje wasije watajijua.

Saa kumi wakaja watu kibaooo. Mjomba mtu ndo mshengaaa. Mama Sisca akaona soo akaenda kukopa bia kwa Mangi, maana ilishaanza kuwa aibu mjue. Bia moja mojaa. Wakaanza kushusha kreti, kwenye gari hatariiiii. Wanajisevia wanawapa na majirani na nini sio ishu. Watu walikoga bia, mi Jackdaniels red lebel za kutosha, black lebel za kutoshaaa.

Sisca akaitwa unamjua huyu? Ndio namjua? Nani? Anaona aibu, mpenzi wangu! Akaambiwa haya nendaa. Mshenga aaknza ooh tupunguzieni kidogooo, tunataka kuoa, hali ya maisha. Mzee akawaambia haipungui labda mpungue niwakopeshe mke, kama mke anakopeshwaaa! Khaaaaaa! Maneno gani tena hayoooo mkwe.

Wakauliza mahari bei gani? Milioni 6! Anapokea nani? Baba mzazi. Wakashusha kimalborooo. Baba akawauliza mnapunguza ngapi tuandikishane? Wakamwambia wewe pokea tutakapoishia ndo hapo hapo. Akasema sawa.

Burungutu 6 cash, million sita cash! Watu wananongonaaaa. Tumeeeee! Wamemalizaaa! Si kwa mahari ileee. Baba akarudisha million! Wakamuulia vipi mzee? Oooooh mahari haimalizwi, lazima tuwadai. Lazimaibaki tunawadai, mkimaliza yote kama tumeuuza mtoto. Mjomba akagomaa, akachomoa 10,000 tu, basi mtatudai hii 10,000.

Basi watu vifijooo, akaitwa akavishwa peteee. Picha na nini, ndo ndoa hivoooooo. Akawa karudi kakwe. Kina Anny wanamwambia sasa ile bridal shower vipi? Sisca anawaambia mnataka nidaiwe milion 6 za watu. Thubutuuuuu! Yani hapa nimekuwa nanadabu hatariii, si kwa mahari ile. Hahaaaaa!

Siku hio ana hili wala lile anamwambia twende tukaandikishe harusi kanisani? Akauliza eeeeh! Hujanisikia au? Aaaasijaelewa! Akamwambia kwa mahari ya milioni 6 ulitegemea sitokufung mpaka kifo kitutenganishe? Hahahahaaa! Sisca akawa hajui yupo serious au anatania. Akajibu hayaaaa! Akawa haamini.

Akamwambia chagua tarehe mwezi huu huu, sitaki mimba ifike miezi 5. Sisca akataja tu anajua mizinguooo. Jumamosi wkaenda akaandikisha kweli parokia yao. Akawa haamini, akaenda kanisani tu asikie tangazo la kwanza linasomwaa! Akaenda na kin Anny na Angy na mitumbo yao. Wakaangaliana. Almanusra washangilie katikati ya misaa.

Anny mamashughuli hatuna mda kabisaa, siku zimeishaa inabidi gauni, sijui nini. Vikao tutakaa lini? Akaensa kuwaambia kwao wakanuna sendoff gani ndani ya mwezi jamanii. Ila akawaambia yeye kama yeye kajiandaa, watakapoishia ataongezea. Baba mtu yupo bora hata ile m6 ipo sio kwa makusudi hayaaaa.

KLM yeye ana watu wake kwama 30 hivi wampa support ya nguvuu,,vijana wa mjini, aliokusanya mama yake niongezaa tu.

Ilivobaji wiki Sisca akamuuliza imekywaje umebadili mawazo juu ya harusi ndo kusema m6 zimekuuma sanaa au? Hahaaa! Manake nishakata tamaa ujue, yaani ulijua kuninyima rahaaaaa si kidogo.

KLM akamwambia ulijua kweli nakuweka suriaa, tunazaa wana haramu? Hahahaa! Hamnaaa! Nisingeweza kufanya hivo. Mimi i wanted to be certain kama unataka ndoa na mimi au harusiiii. Wanawake wengi mnapenda harusiiii, ndoa hampendiii, nikaamua kukupima je harusi isipokuwepo utakuwa mtu wa aina gani? Uzuri hukubadilikaaa. Nibgekwambia nitakuoa kwa mahari ya m6, harusi kubwa na hivi vyote ungejinyenyekeza si kidogo ili upate hio harusiii. A woman who asks for nothing deserves everything. And you are that woman. Think beyond the wedding, think us! Harusi ni kitu cha kupitaaa tuuu.

Wanawake wengi mliosomaa kidogo ningewaambia nizalie afu basi wasingekubali, ila hao hao ningewaambia nitakuoa kwa m6, harusi ya 50m hakuna amabe angekataa, wakati ni mtu yule yule naeombaaa. You deserve this baby, enjoy your day ikifikaaa.

Ila ukae ukijua siku zote mimi ni yule yule KLM, ukinizingua UTAISOMA NAMBA!

THE END!


KATIKA KUBORESHAAA, SEMA NANI KAKUKUNA ZAIDI NA WAPIII! NI NANI EPISODE IPI NI BEST OF THE BEST KWAKO! Nitashukuru for feedback!
 
Mm mpaka nishagombana na mr.analalamika mbona simu siwek chin
 
Back
Top Bottom