Vacancies-deadline 31Dec 09 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vacancies-deadline 31Dec 09

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by carmel, Dec 22, 2009.

 1. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #1
  Dec 22, 2009
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  JAMHURIYA MUUNGANO WA TANZANIA
  OFISI YA WAZIRI MKUU
  TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
  HALMASHAURI YA WILAYA YA LIWALE

  Fax No: 0732933131/0732933118 S.L.P. 23,
  E-mail:liwale.district@yahoo.com LIWALE.

  Kumb. Na. LW/DC/L.20/10 VOL.IV/11 26.11.2009
  YAH: TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

  Katibu wa Bodi ya Ajira ya Halmashauri ya Wilaya ya Liwale Mkoa wa Lindi anawatangazia wananchi wote wenye sifa zilizoainishwa kuomba nafasi za ajira mpya kwa mwaka wa fedha wa 2009/2010 kama ifuatavyo:-

  1. Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja la II (Records Management Assistant II) – Nafasi 1
  SIFA
  · Awe kidato cha sita wenye cheti cha utunzaji kumbukumbu katika mojawapo ya fani za Afya, Masjala, Mahakama na Ardhi.

  Majukumu ya kazi
  · Kutafuta kumbukumbu/nyaraka/mafaili yanayohitajiwa na wasomaji
  · Kudhibiti upokeaji, uandikishaji wa kumbukumbu/nyaraka

  Mshahara:
  Mshahara uko katika ngazi ya Mshahara ya TGS. B sawa na Tshs. 151,240/= kwa mwezi

  2. Katibu Mahsusi Daraja III (Personal Secretary III) – Nafasi I
  SIFA
  Awe kidato cha Nne waliohduhuria Mafunzo ya Uhazili na kufaulu mtihani wa Hatua ya Tatu. Wawe wamefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 80 kwa dakika moja na wawe wamepata mafunzo ya Kompyuta kutoka Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali na kupat cheti katika Programu za Windows, Microsoft Office, Internet, E-mail na Publisher.

  Majukumu ya kazi
  · Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida
  · Kusaidia kupokea wageni na kuwasaili shida zao, na kuwaelekeza sehemu wanapoweza kushughulikiwa
  · Kusaidia kutunza taarifa/kumbukumbu za matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba ya kazi zingine zilizopangwa kutekelezwa katika Ofisi anamofanyika kazi, na kumuarifu Mkuu wake kwa wakati unaohitajika
  · Kusaidia kutafuta na kumpatia Mkuu wake majalada, nyaraka au kitu chochote kinachohitajika katika shughuli za kazi hapo ofisini

  Mshahara:
  Mshahara uko katika ngazi ya Mshahara ya TGS. B sawa na Tshs. 151,240/= kwa mwezi

  3. Afisa Mtendaji Kata III ( Ward Executive Officer III ) – Nafasi 1
  SIFA
  Awe amehitimu kidato cha nne (IV) na (VI) na kuhudhuria mafunzo ya Stashahada ya aina yoyote na kufaulu usaili.

  Majukumu ya kazi
  · Atakuwa Mtendaji Mkuu wa Kata na kiungo cha Uongozi kwa Idara zote katika Kata na atashughulikia masuala yote ya Kata
  · Atakuwa mhamasishaji wa Umma katika mikakati mbalimbali ya uzalishaji mali, kuondoa njaa na umaskini.
  · Atakuwa mlinzi wa amani na msimamizi wa Utawala bora katika Kata
  · Atakuwa ni Katibu wa Kamati ya Maendeleo ya Kata

  Mshahara:
  Mshahara uko katika ngazi ya Mshahara ya TGS. C sawa na Tshs. 201,870/= kwa mwezi

  4. Afisa Mtendaji Kijiji - III ( Village Executive Officer - III ) – Nafasi 20
  SIFA
  Awe amehitimu kidato cha IV na VI waliohitimu Stashahada katika Fani yoyote ya chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali na kufaulu usaili.

  Majukumu ya kazi
  · Atakuwa Mtendaji na Mshauri Mkuu wa Serikali ya Kijiji na Kamati zake katika Mipango ya Maendeleo ya Kijamii na utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo
  · Atakuwa Afisa Mhasibu wa Serikali ya Kijiji na atasimamia mapato na matumizi ya Serikali ya Kijiji.
  · Atakuwa Mlinzi wa Amani na Msimamizi wa Utawala bora katika Kijiji
  · Ataratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo ya Kijiji

  Mshahara:
  Mshahara uko katika ngazi ya Mshahara ya TGS. A sawa na Tshs. 114,910/= kwa mwezi

  5. Afisa Maendeleo ya Jamii Daraja la II (Community Development Officer II) – Nafasi 5
  SIFA
  · Awe na Stashahada ya Juu ya Maendeleo ya Jamii kutoka Chuo cha Maendeleo ya Jamii, Tengeru, au vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali.
  · Awe na Shahada ya kwanza kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, SUA, au Vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali katika fani ya:-
  o Community Development – (Maendeleo ya Jamii)
  o Sociology (Elimu Jamii)
  o Home Economics (Maendeleo Vijijini)
  o Rural Development Planning (Mipango ya Maendeleo Vijijini)
  o Environment Economics (Uchumi wa Maendeleo)
  o Gender in Development (Maendeleo ya Jinsia)

  Majukumu ya kazi
  · Kushirikisha jamii katika kubuni na kupanga miradi mbalimbali katika kata wanazofanyia kazi.
  · Kuongoza na kusimamia utekelezaji wa Mipango/Miradi ya Maendeleo katika Kata zao, kwa kushirikiana Maafisa Maendeleo ya Jamii Wasaidizi
  · Kufanya utafiti na kutoa mapendekezo ya namna ya kukabiliana na matatizo mbalimbali ya maendeleo yanayorudisha nyumba maendeleo ya jamii kwa kushirikiana na watumishi wa sekta nyingine.
  · Kuongeza na kusimamia utendaji kazi wa Maafisa Maendeleo ya Jamii Wasaidizi walioko katika vijiji/kata

  Mshahara:
  Mshahara uko katika ngazi ya Mshahara ya TGS. D sawa na Tshs. 322,460/= kwa mwezi

  6. Afisa Ustawi wa Jamii II (Social Welfare Officer Grade II) – Nafasi 1
  SIFA
  · Awe na Shahada ya Kwanza (B.A. in Social Work or Sociology) au Stashahada ya Juu ya Ustawi wa Jamii (Advanced Diploma in Social Work) kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.

  Majukumu ya kazi
  · Kuendesha usaili kwa wahudhumiwa (watu wenye ulemavu, wazee, familia zenye matatizo, watoto na washtakiwa)
  · Kufanya ukaguzi wa mazingira wanaoyoishi wahudhumiwa ili kupata taarifa zao kamili
  · Kuandaa taarifa za usaili na ukaguzi wa mazingira ya wahudumiwa
  · Kupokea na kukusanya taarifa za Ustawi wa Jamii kutoka kwa wadau na vituo mbalimbali vya Ustawi wa Jamii

  Mshahara:
  Mshahara uko katika ngazi ya Mshahara ya TGS. D sawa na Tshs. 322,460/= kwa mwezi

  7. Afisa Ugavi Daraja la II (Supplies Officer II) – Nafasi 2
  SIFA
  · Awe na Shahada ya Biashara (B. Comm) yenye mchepuo wa ugavi au Stashahada ya Juu ya Ugavi (Advance Diploma in Materials Management inayotolewa na Chuo kinachotambuliwa na Bodi ya Taifa ya Usimamizi wa Vifaa.

  Majukumu ya kazi
  · Kukusanya takwimu za kusaidia kutayarishwa makisio ya vifaa vinavyohitajika (Material Requirement Budget) na Mpango wa Ununuzi (Procurement Plan)
  · Kukusanya na kutunza takwimu za utendaji wa Wazabuni mbalimbali
  · Kukusanya na kutunza takwimu za upokeaji, utunzaji na usambazaji wa vifaa
  · Kusimamia utunzaji wa maghala na hati/kumbukumbu ya vifaa vilivyomo ghalani.
  ·

  Mshahara:
  Mshahara uko katika ngazi ya Mshahara ya TGS. C/D sawa na Tshs. 201,870/ 322,460/= kwa mwezi

  8. Mlinzi (Security Guard) Nafasi 2
  SIFA
  Awe amehitimu kidato cha Nne ambao wamefuzu mafunzo ya Mgambo / Polisi/ JKT au mafunzo ya zimamoto kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali

  Majukumu ya kazi
  · Kuhakikisha kwamba mali yoyote ya Ofisi inayotolewa langoni (nje ya ofisi) ina hati ya idhini
  · Kuhakikisha kuwa mali yote inayoingizwa langoni inazo hati za uhalali wake
  · Kulinda usalama wa majengo, ofisi na mali za ofisi mchana na usiku
  · Kuhakikisha kwamba milango na madirisha yote yamefungwa ipasavyo mwisho wa saa za kazi

  Mshahara:
  Mshahara uko katika ngazi ya Mshahara ya TGOS. A sawa na Tshs. 104,410/= kwa mwezi

  9. Mwalimu III ( Teacher III ) – Nafasi 4
  SIFA
  Awe amehitimu mtihani wa Taifa wa kidato cha Nne ambao wamefuzu mafunzo ya Ualimu ya miaka miwili (2) na kupata cheti cha Ualimu daraja la IIIA

  Majukumu ya kazi
  · Kufundisha masomo aliyosomea Chuoni katika Shule za Awali au Shule za Msingi
  · Kuandaa maazimio ya kazi, maandalio ya masomo, zana za kufundishia / kujifunzia, mazoezi ya wanafunzi, majaribio na mitihani
  · Kusahihisha kazi za wanafunzi
  · Kutathmini Maendeleo ya wanafunzi


  Mshahara:
  Mshahara uko katika ngazi ya Mshahara ya TGTS. B sawa na Tshs. 170,700/= kwa mwezi

  10. Afisa Misitu Daraja la II (Forest Officer II) – Nafasi 1
  SIFA
  · Awe na Shahada ya Misitu kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine au Vyuo Vikuu vingine vinavyotambuliwa na Serikali

  Majukumu ya kazi
  · Kusimamia upandaji wa uhudumiaji wa miti na misitu
  · Kusimamia uendelezaji wa misitu ya kupandwa isiyozidi hekta 5,000 au ya asili isiyozidi hekta 10,000
  · Kufanya utafiti wa misitu
  · Kutekeleza Sera na Sheria za misitu

  Mshahara:
  Mshahara uko katika ngazi ya Mshahara ya TGS. D sawa na Tshs. 322,460/= kwa mwezi
  11. Msaidizi Misitu Daraja la II (Forest Assistant II) – Nafasi 9
  SIFA
  · Awe na Elimu ya Kidato cha nne au sita mwenye Astashahada (Cheti) au Stashahada ya misitu kutoka Vyuo vinavyotambukliwa na Serikali.

  Majukumu ya kazi
  · Kukusanya mbegu
  · Kuhudhumia na kutunza bustani za miti
  · Kutunza na kuhudumia miti na misitu
  · Kufanya doria

  Mshahara:
  Mshahara uko katika ngazi ya Mshahara ya TGS. B/C sawa na Tshs. 151,240/201,870/= kwa mwezi

  12. Afisa Wanyamapori Daraja II (Game Officer II) – Nafasi I
  SIFA
  Awe na Shahada ya Sayansi ya Wanyamapori kutoka Chuo Kikuu kinachotambuliwa na Serikali.

  Majukumu ya kazi
  · Kutekeleza kazi za ushirikishaji wadau katika uhifadhi
  · Kudhibiti utoaji wa leseni za biashara ya nyara na vibali vya kukamata wanyama hai
  · Kushiriki katika kusuluhisha migogoro ya matumizi ya wanyamapori
  · Kudhibiti matumizi haramu ya leseni za uwindaji na kuhakikisha kufuatwa kwa maadili katika kutumia wanyamapori

  Mshahara:
  Mshahara uko katika ngazi ya Mshahara ya TGS. D sawa na Tshs. 322,460/= kwa mwezi

  13. Mhifadhi Wanyamapori Daraja la II (Game Warden) – Nafasi 10
  SIFA
  · Awe amehitimu kidato cha nne (IV) au kidato (VI), wenye Stashahada ya Uhifadhi wa Wanyamapori kutoka Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Mweka au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali, na wenye uzoefu wa kazi kwa muda usiopingua miaka mitatu.

  Majukumu ya kazi
  · Kutekeleza kazi za ushirikishaji wadau katika uhifadhi
  · Kudhibiti utoaji wa leseni za biashara ya nyara na vibali vya kukamata wanyama hai
  · Kushiriki katika kusuluhisha migogoro ya matumizi ya wanyamapori
  · Kudhibiti matumizi haramu ya leseni za uwindaji na kuhakikisha kufuatwa kwa maadili katika kutumia wanyamapori

  Mshahara:
  Mshahara uko katika ngazi ya Mshahara ya TGS. B & C sawa na Tshs. 151,240/201,870/= kwa mwezi


  14. Afisa Ufugaji Nyuki Daraja la II (Beekeeping Officer II) – Nafasi 1
  SIFA
  · Awe na shahada katika fani ya Ufugaji Nyuki au Sayansi ya Elimu ya Mimea, Elimu ya Wadudu au Elimu ya Wanyama kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam au Vyuo vingine vinavyotambulika na Serikali

  Majukumu ya kazi
  · Kusimamia uanzishaji wa hifadhi za nyuki na manzuki
  · Kutangaza Sera na Sheria za ufugaji nyuki
  · Kufundisha masomo ya fani ya ufugaji nyuki
  · Kukusanya takwimu za rasilimali na ufugaji nyuki
  · Kupanga na kupima ubora wa mazao ya nyuki

  Mshahara:
  Mshahara uko katika ngazi ya Mshahara ya TGS. D sawa na Tshs. 322,460/= kwa mwezi

  15. Msaidizi Ufugaji Nyuki Daraja la II (Beekeeping Asst.) – Nafasi 3
  SIFA
  · Awe umehitimu kidato cha nne au sita wenye Astashahada (Cheti) au Stashahada (Diploma) ya Ufugaji Nyuki kutoka katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali

  Majukumu ya kazi
  · Kusimamia Manzuki
  · Kutunza hifadhi za nyuki
  · Kuondoa nyuki wanaodhuru binadamu na mifugo
  · Kukukusanya takwimu za ufugaji nyuki

  Mshahara:
  Mshahara uko katika ngazi ya Mshahara ya TGS. B/C sawa na Tshs. 151,240/201,870/= kwa mwezi

  16. Mpima Ardhi Daraja la II (Land Surveyor) - Nafasi 1
  SIFA
  · Awe na Stashahada ya juu/Shahada kutoka chuo Kikuu Kishiriki cha Ardhi na Usanifu Majengo (UCLAS) katika fani ya Upimaji Ardhi au Taasisi yoyote inazotambuliwa na National Council of Professional Surveyors (NCPS)
  · Awe mwenye cheti cha East African Land Survey (EALSC) au National Council of Professional Surveyors Certificate (NCPSC) katika fani ya upimaji ardhi.

  Majukumu ya kazi
  · Kukagua masuala ya upimaji katika Halmashauri
  · Kukagua kazi za upimaji na kuingiza taarifa za kazi zilizothibitishwa kwenye kompyuta.
  · Kufanya kazi za nje ya Ofisi (field survey operations) chini ya usimamizi wa mpima aliyesajiliwa
  · Kuingiza taarifa za Upimaji (alpha numeric data) kwenye kompyuta

  Mshahara:
  Mshahara uko katika ngazi ya Mshahara ya TGS. D sawa na Tshs. 322,460/= kwa mwezi

  17. Mthamini Daraja la II (Valuer II) – Nafasi 1
  SIFA
  · Awe na Shahada/Stashahada ya juu katika fani ya Land Management and Valuation kutoka Chuo Kikuu Kishiriki cha Ardhi na Usanifu Majengo (UCLAS) au Taasisi nyingine zinazotambuliwa na Serikali katika fani za Usimamizi Ardhi na Uthamini.
  · Awe mwenye cheti cha NCPS katika fani ya Usimamizi Ardhi na Uthamini.

  Majukumu ya kazi
  · Kukusanya taarifa za utafiti na mwenendo wa soko la ardhi
  · Kuhakiki kumbukumbu za utafiti na kuziingiza kwenye kompyuta
  · Kufanya uthamini kwa madhumuni mbalimbali
  · Kuongeza na kusimamia utekelezaji wa tafiti

  Mshahara:
  Mshahara uko katika ngazi ya Mshahara ya TGS. E sawa na Tshs. 408,560/= kwa mwezi

  18. Afisa Kilimo Msaidizi (Assistant Agricultural Field Officer II) – Nafasi 1
  SIFA
  · Awe amehitimu Kidato cha Sita (VI) wenye stashahada ya kilimo kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.

  Majukumu ya kazi
  · Kushirikiana na watafiti kuendesha vishamba vya majaribio
  · Kukusanya/kuhifadhi takwimu za majaribio
  · Kuwafundisha wakulima mbinu za kilimo bora
  · Kuwafikishia wakulima matokeo ya utafiti

  Mshahara:
  Mshahara uko katika ngazi ya Mshahara ya TGS. B sawa na Tshs. 151,240/= kwa mwezi

  19. Fundi Sanifu II (Water Technician II Civil, Haidrojia, electrical) – Nafasi 5
  SIFA
  · Awe na Elimu ya Kidato cha nne au sita mwenye kuhitimu Vyuo vya Ufundi vinavyota mbuliwa na Serikali ambao wana cheti cha Ufundi (FTC) na wenye uzoefu wa kazi kwa muda usiopungua miaka mitano na ujuzi wa kutumia kompyuta.

  Majukumu ya kazi
  · Ukusanyaji na ukaguaji takwimu za maji
  · Kutunza takwimu za maji
  · Kufanya ukaguzi wa vyanzo vya maji pamoja na kuchukua sampuli
  · Kufanya utafiti wa maji Ardhini
  · Ujenzi wa visima vya Maji

  Mshahara:
  Mshahara uko katika ngazi ya Mshahara ya TGS. C sawa na Tshs. 201,870/= kwa mwezi

  20. Tabibu II (Clinical Officer II) – Nafasi 1
  SIFA
  · Awe amehitimu kidato cha nne (IV) au sita (VI) waliofaulu kozi ya Stashahada ya miaka miwili (kidato cha sita) au miaka mitatu (kidato cha nne) katika chuo kinachotambuliwa na Serikali

  Majukumu ya kazi
  · Kazi zote zinazofanywa na Tabibu Msaidizi
  · Kutambua na kutibu magonjwa ya kawaida
  · Kusimamia utendaji wa watumishi walio chini yake na kufanya upasuaji mdogo
  · Kutoa elimu ya Afya kwa Jamii

  Mshahara:
  Mshahara uko katika ngazi ya Mshahara ya TGS. B sawa na Tshs. 200,520/= kwa mwezi

  21. Muuguzi II (Nurse II) – Nafasi 1
  SIFA
  · Kubadilishwa kazi Wakunga Wasaidizi Vijijini (MCHA) waliofuzu mafunzo ya miaka miwili ya MCHA na kutunikiwa cheti.

  Majukumu ya kazi
  · Kutoa huduma kwa mama wajawazito watoto na wagonjwa wengine katika Zahanati na Jamii kwa ujumla
  · Kutoa elimu ya afya kwa jamii kuhusu afya ya uzazi na uzazi salama
  · Kutembelea jamii ili kutathmini afya ya familia na mazingira
  · Kukusanya taarifa na kuziwasilisha kwa mkuu wa kituo

  Mshahara:
  Mshahara uko katika ngazi ya Mshahara ya TGHS. B sawa na Tshs. 200,520/= kwa mwezi

  22. Mhudumu wa Afya II ( Medical Attendant II ) – Nafasi 8
  SIFA
  Awe amehitimu kidato cha nne amesoma mwaka mmoja uhudumu wa Afya na wenye uzoefu wa kazi za uhudumu kwa muda usiopungua miaka miwili katika mojawapo ya fani au sehemu zifuatavyo:-
  · Uuguzi
  · Maabara
  · Meno
  · Mionzi
  · Mzoeza Viungo
  · Viungo Bandia
  · Uchanganya Madawa
  · Afya ya Mazingira
  · Chumba cha Maiti, na fani/sehemu nyingine zinazohusiana na afya  Majukumu ya kazi
  · Kufanya usafi wa vifaa vya kazi usafi wa wodi na mazingira
  · Kusaidia wagonjwa wenye ulemavu na wasiojiweza katika kwenda haja (kubwa na ndogo) na kuoga
  · Kupokea na kutunza sampuli za maabara
  · Kufanya usafi na kutunza vifaa vya huduma za kinywa na meno
  · Kupokea na kutunza picha za mionzi na madawa ya shughuli za Mionzi
  · Kufanya usafi wa wodi, kiliniki za Wazoeza viungo
  · Kuwasafirisha wagonjwa kai ya wodi na Idara ya mazoezi ya viungo
  · Kupokea, kuosha na kutunza maiti


  Mshahara:
  Mshahara uko katika ngazi ya Mshahara ya TGHOS A sawa na Tshs. 134,100/= kwa mwezi

  SIFA ZA JUMLA ZA WAOMBAJI
  · Awe raia wa Tanzania
  · Awe na umri usiozidi miaka 40
  · Awe na Elimu ya Kidato cha Nne (IV) na kuendelea

  Mambo ya kuzingatia
  · Barua za maombi zilizoandikwa kwa mkono (hand – written) ziambatanishwe na vivuli vya vyeti vya taaluma/mafunzo
  · Picha ya “passport size”
  · Namba ya simu kama ipo

  Utaratibu wa kutuma Maombi
  Maombi yote yatumwe kwa:-
  Mkurugenzi Mtendaji (W),
  S.L.P. 23,
  LIWALE.

  NB:
  · Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 31/12/2009 saa 9.30 Alasiri.
  · Halmashauri itakuwa tayari kumruhusu mtumishi kuomba uhamisho baada ya kufikisha miaka mitatu ya Utumishi wake.
  Mbujilo G.M.,
  Kny: KATIBU WA BODI YA AJIRA
  LIWALE
   
 2. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #2
  Dec 22, 2009
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  TGOS,TGHOS & TGS. C shemu safi sana lakini maneno niliyoanza nayo hapo ndio yanakatisha tamaa kusema kweli japo nashida ya kazi sana nitaishia kuomba rushwa ili mtoto asome.
   
 3. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #3
  Dec 22, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  HALAFU MIMI NINA WASIWASI NA HII TAALUMA YANGU!sijawahi kuona tangazo la kazi kwa taaluma yangu zaidi ya nafasi za jeshini!:D
   
 4. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #4
  Dec 22, 2009
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Umesoma nini? kulipua mabomu? au ulisoma SUA upande wa kufundisha panya kutegua mabomu?
   
 5. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #5
  Dec 22, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  we nguli wewe!haya

  kuna kozi zingine hapa tunasubiri tu idara zifuatazo zitubebe kwa mbeleko zao:
  1-usalama wa taifa
  2-jeshi la polisi
  3-jkt
  4-jwtz

  mi sijawahi soma tangazo la kazi wanamtaka ARCHITECT,wala Q.S
   
 6. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #6
  Dec 22, 2009
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Hata mimi sijawahi ona gazeti linatangaza kazi za mtu aliyesoma archaeology/philosophy so we are in the same page na ndio maana mpaka leo nafanya kazi kwenye internet cafe [​IMG][​IMG]
   
 7. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #7
  Dec 22, 2009
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  teh teh teh, hauko peke yako...
   
 8. Azikiwe

  Azikiwe Senior Member

  #8
  Dec 22, 2009
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 191
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Naona mnaleta utani na course za watu, enh?
   
 9. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #9
  Dec 22, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Kwi kwi kwi, kumbe siko peke yangu Geoff,
  Wewe ni kama mimi, manake kazi niliyosomea ni uwaziri, lakini bahati mbaya haijawahi kutangazwa hata siku moja, rais anaishia tu kufanya usaili peke yake bila kutangaza kazi.
   
 10. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #10
  Dec 22, 2009
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Msijali, hizo taaluma zenu zitapata mahali tu ili ziwe useful. so far Nguli we endelea kufanya hapo internet cafe, atleast unapata free access to JF everyday.
  Na Geof, nitafute badae nikuunganishe usalama wa taifa
   
 11. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #11
  Dec 22, 2009
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Na hizi TGSD NA C zitatuingiza majaribuni kwenye kuomba rushwa hadi ya buku kudadeki, ili mradi tu watoto waende msalani.
   
 12. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #12
  Dec 22, 2009
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Mh! usinipotezee mpwa tafadhali bora aendelee hapo alipo tu na Mungu atamsaidia.
   
 13. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #13
  Dec 22, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kama ulishafanya kazi private secta ni ngumu sana kuingia uku na kukaa kwa amani lazima tu utahujumu uchumi wa nchi ila kama umeanzia uku angalau unakuwa unaipenda nchi yako
   
 14. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #14
  Dec 22, 2009
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,937
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Hivi jamani asiye bahati kweli habahatishi.unataka Mungu akupe nini? gunia la chawa ujikune mwaka mzima? Hivi kuna AJIRA IPI NZURI zaidi ya kujiajiri mwenyewe? Mna kila chance ya kujiajiri na kuwaajiri wengine na kuweka matangazo kuwa mnaajiri lakini bado mnataka kuajiriwa.Tutafika kweli jamani!
  Jiajiri! usisubiri usalama wa taifa waje kutangaza ajira ,maana utasubiri mpaka Yesu arudi na hawatangazi ng'ooo.
   
 15. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #15
  Dec 22, 2009
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Shem vipi habari za rombo? kuna baridi? back to mada yetu hii umejibu vizuri, ukiendelea hivyo utakuwa mwalimu, masahihisjo mengine yatafanyika kwenye seneti.(studio) Ila unakipaji.
   
 16. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #16
  Dec 22, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  ZD mjasiri -wa- mali huyu bana acha kabisa. Weka makala hapa ili tujenge moyo wa kijiajiri ZD, itakuwa pouwa sana
   
 17. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #17
  Dec 22, 2009
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  bora hawa jamaa wanatumia email ya yahoo,
   
 18. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #18
  Dec 22, 2009
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mkumbushe mkuu wa kaya kwamba umesomea uwaziri kwa sababu nakumbuka kwenye speach yake ya kutangaza baraza la mawawaziri baada ya lile la richmond alisema hakuna chuo cha kusomea uwaziri nadhani itakuwa vyema ukimkumbusha. Kuna mawaziri wengi tu wako loose na skendo kila siku utakuwa umemsaidia sana muheshimiwa wetu.
   
 19. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #19
  Dec 22, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Liwale pazuri sana pale wanaotaka kazi wilaya ile pale waende ni pazuri pa kuanzia kilimo kwanza, msilaze damu wenye sifa
   
 20. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #20
  Dec 30, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,644
  Likes Received: 1,470
  Trophy Points: 280
  mmh........
   
Loading...