Vaa viatu vyangu halafu chagua cha kuanza nacho...!

StudentTeacher

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2019
Posts
5,635
Reaction score
5,921
Salamu ndugu wana JF

Moja kwa moja kwenye mada. Chukulia kwamba Mungu amekupa uwezo wa asili wa kufundisha na katika kuishi kwako umegusa watu kwenye maeneo mawili muhimu:
1. Elimu ya kitaaluma
2. Elimu ya Kiroho(Uponyaji kupitia Injili ya Yesu Kristo,hapa kuna ambao wameponywa magonjwa yasiyotibika si kwa kuombewa bali kwa kusikiliza na kuyaishi mafundisho ya Injili uliyowafundisha)

Na kote huko watu wamekuwa wakikupa mrejesho chanya baada ya kuyaonja matunda halisi kwenye maisha yao na umekuwa sababu ya wao kumshukuru Mungu kwa TALANTA alizokukirimia na namna unavyozitumia kwa uaminifu.
Sasa 'mgogoro' upo hapa...

Walioonja Uponyaji kupitia Injili uliyowafundisha wanatamani sana ufungue KANISA wakati huo huo walioonja matunda ya Elimu ya Kitaaluma uliyowahi kuwafundisha wanatamani sana ufungue KITUO cha Elimu ili waendelee kufaidi kwa upana zaidi matunda ya ubunifu wako kwenye sekta ya Elimu.

ZINGATIA kwamba yote mawili umekuwa ukiyafanya kwa mtu mmoja mmoja katika namna isiyo rasmi kimfumo,kimiundombinu n.k. Sasa unapaswa ufanyie kazi matamanio ya walaji wako ya kufungua KANISA au KITUO CHA ELIMU katika namna rasmi kimfumo na kimiundombinu na hauna msingi wa kutosha wa kifedha. Je,kama ingelikuwa ni wewe katika hayo mawili KANISA au KITUO CHA ELIMU(ambacho kimsingi kinalenga kutatua changamoto ambazo mfumo rasmi wa Elimu tulio nao hadi sasa umeshindwa kuzitatua hasa kwenye Sayansi na Hisabati) ungeanza na lipi?. Kwa nini?. Na je,ungeanza na hatua zipi?

NB: Projects zote mbili kwa hatua ya AWALI zinahitaji uwepo wako kiutendaji ili kujenga misingi na pia pressure kutoka pande zote mbili ipo equivalent. Hakuna la kupuuzwa. Yote yanapaswa kufanyika!

Karibu kwa michango yenu wakuu. Nitafuatilia kila mchango(maoni) kwa makini ili nipate linifaalo🙏
 
Ongeza wafuasi pande zote. Hao ndiyo watakuwa mtaji wako
 
Anza na kanisa kwan kanisa kwa hapa tz n kama mtaji ambao utakupelekea kumilik shule

Nb ukitangaza nafas ya MWASIBU nipo hapa hautojuta
 
Back
Top Bottom