Uzushi kuhusu walimu kushonewa sare

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
WIZARA YA ELIMU, SAYANSI, TEKNOLOJIA NA UFUNDI

TAARIFA KWA UMMA

YAH: TAARIFA ZA UZUSHI KUHUSU WALIMU KUSHONEWA SARE INAYOSAMBAZWA KATIKA MITANDAO YA KIJAMII

Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi inakanusha taarifa inayosambazwa katika mitandao ya kijamii yenye kichwa cha habari “NDALICHAKO NA WALIMU TZ”.

Taarifa hiyo inadai kuwa Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Prof. Joyce Ndalichako amesema kuwa walimu wanaandaliwa sare watakazo vaa wakati wa kazi.

Tunapenda kuufahamisha umma kuwa Taarifa hizi si za kweli. Aidha, Wizara inawataka watu wanaoeneza taarifa za kizushi za aina hii waache kufanya hivyo ili kuepusha usumbufu unaojitokeza. Hatua za kisheria zitachukuliwa kwa watakaobainika kuanzisha na kueneza uzushi huu.

IMETOLEWA NA

KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
07/04/2016
 
Sare sio na haijawahi kuwa miongoni mwa madai ya msingi ya walimu....

Hatuhitaji sare ili kuinua kiwango cha ufaulu wala kuboresha elimu kwa ujumla....yako mambo ya msingi kabisa na wizara inayatambuA ambayo ndiyo kilio chetu....natumaini awamu hii itayafanyia kazi....

Ni jambo la msingi kwa kuwa mmekanusha uzushi huo!!!!..
 
Kila siku kukanusha kwanini hao wazushi wasikamatwe mbona cyber crime law imetunyima bure mbona hao wazushi hawakamatwi,
Serikali ya makanusho.
 
Ni sahihi kabisa nilitaka kushangaa MTU makini kama Dr. Ndalichako aamue jambo kama hilo, kuna watu utawasikie eti mbona manesi na madaktari wanavaa, hii ni hoja ya watoto wadogo, wanavaa kutokana na asili ya kazi yao na Duniani kote ndivyo ilivyo. Sekta ya elimu INA matatizo mengi ya msingi inasikitisha katikati ya matatizo yao MTU analeta mijadala wa "uniform". Ni matumaini yangu kwa umakini wake mkubwa Dr. Ndalichako atayapunguza na kurudisha hadhi ya ualimu na elimu.
 
WIZARA YA ELIMU, SAYANSI, TEKNOLOJIA NA UFUNDI
TAARIFA KWA UMMA

YAH: TAARIFA ZA UZUSHI KUHUSU WALIMU KUSHONEWA SARE INAYOSAMBAZWA KATIKA MITANDAO YA KIJAMII

Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi inakanusha taarifa inayosambazwa katika mitandao ya kijamii yenye kichwa cha habari “NDALICHAKO NA WALIMU TZ”.

Taarifa hiyo inadai kuwa Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Prof. Joyce Ndalichako amesema kuwa walimu wanaandaliwa sare watakazo vaa wakati wa kazi.

Tunapenda kuufahamisha umma kuwa Taarifa hizi si za kweli. Aidha, Wizara inawataka watu wanaoeneza taarifa za kizushi za aina hii waache kufanya hivyo ili kuepusha usumbufu unaojitokeza.

Hatua za kisheria zitachukuliwa kwa watakaobainika kuanzisha na kueneza uzushi huu.

IMETOLEWA NA

KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
07/04/2016
 
Hvi kuvaa sare ndo wanatumia nguvu zote hzi kukanusha?
Wizara ya elimu ije na hoja kama;
I. Ada elekezi kimyaaa hadi leo.
II. Madai yetu walimu walisema mwishon machi hii ni april katikati.
iii. Vp mbona masters hazina madaraja wakati sector nyingine kuna madaraja na viwango vya mshahara mpaka PhD
iv. Hvi swala la posho kwa waratibu wakuu wa shule na walimu mbona utekelezaji wake ni kifafa kama sio kifo.
v. Lini bodi ya walimu itaanzishwa tuondokane na kuwa watoto wanaomjua mama ila wasiomjua baba yao?
Hizi ndio hoja za kuleta hapa sio viujumbe hivyo mtoto alikuwa anachezea simu ya babake au mamaye akapost.
Leten majibu acheni siasa tumeuliza mpaka tumechoka.
 
umenena ndugu
 
Yan kazi ya ualimu ililaaniwa toka enzi wanavaa kaptula wakati wanasomea ualimu enz hizo.huyo anayetaka leta sare wakati mambo ya msingi hawajafanya alikua anaota au? Sekto ambayo kila anayetaka kujifunza kuongea anapewa ndyo hii.Badala ya kutafuta utatuzi wa matatizo na changamoto za walimu,mtu anaanzisha hoja za sare!sare ndyo inafundisha?
 
Hvi kuvaa sare ndo wanatumia nguvu zote hzi kukanusha?
Wizara ya elimu ije na hoja kama;
I. Ada elekezi kimyaaa hadi leo.
II. Madai yetu walimu walisema mwishon machi hii ni april katikati.
iii. Vp mbona masters hazina madaraja wakati sector nyingine kuna madaraja na viwango vya mshahara mpaka PhD
iv. Hvi swala la posho kwa waratibu wakuu wa shule na walimu mbona utekelezaji wake ni kifafa kama sio kifo.
v. Lini bodi ya walimu itaanzishwa tuondokane na kuwa watoto wanaomjua mama ila wasiomjua baba yao?
Hizi ndio hoja za kuleta hapa sio viujumbe hivyo mtoto alikuwa anachezea simu ya babake au mamaye akapost.
Leten majibu acheni siasa tumeuliza mpaka tumechoka.
Mkuu nimeipenda 100%
 
WIZARA YA ELIMU, SAYANSI, TEKNOLOJIA NA UFUNDI
TAARIFA KWA UMMA​
YAH: TAARIFA ZA UZUSHI KUHUSU WALIMU KUSHONEWA SARE INAYOSAMBAZWA KATIKA MITANDAO YA KIJAMII
Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi inakanusha taarifa inayosambazwa katika mitandao ya kijamii yenye kichwa cha habari “NDALICHAKO NA WALIMU TZ”.
Taarifa hiyo inadai kuwa Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Prof. Joyce Ndalichako amesema kuwa walimu wanaandaliwa sare watakazo vaa wakati wa kazi.
Tunapenda kuufahamisha umma kuwa Taarifa hizi si za kweli. Aidha, Wizara inawataka watu wanaoeneza taarifa za kizushi za aina hii waache kufanya hivyo ili kuepusha usumbufu unaojitokeza.

Hatua za kisheria zitachukuliwa kwa watakaobainika kuanzisha na kueneza uzushi huu.
IMETOLEWA NA
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
07/04/2016
 
Kila siku kukanusha kwanini hao wazushi wasikamatwe mbona cyber crime law imetunyima bure mbona hao wazushi hawakamatwi,
Serikali ya makanusho.

Halafu walisema wamenunua mitambo ya kuwakamata hao wahalifu mbona hatuoni wakikamatwa au inakamata watu maalumu
 
ITAPENDEZA,kwani itakuwepo nidhamu na haiba nzuri ya uvaaji inayofanana kwa wote,hakuna ubaya.
 
Back
Top Bottom