hili nakubaliana nalo lakini linategemea na hali mkuu Tyta na hali zenyewe ni kama mko mazingira mamoja na huyo atakayekuvutia tabia,ikiwa uko naye muda mwingi na unaona jinsi anavyoishi na watu,anavyojiheshimu ni wazi kuwa unaweza kujikuta umevutiwa naye kwa tabia zake,lakini vipi kwa wale ambao ndo kwanza wamekutana na mmoja wapo akatamani mtu huyo awe mwenzi wake,nini nini kitaanza kwanza kumvuta au kumshawishi aje awe wake?
Sio wanawake wote kwangu mimi aliyenitoa bikira sitaki hata kumsikia.
Dude we are married for wrong reasons ila kwa good intention... waliochunguza tabia ni mitume na wanajimu wa zamani walioongozwa na elimu ya nyota ambao wakivutiwa na kitu ni lazima waanze kuchakura matunguli yao....
Assume wewe ni kijana safi ambaye chovya chovya ya elimu ya kuunga unga umejikuta ume attain college/University bila kujali means iliyokuleta kisha unakutana na descent girl aliyekuja pale purposely na incidentally mnajikuta mshamezeana mate...wewe kwa ajili ya miugwadu yako wakati yeye kavutwa na umahiri wako wa kucontribute constructive ideas kwenye maisha ya kila siku kwenye campus na muda unavyosogea mnajikuta viungo vyote vya miili yenu vimeshazoeana isipokuwa hivi viungo pendwa na mnajikuta hamna namna ya kuvikutanisha isipokuwa kufanya kile mlichokatazwa na wazazi.
..mnafanya...mnafanya tena na baada ya kunogewa mnajikuta hamna namna nyingine ya kuendelea kuibana isipokuwa kulegalize wizi huo kwa kuingia mkataba wa kuishi pamoja kwa kufanya mbwembwe za miezi miwili mitatu na kuwarubuni watu kwa wali na soda na hatimaye mnachukuana! Swali hapa ni muda gani mtakuwa mmepata wa kuchunguzana tabia? Huoni kama mtakuwa ni watu mlio bize kabisa mtaendelea kufaidi ya dunia bila kijuana hadi umri wenu wa pensheni ndipo muanze kujiuliza ili kuwakuwaje tukawa pamoja?
ni kweli outlook inakuwa first impression na kitakachofuata ni kumsoma tabia inayoweza kuhitaji muda zaidi..
mia mkuuu you have been honest ni kweli uzuri unamata pia lakini tabia ndugu yangu maanake wengine ni kunguru hafugiki mpaka hata huo uzuri utauona mchungu.
Kwa mara ya kwanza ntavutiwa na kitu toka kwa mwanaume iwe uongeaji wake,umbile lake au mvuto wake pili kinachofuata kujua tabia zake zikoje na je tunaendana? Maana anaweza kuwa HB la nguvu but tabia zake mbovu na zisizostahimilika.
Kwa hiyo tabia ina nafasi kubwa sana katika mahusiano
mimi naamini kuna wanawake(hopeful uwmewahi kuwaona mtaani) wameumbwa wasiolewe-hata angekua mchungaji hawezi vumilia vitendo vyake
nitakwambia lakini pia kama hutojali si hapa nitakuambia in private nitakupm ila sio sasa excuse me.
Habarini wana MMU,
Kuna usemi usemao uzuri sio urembo au mwonekano wa nje ila ni tabia,usemi huu una maana yake na kuna ukweli ndani yake,lakini swali linakuja,unawezaje kuanza kumchunguza mtu tabia pasipo kuvutiwa naye kwanza? yaani kupata sababu inayoweza kukufanya ukaanza kumchunguza mtu tabia yake?
Kwa binafsi yangu nafikiri mwonekano huwa wa kwanza,na hicho ndicho humfanya mtu akaanza kuchunguza tabia ya mtu fulani.
Wengine huvutiwa na nywele,kifua,sauti,kucha,pua,rangi,macho,lipsi,tembea au jinsi tu mtu huyo alivomchunguza tabia moja kwa moja bila kuvutiwa na kitu chochote kutoka kwake.
Wale ambao bado mnatafuta wenzi wenu wa maisha kwa sasa unaweza kuanza tu ilimradi kila mmoja ana kipimo cha kitu kinachomfurahisha binafsi kuwa anafaa kuwa naye na ikiwa hafai hata licha ya mwonekano mzuri ambao umemvutia mtu huyo anaamua hawezi kuishi naye. Hapo ndo ule usemi uzuri sio mwonekano wa nje bali ni tabia unatimia, lakini ni baada ya kuvutiwa na mtu fulani kwa nje kisha kuona kuwa kimwonekano anavutia lakini kitabia si mzuri.
Wengine mnasemaje juu ya hili?
kuna yeyote aliyewahi kuanza kumchunguza mtu wa jinisa tofauti ambaye leo hii ni mume/mke wake tabia yake ilhali hajavutiwa na kitu chochote kutoka kwa mtu huyo?
Na kwa wale ambao hawajafunga ndoa bado je mchumba uliyenaye kwa sasa,ulianza kuhunguza tabia ya mtu wa jinsia tofauti bila kuvutiwa na chochote kutoka kwake?
Hapa naongelea ule uhusiano unaopelekea kwenye ndoa na sio uboyfriend na ugilfriend karibuni wana mmu.
Blue G,Kwenye mahusiano ya aina yoyote na namaanisha aina yoyote lazima kuwe na mvuto kwanza…sasa hayo yanakuwa malengo ya mtu binafsi kama avutiwe na maumbile/muonekano au busara/hekima,wema au tabia…Lazima kuna kitu ambacho kitakuvuta uongee na mtu inawezekana ulivutiwa na uchangamfu wake au maongezi mloongea ambayo hupelekea kutaka kumchunguza mtu huyu kwa undani zaidi kama ni right candidate kwako!!
I Meant ulikua hujui kwamab uzuri wa mwanamka sio sura ni tabia??Mkuu sijakupata ulitaka kumaansiha nini?
I Meant ulikua hujui kwamab uzuri wa mwanamka sio sura ni tabia??
nalijua hilo tena sana tu,lakini mkuu unawezaje kuanza kumchunguza mtu tabia yake ikiwa hajakuvutia walau kwa kitu chochote,na kwa thred hii nilimaanisha kuwa huwa kuna jambo linakufanya uvutiwe kuazna kuchunguza tabia ya mtu.