Uzoefu wangu kuitwa na Kamati ya Bunge: Japo ameitwa kwa dharau, kwa kutishiwa pingu, lakini kiukweli CAG ameheshimiwa sana!

Hivi Paskal, kulalamika mbele ya baba na kulalamika mbele ya hadhara ya watu tena mnadani mambo yq nyumbani kwenu ni sawa sawa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
CAG akiitikia wito basi nchi inaelekea kubaya maana kumbe mtu yeyote anaweza kuvunja katba kwa kutumia mamlaka akiamua

Ni kweli uliyonena hilo halina Ubishi, watanzania wakiona CAG kaenda Dodoma kisa kuogopa Pingu watachukia na kumdharau sana kwani atakuwa kaharalisha uvunjaji wa katiba na sheria, ni vigumu kuwabadili wananchi watii katiba na sheria pindi Spika na CAG wanakwenda kinyume kwa kuwa mifano ya ajabu.
 
Nimeipenda hili andiko lako. Kwa mtu anayeelewa serikali hii na bunge lake hatapata shida. Ni ajabu sana kupewa appointment leo jioni halafu kesho ufike asubuhi, hii style inatumika kwenye awamu hii kukomoa hakuna lingine ila visasi visasi tu (Vendetta), Najua kabisa ungechelewa kidogo tu ungeambiwa umedharau bunge wakati ulitakiwa upewe usafiri na per Diem na pesa ya usumbufu. Huo ni udikteta na upuuzi wa bunge hasa kwenye kipindi hiki. Kumwita CAG kwa style hii haijawahi kutokea kwenye bunge lolote la Commonwealth tunaelezwa kwenye barua ya huyo Ndugai( Mpiga wenzake bakora) kwa bunge la jumuiya ya madola anasema TANZANIA NI NCHI HURU???? Kwani nchi zinazofuata sheria haziko HURU?? Ndugai anaongea asilolijua....Anatumia kivuli cha bunge kutimiza azma ya Magufuli ya kuonea wengine na kunyamazisha wengine kama vile anavyofanya Paul Kagame.(Magufuli anaiga Kagame's style)
 
Ni vizuri ukatueleze kilichotokea kwenye mahojiano hayo, unless kama sheria haziruhusu.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mie kwa uelewa wangu c.a.g.hajaitwa na spika.alie itwa ni mussa assad.hayo aliyosema assad kuwa bunge ni dhaifu,ni maoni yake binafs km assad.

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
So you're talking about retirement! Wasubiri atakapo staafu maana CAG haitwi kifala hivyo,wamsubiri Assad after being retired

Sent using Jamii Forums mobile app
UNAWEZA KUMTOFAUTISHA CAG NA ASSAD.HV ASSAD AKITOA ZAWADI HATA KWENYE HARUSI, OFISI YA CAG ITAHUSISHWA??!! TUSIPOTOSHE WATU. OFISI YA CAG IKITAKA KUTIMIZA MAJUKUMU YAKE HUTIMIZA KW MAANDUSHI.NA MAONI YA CAG YAPO OFSI YA BUNGE KW MAANDISHI.KM KM KW UCHUNGUZ WAKE KM CAG AMEONA BUNGE NI DHAIFU;ANGEANDIKA NA KUWAPA OFISI YA BUNGE.(IELEWEKE KUWA SISEMI KM BUNGE NI DHAIFU AU SIYO DHAIFU) JE CAG KWENYE MAANDIKO YAKE JUU BUNGE KUNA MAHARI KAANDIKA BUNGE NI DHAIFU??!! KW SABABU KILA ANACHOANDIKA CAG NI BAADA YA UCHUNGUZ WA KITAALUMA KUFANYIKA.ÇAG AKIWA ANATIMIZA MAJUKUMU YAKE YA KIKATIBA HAKUNA MAMLAKA YOYOTE INAWEZA KUMHOJI AU KUMWITA.

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Pascal nimecheka sana -uliposema umetumia usafiri wa Gambosh ukafika-
Nice article
 
Ukiona baba yako kakalia malalamiko yako kama spika alivyokalia file la trilion 1.5 unalalamika kwenye umati hata sokoni kkoo watu wajue kero yako hakuna ubaya kulalamika mbele za umma
Siyo kweli mkuu! Kama umekulia katika mji ambao hauna maadili haya yanawezekana lakini kama umekulia kwenye mji wenye Baba na Mama wanaofahamu nini maana ya malezi hakuna kitu kama hicho kutokea. Huyu Prof wenu yeye ana beef ninafsi na JPM na zina msukumo mkubwa na mambo fulani fulani na ndiyo maana hata Zitto kalishikia kibwebwe sana. Kumbuka issue ya Dau na uunganishe dots then kichwa kitakupoa. CAG kapotoka. Hawa wazungu nyie hamuwafahamu hata robo. Paskal ataweza kuelewa nazungumza nini!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kabla ya Assad kuwa CAG aliwahi kuzungumzia udhaifu wa bunge? kama hapana , basi aliyeitwa ni CAG Prof. Mussa Assad kwa sababu moja ya majukumu yake kukumbusha umuhimu wa bunge imara katika kutekeza majukumu yake katika kuisimamia serikali. binafsi yangu , sijui ASSAD alimaanisha udhaifu upi uliomfanya aseme bunge ni dhaifu kutokana na kazi zake kama CAG na hapo ndipo tutapata kitu kinachoitwa ' weak Parliament in relation to CAG activities'. kwa hiyo ni vema akaelezea udhaifu huo pengine atasikilizwa na kufanyiwa kazi na kupata bunge imara kulingana na matarajio ya ofisi kuu ya ukaguzi na CAG
 
Kwa hiyo ni double standard za "baba". Anapenda watoto wasio na tija kwenye familia. Ukiwa na tija baba anaona unamzidi kutimiza majukumu ya familia, anakushughulikia kupia kwa ndugu zako wasio na tija yeyote kwenye familia.

Pole mkuu P.

Naam, kuna wszazi wa aina hii. Baba mmoja jirani yangu aliombwa na mototo wake mahali pa kuweka genge karibu na nyumba yao akamkatalia. Baba huyo huyo akaombwa nafasi hiyo hiyo na mpngaji kwenye nyumba yake akamkubalia! Mpangaji anayo tija kuliko mtoto wake tena anayeonyesha bidii kubwa?
 
Prof. Assad hatapungukiwa chochote kwa kuitikia wito. Sana sana hadhi yake itapanda zaidi. Sidhani hata kuna maswali ya maana watakayomuliza. Ametoa maoni yake kuhusu Bunge kama raia na kama CAG full stop. Hilo Bunge kama linao uwezo wa kumwadhibu kwa hilo well and good. Lakini nadhani kinachotafutwa hapa ni upenyo wa kutokea ili kutofanya kazi na Prof. Assad. Wakati wa mjadala wa Tegeta escrow Mzee Wassira aliwakemea wabunge waliojaribu kunenga hoja ya kuikataa taarifa ya kamati ili eti kuwatetea wenzao waliobugi. Aliwaambia kuwa taarifa ya kamati ni taarifa ya CAG na haiwezekani hata siku moja kjikataa taarifa ya CAG vingenevyo tutakuwa hatuna nchi.
 

Methinks lengo la kumuita kwa namna ile ni ili akatae kwenda na hapo itakuwa imepatikana sababu ya Bunge kuamua kutofanya kazi naye kwani kiini cha tatizo ni taarifa zake. Kwa hali ilivyo, Prof. Assad ameshakuwa kero kubwa sana kiasi kwambà haiwezekani kumruhusu kuendelea kutoa taarifa zake. It is unthinkable and unacceptable in this era.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…