Uzoefu wangu kuitwa na Kamati ya Bunge: Japo ameitwa kwa dharau, kwa kutishiwa pingu, lakini kiukweli CAG ameheshimiwa sana!


Pascal Mayalla

Pascal Mayalla

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2008
Messages
27,603
Likes
32,143
Points
280
Pascal Mayalla

Pascal Mayalla

JF-Expert Member
Joined Sep 22, 2008
27,603 32,143 280
Wanabodi,

Japo CAG ameitwa na Spika kwa dharau kwa kutishiwa kuletwa kwa pingu, lakini nikilinganisha na mimi nilipoitwa na kamati hiyo, kiukweli kabisa CAG ameheshimiwa sana haswa kwa ile tuu kuitwa na kutajiwa tarehe ya wito.
My Story.

Tangu nilipoitwa kuhojiwa na Kamati ya Bunge kwa kosa kama la CAG la kulidhalilisha Bunge, sijawahi kuleta mrejesho wa nini kilijiri katika mahojiano hayo, na huu sio mrejesho bali ni uzoefu tuu wa kulinganisha kuitwa kwangu na kuitwa kwa CAG.
Chanzo cha Mimi Kuitwa.

Mimi niliuliza tuu humu jf kama " Jee Bunge Linajipendekeza kwa serikali?..". Gazeti lika peak na kuiifanya ni headline story ila alama ya kuuliza ikiwemo.

Mhe. Mbunge mmoja kama vile ni kilaza fulani, akaibuka na gazeti bungeni, akaisoma headline as a statement bila kuweka alama ya kuuliza
Mbunge kama huyu, ukiwaita baadhi ya wabunge wetu ni vilaza, utakuwa umewakosea? - JamiiForums

Ndipo Spika akalipokea.
“Naagiza hawa wote wafikishwe kwenye kamati ya maadili” –Spika Ndugai via YouTube
Spika na Maneno Ya Kujazia Jazia.
Hata mimi nilipoitwa, Spika alitamka maneno fulani ya kujazia jazia kunihusu mimi ambayo hayahusu, nilichoandika, ila kwa vile mimi ni nobody, maneno yoyote kunihusu hata Yakima ni ya hovyo, kwa someone who is nobody, its ok and I doesn’t matter much, lakini kumuita GAG kwa maneno ya kumtishia kwa pingu, kiukweli kabisa, it was uncalled for. Bunge letu lisikubali udhaifu binafsi wa viongozi wa Bunge kulifanya Bunge lidharauliwe. Mhe Spika nae ni binadamu tuu kama sisi na sio malaika, hivyo anaweza kukosea kiubinaadamu tuu, lakini tusikubali kuutetea udhaifu binafsi wa kibinadamu kwa kuuoanisha au kuuingiza kwenye uspika wa Bunge letu tukufu.

GAG Kapewa Muda wa Kutosha, Hii ni Heshima Kubwa.
Mimi nilipoitwa na Spika, alitangaza tuu Bungeni kuwa tutaitwa, lakini hakutangaza siku. Lakini kuitwa kwa CAG, tangu ile Press Conference, Spika ameitaja tarehe 21 Jan.

Barua Rasmi ya Wito.
Mimi tangu nilipotangwa kuitwa hadi kupewa barua, kilipita kipindi kirefu, lakini CAG kaitwa kwa kupangiwa tarehe tayari na baada ya siku 3, amepelekewa barua rasmi akiwa na siku zaidi ya 10 za kujiandaa kabla hiyo tarehe ya kuhojiwa.

Mimi niliitwa Ofisi ya ndogo ya Bunge na kukabidhiwa barua ya wito saa 9:00 mchana wa leo, kuifungua barua unatakiwa uwepo viwanja vya Bunge kesho yake asubuhi. Sasa mtu unajiuliza huu wito wa saa 9:00 mchana, kutakiwa Dodoma asubuhi ya siku inayofuata kwa usafiri gani wa public transport?!, unless kila anayeitwa kuhojiwa na kamati ya Bunge ana assume perliamentarian status anakuwa na shangingi, anajaza tuu mafuta na kuelekea Dodoma.

Thanks God, sisi wengine kwetu ni Gambosh, ile kufunga tuu macho, kufungua unajikuta uko Bungeni Dodoma tayari kuhojiwa, umekujaje, umetumia usafiri gani, only God knows!, ila cha muhimu nilifika na nilihojiwa

Pascal Mayalla ahojiwa na kamati ya Bunge - JamiiForums

Hivyo kuitwa kwa CAG, wengi wanaona kama ameitwa kwa kudharauliwa kwa kutishiwa asipoitika wito, atapelekwa kwa pingu, mimi naamini mtu kama mimi niliyeletewa barua leo na kutakiwa kuripoti kesho yake ningeshindwa ndio pingu zingenihusu, lakini kwa mtu kama CAG kuitwa kwa kutishiwa pingu, is not right at all.

Justification ya Wito.
Mamlaka ya Spika kumsummon mtu yoyote mbele ya kamati kwa kulidharau Bunge yako kwenye sheria na kanuni na sio kwenye katiba. Kinga ya CAG kutokuhojiwa na yeyote zaidi ya Mahakama iko kwenye katiba na kwenye sheria. Inapotokea sheria yoyote ikakinzana na Katiba, Katiba ndio supremacy na sheria inayompa mamlaka Spika kumsummon mtu yoyote ni batili.Tangu lini sheria na kanuni tuu ikaizidi katiba?.

Huku ni sawa na masikio kuzidi kichwa!. Japo Spika amemuita CAG kwa mujibu wa mamlaka yake, lakini mkisikia mambo ya mihimili kujiinua kuvuka mipaka ya mamlaka yake ndiko huku, watu wote wenye kuheshimu katiba na sheria, watamshangaa sana CAG kama ataitika wito huu kwa kuogopa tishio la pingu. Sisi ambao ni washabiki wa kuheshimiwa kwa katiba na kutekelezwa kwa sheria, taratibu na kanuni, tunapenda kuona huu mtanzuko ukimalizika kwa kufunuliwa kwa sheria batili ya mamlaka ya Spika na katiba ikiheshimiwa.

Tunasubiri kwa hamu hiyo tarehe 21, ila kwa sisi waelewa, ukiona watoto wawili wa baba mmoja, mmoja anasema ukweli wa udhaifu wa mwenzake mbele ya baba, halafu yule mwenye udhaifu badala ya kukanusha udhaifu wake ndio kwanza anamtishia mwenzake kuwa atamkomesha, na huku baba amenyamaza kimya tuu, wa kuelewa tumeelewa!.

NB. Naomba msiniulize kilichojiri kwenye mahojiano yale, nawaombeni sana mniruhusu ni reserve my comments.

Nawatakia Furahi Dei Njema.

Paskali
 
J

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Messages
14,632
Likes
12,524
Points
280
J

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined May 27, 2014
14,632 12,524 280
Sasa Paskali Assad ni Profesa NA tena ni Alhaj, hii maana yake ni kwamba anakubalika kote Mbinguni na Duniani kwa viwango vya juu lazima aheshimiwe.

Wewe na Mdee na huyo aliyewaita mnakubalika hapa duniani tu tena kwa kiwango cha vidigirii tu hata udaktari wa falsafa hamna ni halali yenu kuitwa kama aitwavyo PUSI aka Nyau.

Prof alhaj Assad ni level nyingine mkuu......... Na huo ndio ukweli mchungu!
 
Crimea

Crimea

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2014
Messages
5,536
Likes
4,360
Points
280
Age
29
Crimea

Crimea

JF-Expert Member
Joined Mar 25, 2014
5,536 4,360 280
Mm hii kwangu naona sinema kama zilivyo sinema nyingine ambazo huwa zinaratibiwa vizuri sana hapa nchini,

Kule kwetu mama akiona chakula siku hiyo hapasomeki, anawakaangia mahindi muendelee kutafuna huku muda ukiendeleea kusogea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
fogoh2

fogoh2

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2017
Messages
1,765
Likes
1,028
Points
280
fogoh2

fogoh2

JF-Expert Member
Joined Apr 13, 2017
1,765 1,028 280
Utakua hujamuelewa mtoa mada
Sasa Paskali Assad ni Profesa NA tena ni Alhaj, hii maana yake ni kwamba anakubalika kote Mbinguni na Duniani kwa viwango vya juu lazima aheshimiwe.

Wewe na Mdee na huyo aliyewaita mnakubalika hapa duniani tu tena kwa kiwango cha vidigirii tu hata udaktari wa falsafa hamna ni halali yenu kuitwa kama aitwavyo PUSI aka Nyau.

Prof alhaj Assad ni level nyingine mkuu......... Na huo ndio ukweli mchungu!
 
pepsin

pepsin

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2015
Messages
3,171
Likes
3,949
Points
280
pepsin

pepsin

JF-Expert Member
Joined Apr 23, 2015
3,171 3,949 280
Kwa hiyo ni double standard za "baba". Anapenda watoto wasio na tija kwenye familia. Ukiwa na tija baba anaona unamzidi kutimiza majukumu ya familia, anakushughulikia kupia kwa ndugu zako wasio na tija yeyote kwenye familia.

Pole mkuu P.
 
idawa

idawa

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2012
Messages
20,925
Likes
16,481
Points
280
idawa

idawa

JF-Expert Member
Joined Jan 20, 2012
20,925 16,481 280
Badala ya kusikitika nimebaki nacheka tu kwa jinsi ulivyowasilisha ujumbe wako , hata hivyo pamoja na kupewa vitisho huko kwenye kamati ya bunge lakini bado msimamo wako umebaki palepale...

Lile swali la kikatiba ulilouliza pale ikulu, litasimama siku zote za utawala huu.!
 
Nas Jr

Nas Jr

JF-Expert Member
Joined
May 15, 2018
Messages
2,208
Likes
1,460
Points
280
Nas Jr

Nas Jr

JF-Expert Member
Joined May 15, 2018
2,208 1,460 280
ukiona watoto wawili wa baba mmoja, mmoja anasema ukweli wa udhaifu wa mwenzake mbele ya baba, halafu yule mwenye udhaifu badala ya kukanusha udhaifu wake ndio kwanza anamtishia mwenzake kuwa atamkomesha, na huku baba amenyamaza kimya tuu, wa kuelewa tumeelewa
Hili bandiko litakurudisha tena kamatini
 
T

Tigershark

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2018
Messages
2,457
Likes
4,103
Points
280
T

Tigershark

JF-Expert Member
Joined Oct 9, 2018
2,457 4,103 280

Forum statistics

Threads 1,250,106
Members 481,224
Posts 29,720,833