Uzoefu wangu katika ufugaji wa kuku

mutu ya momba

New Member
Jan 28, 2016
4
11
Mwaka huu(2020) mwanzon niliamua kuanza ufugaji wa kuku chotara. Niliamua kuanza na kuku 120. Nlinunua vifaranga wa mwez mmoja

Changamoto
Magonjwa, hii ilkuwa changamoto ndogo magonjwa hayakuwa meng. Niliweza kuyatibu kwa wakati Ukuaji, niliambiwa wataanza kutaga wakifikisha miez minne.. lakn kiuwel walianza kutaga walipofikia miez 6.

Mapato
Nilitegemea kukusanya trei tatu kwa siku ambazo ngeuza elf kumi kwa trei.Wastan wa lak 9 kwa mwez.😀😀😀😀haikuwah kuwa hivo.
Nlkusanya mayai maximum trei mbili kwa siku bei elf saba mia tano kwa trei lak nne na nusu kwa mwez kwa wastan

Hitimisho
kuku hawa walikuwa wanakula kg 390 kwa mwez wastani wa mifuko 8 wastan wa 360,000/=kwa mwez ukiweka madawa na gharama zngne inakuwa lak nne kwa mwez. Kuna kipind walitaga pungufu ya trei mbili. unaweza ona hasara niliyopata. Wanaopata faida sijui wanatumia ujanja gani.
 
Duuh namimi nimeianza ya kuku wa kienyeji
Nina kuka majike ma 4.
Mmoja kashatotoa vifaranga 9 ila 7 ndo vipo hai vina kama week 4.

Mwingine katotoa vifaranga 14 juzi bado wapo.

Mwingine analalia mayai 12 na expect atatotoa next week.

Mwingine amezila kulalia nafikiria kumchinja.

Ngoja nione ila I believe Tutafanikiwa.
 
Ukilisha chotara chakula cha dukani usikae nao muda zaidi ya miezi 3. Lakini kama unataka biashara ya mayai nunua kuku wa mayai wa kisasa.

Ili upate faida ya chotara baada ya mwez mmoja wa kufuga changanya chakula chako mwenyewe.
 
Miez 9..lakini kila nikipiga hesabu sion dalili ya faida
Vifaranga ulinunua kwa mtu binafsi au kwenye makampuni makubwa kama interchick?

Kuna mdau humu alisema vifaranga wengi wanao nunuliwa kutoka kwa watu mtaani huwa na matokeo duni.

Tray 2 = 60eggs

Jumla kuku wapo 120

60/120 = 0.5 = 50% Duuh

Cc theriogenology
 
Hujapata hasara,umepata faida ya kujifunza ufugaji kwa vitendo na pesa kidogo iliyozama ni kama ada ya masomo.

Ili ufuge kibiashara na upate faida nzuri.
1)Jipange kwa mtaji wa kutosha hasa pesa ya chakula cha kuku.

2)Banda bora lenye nafasi ya kutosha kupitisha mwanga na hewa safi.

3)Vifaranga bora vya mayai.

4)Maji safi,Chakula bora na cha gharama nafuu.

5)Kudhibiti magonjwa ya kuku kwa kufanya usafi wa banda mara kwa mara.

6)Kuwapatia kuku chanjo na virutubisho kwa wakati.

7)Kuwaandalia kuku mahala pakutagia(viota)ili kuthibiti upotevu na kupasuka kwa mayai.

8)Kuweka rekodi ya maandishi mambo kama mapato na matumizi,ratiba za chanjo,mshahara wako na wafanya kazi n.k.

9)Ili upate faidi jitahidi sana kupunguza gharama za matumizi yasiyo ya lazima.

10)Fatilia kwa karibu kuku wako ikiwezekana simamia ufagaji kwa kadiri uwezavyo wewe mwenyewe.

11)Ukipata changamoto ya magonjwa na mambo mengine yanayohusu afya ya kuku wako basi wasiliana haraka na mtaalam wa mifugo.
 
Duuh namimi nimeianza ya kuku wa kienyeji
Nina kuka majike ma 4.
Mmoja kashatotoa vifaranga 9 ila 7 ndo vipo hai vina kama week 4.

Mwingine katotoa vifaranga 14 juzi bado wapo.

Mwingine analalia mayai 12 na expect atatotoa next week.

Mwingine amezila kulalia nafikiria kumchinja.

Ngoja nione ila I believe Tutafanikiwa.
Mkuu katika hao wa nne sijaona ulipotaja jogoo, hapo jogoo unatoa wapi au unategemea majogoo ya mtaani
 
Hujapata hasara,umepata faida ya kujifunza ufugaji kwa vitendo na pesa kidogo iliyozama ni kama ada ya masomo.

Ili ufuge kibiashara na upate faida nzuri.
1)Jipange kwa mtaji wa kutosha hasa pesa ya chakula cha kuku.

2)Banda bora lenye nafasi ya kutosha kupitisha mwanga na hewa safi.

3)Vifaranga bora vya mayai.

4)Maji safi,Chakula bora na cha gharama nafuu.

5)Kudhibiti magonjwa ya kuku kwa kufanya usafi wa banda mara kwa mara.

6)Kuwapatia kuku chanjo na virutubisho kwa wakati.

7)Kuwaandalia kuku mahala pakutagia(viota)ili kuthibiti upotevu na kupasuka kwa mayai.

8)Kuweka rekodi ya maandishi mambo kama mapato na matumizi,ratiba za chanjo,mshahara wako na wafanya kazi n.k.

9)Ili upate faidi jitahidi sana kupunguza gharama za matumizi yasiyo ya lazima.

10)Fatilia kwa karibu kuku wako ikiwezekana simamia ufagaji kwa kadiri uwezavyo wewe mwenyewe.

11)Ukipata changamoto ya magonjwa na mambo mengine yanayohusu afya ya kuku wako basi wasiliana haraka na mtaalam wa mifugo.
Umemaliza.
Hudhuria pia semina, warsha, zidi kujifunza uongeze maarifa ya ufugaji.
 
Mwaka huu(2020) mwanzon niliamua kuanza ufugaji wa kuku chotara. Niliamua kuanza na kuku 120. Nlinunua vifaranga wa mwez mmoja

Changamoto
Magonjwa, hii ilkuwa changamoto ndogo magonjwa hayakuwa meng. Niliweza kuyatibu kwa wakati Ukuaji, niliambiwa wataanza kutaga wakifikisha miez minne.. lakn kiuwel walianza kutaga walipofikia miez 6.

Mapato
Nilitegemea kukusanya trei tatu kwa siku ambazo ngeuza elf kumi kwa trei.Wastan wa lak 9 kwa mwez.😀😀😀😀haikuwah kuwa hivo.
Nlkusanya mayai maximum trei mbili kwa siku bei elf saba mia tano kwa trei lak nne na nusu kwa mwez kwa wastan

Hitimisho
kuku hawa walikuwa wanakula kg 390 kwa mwez wastani wa mifuko 8 wastan wa 360,000/=kwa mwez ukiweka madawa na gharama zngne inakuwa lak nne kwa mwez. Kuna kipind walitaga pungufu ya trei mbili. unaweza ona hasara niliyopata. Wanaopata faida sijui wanatumia ujanja gani.

Possibly mbegu haikuwa nzuri!

Kwa uzoefu wangu ungeweka kuku wa mayai hawa machotara wengine si wa mayai wanakushikisha kimagumashi kuwa wana uwezo mkubwa kutaga kimbe siyo.

Pia, hawa kuku ukifuga chini ya mia mbili ni hasara sababu madawa mengi yametengenezwa kwa ratio ya kuku 200, inayobaki ndiyo hasara
 
Ulipokosea ni kwenye msosi tu basi, hukutakiwa kuwalisha chakula cha dukani ungenunua pumba mashineni ukawachanganyia na damu, alizeti, vumbi la dagaa/uduvi, chokaa, mifupa, nk wanakila vizuri tu na bado ungepata matokeo bora zaidi. Next tym fanya hivyo mkuu mimi ninao wachache ninauza mayai mengine natotolesha nauza vifaranga na kuku na mayai tray nauza 13
 
Ukilisha chotara chakula cha dukani usikae nao muda zaidi ya miezi 3. Lakini kama unataka biashara ya mayai nunua kuku wa mayai wa kisasa.

Ili upate faida ya chotara baada ya mwez mmoja wa kufuga changanya chakula chako mwenyewe.
Kweli kabisa mkuu
 
Duuh namimi nimeianza ya kuku wa kienyeji
Nina kuka majike ma 4.
Mmoja kashatotoa vifaranga 9 ila 7 ndo vipo hai vina kama week 4.

Mwingine katotoa vifaranga 14 juzi bado wapo.

Mwingine analalia mayai 12 na expect atatotoa next week.

Mwingine amezila kulalia nafikiria kumchinja.

Ngoja nione ila I believe Tutafanikiwa.
Aliyezira kulalia uaimchinje. Mpe kazi yz kutaga. Inapowezekana, si lazima wote wallie.
Inafaa walalie wavivu wa kutaga.
Anayetaga vizuri/mayai mengi afanye kazi ya kutaga.
Kulalia wanafaa kuku wakubwa ambao utawapa mayai mengi.
 
  • Thanks
Reactions: apk
Shukrani mkuu maana nilikua nime mpania, nikirudi home ameisha!
Aliyezira kulalia uaimchinje. Mpe kazi yz kutaga. Inapowezekana, si lazima wote wallie.
Inafaa walalie wavivu wa kutaga.
Anayetaga vizuri/mayai mengi afanye kazi ya kutaga.
Kulalia wanafaa kuku wakubwa ambao utawapa mayai mengi.
 
Nategemea mtaani Mkuu
Ila kwa baadae vifaranga vikikua ntakua na majogoo yng

Na ninampango kuwafuga kisasa zaidi
Sawa mkuu, kwenye ufugaji wowote kua na dume bora ni jambo la muhimu sana hii ni kanuni ambayo wafugaji na kwa upande wa wakulima (mbugu bora ni jambo la muhimu sana) kumbuka dume ndio linatoa mbegu ili kuzalisha majike

Mama yangu alifanyaga cross breed ya dume la ng'ombe kutoka kitulo (la kisasa) na ngombe wa kienyeji ambao walikua wanatoa maziwa kidogo sana kupata lita tatu ilikua ni kwa mbinde sana, lakini watoto waliozaliwa baada ya lile dume aisee walikua ni kama purely ng'ombe wa kisasa walikua wanatoa kuanzia lita tisa mpaka kumi na tatu kwa mkamuo kutokea hapo nilijifunza umuhimu wa mbegu/ dume bora
 
Ulipokosea ni kwenye msosi tu basi, hukutakiwa kuwalisha chakula cha dukani ungenunua pumba mashineni ukawachanganyia na damu, alizeti, vumbi la dagaa/uduvi, chokaa, mifupa, nk wanakila vizuri tu na bado ungepata matokeo bora zaidi. Next tym fanya hivyo mkuu mimi ninao wachache ninauza mayai mengine natotolesha nauza vifaranga na kuku na mayai tray nauza 13
Unaweza kutusaidia hiyo fomula?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom