Uzoefu wa Kukaribia Kifo

Karibu mkuu tunasubiri ushuhuda.
Mwaka 2009 tlikuwa kuna sehemu tunashuka mizigo kutoka kwenye tandamu (Fuso ndefu zile) ..Sasa bhana , niliporomoka kule juu kwa vile nilikuwa natoa tu mizigo wa chini wanapokea , yaani nilivuta kiroba kwa nguvu kumbe hamna kitu ndani so nikajipusha kurudi nyuma , nikapiga kisogo , kutoka juu kabisa kule ya bodi ya tandam.

Kumbe nilizima , sasa bhana baada ya kuanguka naona jamaa wamenizunguka kabisa ,mimi nawaona kabisa ila siwasikii wanaongea nn , nikitaka kumka viungo havifanyi kazi ,baadaye kidogo fikra zikaanza kujirudi kama mtu ninayerudi nyumbani , kwetu tunapoishi ilikuwa nyuma tu sio mbali na hapo , yaani mawazo yananionesha narudi ile njia niliyokujia mpaka nafika home , kama namuona mzee yuko home anasoma gazeti na mother anapika , yaani nawaona kabisa na mwili uko huku eneo la tukio . Nilijiwa na kumbukumbu za udogoni kabisa nacheza na jamaa zangu , muda huyo tulikuwa ni wakubwa .

Nilikuja kuzinduka kama nusu saa hivi , ila nilikuwa natokwa na machozi .jamaa wakaniambia nilikuwa nimezima ...Hayo mambo mengine sikuona , ila mazingira nilikuwa naona mwanga mkali .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…