Uzinzi umemponza

LE GAGNANT

JF-Expert Member
Jan 20, 2011
1,241
251
Herman Cain. Aliongoza mwanzoni kwenye mbio za kuwania urais wa marekani kwa tiketi ya chama cha republican.
Imebidi ajitoe baada ya kukabiliwa na mfululizo wa tuhuma za uzinzi na kudhalilisha wanawake, na wote ni wazungu.

Herman-Cain-David-Tulis-AP.jpg
 
Wote si wazungu, wa mwisho ambaye akatoa na ushahidi wa text msgs, phone logs na autographed book hakuwa mzungu. Kwani jamaa alikuwa hajui kama siasa za kimarekani zina mchezo huo?
 
Ingekuwa na nchi yetu viongozi wanajitoa baada ya tuhuma zozote zinazo wakaba roho tungekuwa mbali, bali wanakuwa wanang'ang'ania wakijua kuchakachua watapita.
 
Baada ya Obama wahafidhina/wabaguzi hawako tayari kuwa na rais mwingine mweusi. Hivyo 'nuksi' imeshughulikiwa mapema. Na huyo naye huko GOP anatafuta nini? Hakujua yatakayompata?
 
Ingekuwa na nchi yetu viongozi wanajitoa baada ya tuhuma zozote zinazo wakaba roho tungekuwa mbali, bali wanakuwa wanang'ang'ania wakijua kuchakachua watapita.

ndugu yangu huku bongo kwa swala la uzinzi hakuna atakae toka hata afumaniwe live nakwambia... huku tumeozaaa....
let me shout "HUKU TUMEOZAAAAAAAAAA" hatuna tunachojua kama ingekua tuna kitu chochote tunachojua tungekua tumelivua hili gamba siku nyingi sana...!
 
Yap nilipomuona siku anahutubia kujitoka kwenye kinyanganyiro hicho nilishangilia,nikasema Yap,Once Black Always Black.Hicho ndio kidume kinachotakiwa.
 
Baada ya Obama wahafidhina/wabaguzi hawako tayari kuwa na rais mwingine mweusi. Hivyo 'nuksi' imeshughulikiwa mapema. Na huyo naye huko GOP anatafuta nini? Hakujua yatakayompata?

GOP ni chama cha mabepari, kule pamoja na pesa kukuruhusu rangi nayo inafuata mkondo. Wangemruhusu angeweza penya kwenye tundu la sindano kama ilivyotokea kwa Obama. Bora kumtosa mapema.
 
Back
Top Bottom