ni kweli, hiyo mifano nimewahi kumsikia mmoja wa mhubiri akiitoa ila inaponichanganya nimekutana na kipengere katika chapishi hili
VIPENGELE VYA SOMO(1). NI MAANA YA KUKUFURU?(2). DHAMBI YA KUMKUFURU ROHO MTAKATIFU IKOJEE?(3). DHAMBI YA KUMKUFURU MUNGU ILIFANYWA NA SHETANI NA MALAIKA ZAKE WALIOASIUTANGULIZIKumkufuru Roho mtakatifu ni dhambi nyingine mbaya sana tena kubwa zaidi ambayo haina msamaha milele na milele.Na ole...
mwandishi anasema : -
Dhambi ya kumkufuru Roho haiwezi kufanywa na watu ambao bado hawajaokoka.
Wala Dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu haiwezi kufanywa na mkristo yoyote tu wa kawaida ambaye hajainuliwa na Mungu katika ngazi yoyote ya utumishi katika huduma iliyowekwa na Mungu ndani yake.
Nini maana ya kukufuru?
Ni maneno ya dhihaka, dharau, kejeli, matusi kinyume na Mungu.
Ayubu 2:9 Ndipo mkewe akamwambia,je wewe hata sasa washikamana na utimilifu wako? Umkufuru Mungu ukafe.
Walawi 24:16 Na yeye atakayelikufuru jina la BWANA hakika atauawa, mkutano wote watampiga kwa mawe....
Agano la kale(torati) aliyemkufuru Mungu ilimpasa auawe kwa kupigwa kwa mawe.
Agano jipya imeenda zaidi kwa anayekufuru kutosamehewa milele,na na imekuwa specified kumkufuru Roho Mtakatifu.
Kwa tunaoamini kuhusu uungu nafikiri tutaelewa kirahisi kwanini sio Mungu baba,wala Mwana bali Roho Mtakatifu?
Marko 3:28-29 Amin nawaambia dhambi zote watasamehewa wanadamu na kufuru zao watakazokufuru zote,
29.bali mtu atakayemkufuru Roho Mtakatifu hana msamaha hata milele ila atakuwa na dhambi ya milele.
Luka 12:10 Na kila mtu atakayenena neno juu ya Mwana wa Adamu atasamehewa,bali aliyemkufuru Roho Mtakatifu hatasamehewa.
Kwanini Roho Mtakatifu?
Yohana 16:8 Naye akiisha kuja huyo,atauhakikishia ulimwengu kwa habari ya dhambi,na haki,na hukumu.
Roho Mtakatifu ndiye anayetushuhudia kwa habari ya dhambi zetu,huachilia hali ya kusikia hatia(convict)tunapokosea mioyoni mwetu ili tutubie dhambi zetu kwa toba,hutuelekeza kwenye haki.
Yeye ndiye anayewavuta wenye dhambi kwa kuweka hali ya kujutia makosa yao na kuamua kuokoka.
So Biblia inamaanisha huyo Roho Mtakatifu akifanya hayo yote kwako na kumjua Mungu na kumtumikia chini ya nguvu ya Roho Mtakatifu ukaona kwa dhahiri nguvu na uwezo wa Mungu kwa dhahiri watu wakajua na kukuheshimu kama mtu wa Mungu na shetani amejua,ghafla ukiiacha hiyo neema na kuanza kukufuru matukufu ya Roho Mtakatifu ndio inaitwa dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu.
Unakuwa umemhuzunisha na kumnyamazisha ndani yako unasaidikaje?
Unakuwa kama mnyama tu,husikii hali ya hatia,huhisi tena hukumu ukikosea ili utubu nafsi inakuwa imekufa haiwezi kufanywa hai tena maana aletaye hali ili utafute kuwa hai anenyamaza kwa kumnyamazisha makusudi kwa dhihaka,dharau.
2 Petro 2:12 ...Kama wanyama wasio na akili...wakimufuru....wataangamizwa.
Waefeso 6:4 Kwa maana hao waliokwisha kupata nuru na kukionja kipawa cha nguvu,na kufanywa Washirika wa Roho Mtakatifu,
5,na kulionja neno zuri la Mungu na nguvu za zamani ,zijazo
6.Wakaanguka baada ya hayo HAIWEZEKANI kuwafanya UPYA TENA hata WAKATUBU,kwa kuwa wamsulubisha Mwana wa Adamu mara ya pili kwa nafsi zao na KUMFEDHEHI KWA DHAHIRI.