Uzinzi, dhambi namba moja duniani

Uzinzi, dhambi namba moja duniani

Mungu ni mwingi wa huruma,hakuna dhambi asiyo samehe.Ukijuta na kudhamiria kutokutenda tena dhambi anasamehe.Dhambi kubwa afrika ni ufisadi,rushwa,uongo,unafiki,fitina,masengenyo,wizi,ulafi,kutokuwa mwaminifu,ubinafsi kujilimbikizia mali hili hali ndugu zako umewatupa hii nazungumzia ubinafsi mtu kupata cheo nakutumia fursa hiyo kujilimbikizia mimali n.k mali njema ni nzuri sio kila mali ni mbaya.Mtu anaweza asiwe mzinzi na mwasherati ukamkuta kwenye hayo maeneo.Kwa wazungu starehe,sex ni vitu vya kawaida lakini ni waminifu kupita maelezo hila sisi wafrika ni waigizaji wakubwa sana ndio manake atuendelei.
 
Usinzi ni kutoka nnje ya ndoa, na ni kosa kubwa. Kama ni mtu mzima kuwa na rafiki sioni kosa ili mradi mnaelewana pasipo kulazimisha. Kosa ni kumsababishia mwenzio matatizo kwa makusudi. Ukiwa na kijana wako zaidi ya miaka 18 akakutambulisha rafiki yake wa kike utasemaje? Watu wa dini wanasisitiza mpaka ndoa, asiyependa kuoa au kuolewa afanyeje?? Kwangu sio kosa ni maelewano tu ila sio zaidi ya mmoja ili kulinda urafiki
 
Nionavyo mimi, kuzini ndio dhambi ambayo inaangusha wengi kuliko zote. Watu wengi wanaamini kwamba hawawezi kukaa bila kufanya ngono hadi siku watakapooa rasmi.
Wanaona kuwa kukaa bila kufanya mapenzi ni kitu ambacho hakiwezekani kabisa. Hivyo basi wengi wameamua kufanya uasherati na uzinzi kwa sana, kwa sababu wanafikri ni jambo lisilokwepeka.

Imefikia hatua kwenye jamii zetu, mtu akionekana hajihusishi sana na mambo ya mapenzi, hasa wanaume, basi anatiliwa mashaka na kuonekana kwamba pengine hayuko sawa kimaumbile, mfano labda jogoo hawiki n.k

Na wale ambao ni play boys, ambao hawapitwi mbele na sketi, eti hao siku hizi ndio wanaonekana, majembe, wanaume wa ukweli, tofauti na wale ambao hawajishughulishi na ngono ambao huambulia kejeli na matusi kibao.

Sasa sijui tumerogwa na nani?
Yaani uzinzi umekuwa fasheni, ukiufanya unasifiwa, ukitulia usifanye ngono ovyo, unatukanwa. Na kuitwa majina ya ajabu ajabu.

Leo hii, mawazo karibia ya vijana wote ni uzinzi mtupu, wanawaza ngono tu, kama huamini, fanya research hata kwenye mitandao ya kijamii, utaona uzinzi ulivyoota mizizi, nenda kwenye groups za WhatsApp uone jinsi vijana wanavyoshinda wakitongozana tangu asubuhi mpaka usiku wa manane, nenda fb, nenda Hitwe, njoo jf, n.k Kutongozana kunaenda sambasamba au hata kuzidi mada zingine zote mitandaoni.
Wnafunzi wanaoenda vyuoni pia kando na kusoma lengo lingine ni kwenda kuendekeza uzinzi chuo.

Kijana akiona binti, wazo la kwanza linalomjia kichwani ni kufanya naye mapenzi, atajitahidi mpaka alale naye. Ndio maana hakuna urafiki wa kudumu kati ya binti na kijana.

Watu wazima, wasomi na akili zao, wameacha wake zao nyumbani, wamehamia kwa michepuko.

Iwe shuleni, kazini, nyumbani, Kanisani, Msikitini, Chuoni, KOTE HUKO. NGONO NDIO HABARI YA MJINI.

Matokeo yake ni ndoa kuvunjika, magonjwa, kifo na mwisho KUKOSA UZIMA WA MILELE.

KUACHA UZINZI INAWEZEKANA, AMUA UTASHINDA! MUNGU HAKUTUPATIA AMRI NZITO TUSIYOWEZA KUISHIKA, AMRI ZOTE NI NYEPESI NA ZINASHIKIKA.

Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu, kwamba tuzishike amri zake; wala amri zake si nzito.

1 Yohana 5:3
Kwa mujibu wa kitabu kitakatifu tunachotumia hakuna dhambi kubwa wala ndogo! Sina hakika na ulichosoma wewe!
 
Tupo katika zama ambazo kuishikilia dini ni kama kushika kaa la moto..!
 
KWANGU, IMEFIKA WAKATI NAONA NENO DHAMBI NI RELATIVE.
 
Back
Top Bottom