Uzinduzi wa Studio mpya za Azam Media

Uzinduzi wa Studio mpya za Azam Media

Magazetini

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2014
Posts
593
Reaction score
1,713
Habari wakuu,

Leo ni uzinduzi wa studio mpya za Azam zilizopo Tabata Dar es Salaam, wazo ambalo lilitolewa March 8, 2014 na tenda hio kupewa kampuni kutoka Uingereza na kuigharimu Azam zaidi ya bilioni 53. Kulingana na maelezo ya Tido ndio studio bora zaidi Tanzania mpaka sasa. Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais Jakaya Kikwete. Kuna wageni wengi waalikwa wakiwemo James Mbatia, Mwigulu Nchemba, Prof Lipumba, Filbert Bayi, Jamal Malinzi, Taji Liundi na wengineo.

Azam Studio.jpg
================

Mwigulu: Mmeonyesha uzalendo katika matangazo, mwekezaji aliewekaza katika studio hii ameonekana kuwa na mafanikio kila anapowekeza kwenye sekta nyingine, tupo kwenye safari kuifanya nchi kuwa ya kiwango cha kati, tunahitaji serious investors ambao ni watanzania na wataajiri wafanyakazi wa kiwango cha kati.

Mbatia: Kazi kubwa ya vyombo vya habari kuhabarisha, kuelimisha na kuburudisha, vyombo kama hivi vinafikisha taarifa mapema

Prof J (Mwanamuziki): Azam anazidi kuvuka mipaka na kuuza kazi zetu nje, tuendelee kuwapa sapoti.

Mpinga: Itasaidia katika kuelimisha, kwa upande wangu naomba pia wajikite katika kuelimisha mambo ya barabarani
 
Pamoja na ubora wa vifaa ambao unasisitizwa sana katika uzinduzi huu, utendaji kazi hasa katika utangazaji, utafutaji na uwasilishaji habari ni vya muhimu zaidi.

Habari zinazofuatiliwa na zenye tija kwa jamii ndicho kinachotambulisha chombo kizuri cha habari.

kazi kwenu Azam Media.
 
Mfano umeanzia kwa Tido Muhando natumaini wafanyakazi wataajiriwa kwa qualification.

Wabongo bwana! Hivi mtaacha lini kuwapangia watu cha kufanya, hivi wewe kwa akili yako unaweza kumpangia bakressa jinsi ya kuajili au unadhani lile ni shilika la umma? Yule ni mfanya biashara na kila kitu kwake anaangalia faida kwanza, angekua haajili kwa sifa asingefika hapo aliopfika. Tido ameajiliwa miezi karibu mitatu iliyopita na mtendaji mkuu wa azam media ni mzungu.
 
Dah!,kweli miti imeota kwa wajenzi sasa no kazi na dawa
 
Wabongo bwana! Hivi mtaacha lini kuwapangia watu cha kufanya, hivi wewe kwa akili yako unaweza kumpangia bakressa jinsi ya kuajili au unadhani lile ni shilika la umma? Yule ni mfanya biashara na kila kitu kwake anaangalia faida kwanza, angekua haajili kwa sifa asingefika hapo aliopfika. Tido ameajiliwa miezi karibu mitatu iliyopita na mtendaji mkuu wa azam media ni mzungu.

Umeongea vizuri sana mkuu,Mali ya MTU si ya umma jamani mtambue hill hats akisema ndugu zake tu yeye ndo anaju anataka mini na kwa staili gani
 
Wabongo bwana! Hivi mtaacha lini kuwapangia watu cha kufanya, hivi wewe kwa akili yako unaweza kumpangia bakressa jinsi ya kuajili au unadhani lile ni shilika la umma? Yule ni mfanya biashara na kila kitu kwake anaangalia faida kwanza, angekua haajili kwa sifa asingefika hapo aliopfika. Tido ameajiliwa miezi karibu mitatu iliyopita na mtendaji mkuu wa azam media ni mzungu.

Sasa umeeleza tofauti gani na nilivyoeleza? Nililoandika ni tumaini langu kutokana na dalili za kumuajiri Tido. Pamoja na kuwa mfanyabiahsra nchi na jamii huwa zina utaratibu wake. Kuwa mfanyabishara si kigezo cha kufanya chochote anachotaka! Kungekuwa hakuna utaratibu angeweza kuamua kuajiri wafanyakazi wote waarabu kutoka uarabuni!
 
Kwa studio kama iyo hao watangazaji sasa inabidi wakajifunze kwa wenzao wa citizen ya kenya wanavyojiachia kwa kutangaza na lugha sahihi . Sio hapa watangazaji hawajui hata kutofautisha R NA L yani huwa inakera sana..ukiangalia news citizen yani unasikia raha kwa kiswahili chao sahihi
 
Sasa umeeleza tofauti gani na nilivyoeleza? Nililoandika ni tumaini langu kutokana na dalili za kumuajiri Tido. Pamoja na kuwa mfanyabiahsra nchi na jamii huwa zina utaratibu wake. Kuwa mfanyabishara si kigezo cha kufanya chochote anachotaka! Kungekuwa hakuna utaratibu angeweza kuamua kuajiri wafanyakazi wote waarabu kutoka uarabuni!

Unazidi kujichanganya yeye kama mfanya biashara kama angekua haajiri kwa mujibu wa sifa(angalia post yako #11 ) angefiakje hapo. Huyu mtu ameanza biashara zake tokea miaka ya sabini na kipindi chote hicho amekua akiajili kulingana na mahitaji yake na ndo chachu ya mafanikio yake.
 
Back
Top Bottom