Uzinduzi wa miradi mipya ya ACT - Wazalendo Mbozi

Uzinduzi wa miradi mipya ya ACT - Wazalendo Mbozi

Mkutano huo utahusisha uzinduzi wa salon ya kiume iliyopo stendi ya malori mjini Vwawa na bodaboda mpya tatu. Miradi hiyo mipya ni miongoni mwa miradi ambayo tayari ilishazinduliwa miezi miwili iliyopita.

>Miradi inayomilikiwa na ACT Mbozi ambayo tayari ilishazinduliwa ni:

*Kikundi cha kukopesha fedha kwa riba chenye ofisi zake stendi ya makaburini mjini Vwawa

*Ng'ombe tisa wa maziwa

*Kiwanda kidogo cha kutengeneza samani kilichopo stend ya makaburini mjini Vwawa.

*Bodaboda tisa

-Na ijulikane kuwa miradi yote, shabaha yake kubwa ni kutoa ajira kwa wanachama na raia wote wa Tanzania kwa ujumla.

Vipi kuhusu wakimbizi wa Burundi mliowasajiri kama wanachama wenu pale kakonko?Elisha wadingulia miradi?
 
Tukundane we sijue nikuelewe vipi kilasiku unajifanya unatujua, afu umechukua kadi kwenye mikutano huji. Kazi kuizungumzia CUF, aliyekwambia pale ni pa CUF ni nani??

Naona mna lazimisha uanachama kwenye saccoss ya mwandiga
 
Tukundane we sijue nikuelewe vipi kilasiku unajifanya unatujua, afu umechukua kadi kwenye mikutano huji. Kazi kuizungumzia CUF, aliyekwambia pale ni pa CUF ni nani??

Mnalazima umaarufu,jambo ambalo ni hatari kabisa
 
ACT mbozi na ninyi mmezidisha uongo,mnamiradi gani Mbozi zaidi ya kuweka bendera yenu katikati ya bendera ya CHADEMA na CCM,labda kama miradi yenyewe ni kufunga bendera yenu kwenye mlingoti mrefu zaidi ya vyama vingine hapo sawa,zaidi ya hapo hakuna cha mradi wala mama yake na mradi.

.... Hahahahaha, Tukundane Bana Umenichekesha Sana
 
We Tukundane Tunakufaham we Nimpinga Act Ndani Ya Act

Ah! sasa chama kinachopigania kuchukua dola ati kinafungua mradi wa saloon ya kiume na vikoba, hebu tukumbushani saloon ya kiume ina vitu gani, vioo vikubwa viwili, mashine mbili za kunyolea, taulo kuukuu tatu, nini kungine, huo nao ni mradi wa chama. Haahahahahahahahahahaha, acha ncheke miye
 
Ah! sasa chama kinachopigania kuchukua dola ati kinafungua mradi wa saloon ya kiume na vikoba, hebu tukumbushani saloon ya kiume ina vitu gani, vioo vikubwa viwili, mashine mbili za kunyolea, taulo kuukuu tatu, nini kungine, huo nao ni mradi wa chama. Haahahahahahahahahahaha, acha ncheke miye

Akikuambia mwanzo mgumu utabisha?:beer:
 
Akikuambia mwanzo mgumu utabisha?:beer:

Hawa jamaa ni waongo kama shetani ni juzijuzi mleta uzi alileta uzi uliokuwa unasema kuwa ACT mbozi wampindua mwenyekiti wao.

Katika uzi wake huo alieleza kuwa sababu za kumpindua mwenyekiti wao ni kwamba ni mtu mchafu,asiye jipenda,anayetanguliza masilahi mbele na mlevi wa pombe za kienyeji.

Kwa ujumla huyu mwenyekiti wao ninafahamu kwa kuwa nilishawahi kuishi mbozi baada ya kutoka kanda ya ziwa,ana fanya kazi ya kung'arisha viatu katika mtaa mmojawapo pale Vwawa.

Sasa je kama wana miradi ya bodaboda,kiwanda cha kutengeneza samani,mradi wa bajaji na wanakopesha fedha kwa wanachama wao pamoja na wananchi wengine wasiyokuwa wanachama.

Wanampinduaje mwenyekiti wao kwa uchafu wakati walitakiwa wamkopeshe fedha ili anunue nguo za kuvaa na kununulia sabuni za kufulia nguo zake?,wanamuachaje mwenyekiti wao aendelee na kazi ya kung'arisha viatu wakati wana mradi wa bajaji na bodaboda 9 badala ya kumpa bodaboda au hata bajaji moja mwenyekiti wao ili aondokane na kazi ya kungarisha viatu kijiweni?.

Kuna usemi unaosema nyumbani kwanza,hawa ACT mbozi wanasema kuwa wanawakopesha fedha wanachama na wasio kuwa wanachama,ilikuwaje wakashindwa kuanza na mwenyekiti wao aliyekuwa wa wilaya ambaye sasa hivi wanasema ni katibu mwenezi kumkopesha fedha ambazo zingemsaidia kuondokana na kazi anayo ifanya,fedha ambazo zingemsaidia pia kuondokana na uchafu pamoja na ulevi wa pombe za kienyeji badala ya kumpindua?.
 
Back
Top Bottom