Uzi wa stori za vijiweni

Uzi wa stori za vijiweni

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
37,136
Reaction score
55,605
KIJIWE CHA KAHAWA

Siku moja nilienda kutembelea kijiwe kimoja cha kahawa, huko mkoani Kilimanjaro bara bara ya kuelekea mlima kilimanjaro.

Kulikuwa na wazee na vijana wengi wakipata kahawa, huku wakileta stori za hapa na pale, ili mradi kuchangamsha kijiwe, huku tukisikiliza BBC matukio ya dunia. Na kutokana na hali ya hewa, kijiwe kilichangamka.

Mzee mmoja, akasema wajukuu zangu, ‘’nawausia sana, msiwe na tamaa ya pesa, mnaliona lile jengo kubwa pale karibu na mjini, lina historia ndefu.

Waliolijenga hilo jengo ambao ni wamiliki walishatangulia mbele za haki, walikuwa vijana wawili, walienda machimboni na walikuwa marafiki kweli kweli, na wote walikuwa wanatoka kijiji kimoja.

Baada ya kufika huko machimboni, walifanikiwa kupata jiwe lenye thamani kubwa; na baada ya kuliuza walipata hela nyingi, wakaamua kulijenga hilo jengo ili liwe hotel.

Wakalisimamisha hilo jengo kwa haraka sana, pamoja na kuweka mazingira ya nje kwa ajili ya kuvutia wateja.

Kwa bahati mbaya, mmoja kati ya wale wamiliki akaingiwa na roho ya ubinafsi, tamaa, na kutaka kumzidi kete mwenzie. Akamfanyia mwenzie mambo ya ajabu ajabu mpaka umauti ukamfika huko machimboni.

Kwa sababu yule kijana ndio aliyebaki, na ndiye anapafahamu kwa mwenzie ambaye ni marehemu, alitoa taarifa kwao, na akafanya utaratibu wa kusafirisha mwili kwa ajili kuweka msiba. Taratibu za mazishi zikapangwa, na akazikwa.

Lakini wazazi wa yule marehemu wakawa wana maswali mengi kuhusu kifo cha mtoto wao; ndipo wakatoa tamko, tunafanya tambiko kwa yeyote aliyehusika kwa kifo cha mtoto wetu, naye adhurike; wakafanya machinjo ya mifugo pamoja na mila zao.

Haikuchukua wiki, yule kijana akaanza kuvimba tumbo; na hatimaye akaenda kukiri ndiye aliyemsababishia umauti mwenzie, na baada ya hapo naye alifariki.

Ikawa wote wamiliki wa lile jengo wamefariki, na hakuna mmiliki mwingine aliyebaki; lile jengo likawa limetelekezwa kwa miaka mingi, na kwa sababu liko sehemu nzuri kibiashara likawa linawavutia wengi, lakini hawajui waanzie wapi kuja kulipata.

Baadaye kukawa na habari za chini chini mara limetaifishwa n.k’’

Cha kujifunza hapa, 'partnership' kwa sisi waafrika bado, mtaanza vizuri, lakini baadaye mafanikio yakionekana kuna kugeukana, kila mmoja atataka awe boss kwa mwenzie.

Leteni stori za vijiweni wakuu, tupate kujifunza
 
Hii nayo niliipata kwenye gahawa,ilitokea maeneo ya buguruni enzi hizo buguruni peusi,kulikua na jamaa wawili walikua wanafanya kazi maeneo ya shaurimoyo,hawa jamaa walishibana kweli kweli kwenye urafiki wao.

Basi bhana mmoja akamuomba mwenzie waje maeneo ya buguruni kutafuta kiwanja ili amfanyie "surprise" mkewe.Hivyo wakaenda maeneo hayo akanunua eneo na shahidi akiwa rafiki yake. Basi ujenzi ukaanza bila ya kushilikisha familia yake mpaka ikafika kwa asilimia 75,yule mwenzie akaingia na tamaa akafanya ya kuyafanya akampeleka mwenzie mbele ya haki.

Basi akajimilikisha ile nyumba akazaa na vizazi kwenye hiyo nyumba mpaka mambo yalipovuja mana dunia haina siri ya kiasi hiko mpaka wasijue kabisa jambo lililotendeka, familia ikaja ikatililishwa kwamba hakuna kitu kama hiko.

Ila yule mzee marehemu kwa sasa inasemakana yeye ndio aliutoa huo ushuhuda kabla ya kufa kwa maandishi maana hakuwa na uwezo wa kuongea wakati anaumwa mana alipata kansa ya koo.
 
Maisha haya hakuna kumwamini mtu baki, muamini yule aliyetengeneza bond na wewe, kwa sababu kuna uhusiano wa damu kati yenu
 
Sasa hii ndo bdo mbichi kabisa ...meneo ya makambako mkoa wa njombe....unaambiwa kuna dingi mmoja
Alikuwa anafanya kazi hpo makambako na familia ilikuwa inaishi hpo .....lakin Mzee kuna eneo alinunua na kujenga nyumba kimya kimya bla kushirikisha familia.., though hiyo familia kwasasa haipo Tena mji huo waliamua kurudi home baada ya Mzee wao kupata mwaswahibu ya ajali ambayo ilepelekea Mzee kupoteza kumbukumbu zote za nyuma kias kwamba hata familia hamkumbuki member hata mmoja!!
Picha linaanza baada ya dalali aliyemuunganisha kununua lile eneo kumtembelea hospital baada ya kuckia mteja wake alipata ajali na amelazwa....dalali baada ya kufika pale akakuta mteja wake hamkumbuki...hata alipojaribu kumkumbusha alisema hamfaham na yy yupo pale hospital anaambiwa aliletwa tu hajui nn kilitokea ila kuna huyu mwanamke na watoto wake ndo wananisaidia lakin siwafaham na sijawahi waona .... kumbuka wanaomsaidia hao ni mke wake na watoto wake....Sasa bwana....ndugu dalali baada ya kujiridhisha Mzee hakumbuki kitu ..akatoka pale na kwenda kujenga fence na Kuweka gate ili nyumba ambayo mgonjwa aliijenga Kwa siri paspo familia kujua...mpka Leo hii jamaa kajimilkisha nyumba hiyo .....Sasa wakati wanataniana na mshikaji mmoja kwenye gahawa ndo jamaa akamwambia ww huna utu kabisa umefanya kitu Cha kinyama Sana ....jamaa anajitetea kwamba hiyo ni bahat yake....
 
Hata majambazi,huwa wanapanga vizuri mipango yao,wakifanikiwa kufanya tukio,matatizo huja kwenye mgawo,hapo ndipo hata risasi na visasi huanzia.
 
KIJIWE CHA KAHAWA

Miaka zaidi ya 20 imepita, kuna mkandarasi mmoja wa barabara alikuwa anatembea na mke wa mdosi mmoja. Huyo mdosi alikuwa ana hela na madaraka pia.

Kwa kuwa huyo mdosi alikuwa mzee, na mkewe alikuwa bado binti mwenye utamu wake, akawa ameoza kwa mkandarasi aliyekuwa akipata mawe (fedha) kwa ujenzi wa barabara.

Inasemekana mdosi alikuja kupata taarifa kuwa mkandarasi anatoka na mkewe; Bila kujua hili wala lile, mkandarasi kama kawaida yake, kaingia kwenye kijiwe chake cha kahawa na kuanza kunywa zake kahawa .

Ghafla akatokea mtu kama chizi, akamrarua yule mkandarasi na kitu chenye ncha kali, baada ya kuwahishwa hospitali, umauti ukamkuta. Uchunguzi kuendelea, ikaonekana jamaa aliyesababisha kifo, alikuwa chizi.

Mdosi naye alihamishwa kituo cha kazi, na maisha yakaendelea.
 
Sasa hii ndo bdo mbichi kabisa ...meneo ya makambako mkoa wa njombe....unaambiwa kuna dingi mmoja
Alikuwa anafanya kazi hpo makambako na familia ilikuwa inaishi hpo .....lakin Mzee kuna eneo alinunua na kujenga nyumba kimya kimya bla kushirikisha familia.., though hiyo familia kwasasa haipo Tena mji huo waliamua kurudi home baada ya Mzee wao kupata mwaswahibu ya ajali ambayo ilepelekea Mzee kupoteza kumbukumbu zote za nyuma kias kwamba hata familia hamkumbuki member hata mmoja!!
Picha linaanza baada ya dalali aliyemuunganisha kununua lile eneo kumtembelea hospital baada ya kuckia mteja wake alipata ajali na amelazwa....dalali baada ya kufika pale akakuta mteja wake hamkumbuki...hata alipojaribu kumkumbusha alisema hamfaham na yy yupo pale hospital anaambiwa aliletwa tu hajui nn kilitokea ila kuna huyu mwanamke na watoto wake ndo wananisaidia lakin siwafaham na sijawahi waona .... kumbuka wanaomsaidia hao ni mke wake na watoto wake....Sasa bwana....ndugu dalali baada ya kujiridhisha Mzee hakumbuki kitu ..akatoka pale na kwenda kujenga fence na Kuweka gate ili nyumba ambayo mgonjwa aliijenga Kwa siri paspo familia kujua...mpka Leo hii jamaa kajimilkisha nyumba hiyo .....Sasa wakati wanataniana na mshikaji mmoja kwenye gahawa ndo jamaa akamwambia ww huna utu kabisa umefanya kitu Cha kinyama Sana ....jamaa anajitetea kwamba hiyo ni bahat yake....
Hatari sana, dunia ina mambo ya ajabu sana
 
Back
Top Bottom