Uzi maalumu wa kupeana hamasa ya kuweka akiba/kuzichanga

Merchante

JF-Expert Member
May 9, 2017
1,293
2,681
Wakuu
Kama kichwa cha uzi kinavyojileza hapo juu. Kama mjuavyo wakuu, akiba ni kitu muhimu sana katika maisha,"akiba haiozi".

Lengo la huu uzi ni kupeana hamasa ya kuzichanga mdogo mdogo, uzi huu utasaidia kuweka akiba ya kila tupatacho haijalishi ni kidogo kiasi gani,kisha mwisho wa mwaka huu tutapeana hesabu ya kilichopatikana. Pia kwa watakao hitaji ushauri wa hiyo pesa walochanga wafanyie nini nadhani watapata ushauri hapa hapa jukwaani.
Hata ukipata buku mbili kwa siku,sio mbaya, weka akiba hata 500 sio mbaya, then baada ya muda naamini utapata matokeo chanya.

Tutakuwa tunapeana updates za salio la akiba tulizojiwekea. Huu uzi utakuwa ni msaada kwetu sote kama ulivyo ule uzi wa "ULIANZAJE KUKAA GHETTO" uloanzishwa na Walec

Uzi huu ni kwaajili ya watu wote ila muhimu zaidi kwa wale wapambanaji wadogo, wanangu wa Maghetton uzi huu ni bora pia, wanangu wa gereji, bodaboda, machinga, mafundi simu, nyumba,n.k. Waua Wenger pia uzi unawahusu huu, wabeba box tuko pamoja kuzichanga hapa.

Tusikatishane tamaa, tupo hapa jukwaani kupeana courage na mbinu mbalimbali za kujikwamua kimaisha.

MAMBO YA KUZINGATIA
1: Kupeana updates
2: Hamasa ya kupambana
3: Kupeana mbinu za kujikwamua kwa yule ambae atakua anapitia katika wakati mgumu.
 
Kuweka akiba ni muhimu sana, nidhamu ya fedha ni muhimu pia.
Baada ya kuweka akiba ni vizuri pia kuiweka mipango akiba yako. Kuna mtu anaweka akiba(mfano kibubu) kwa muda mrefu, akija kuvunja anainywea hela yote pombe na starehe ndani ya siku chache tu na yanaanza majuto. Ni vizuri kuielekeza kwenye matumizi yenye manufaa na faida.
 
Naomba nikae siti ya hapa....
1675627871260.png
 
Kuweka akiba ni muhimu sana, nidhamu ya fedha ni muhimu pia.
Baada ya kuweka akiba ni vizuri pia kuiweka mipango akiba yako. Kuna mtu anaweka akiba(mfano kibubu) kwa mda mrefu, akija kuvunja anainywea hela yote pombe na starehe ndani ya siku chache tu na yanaanza majuto. Ni vizuri kuielekeza kwenye matumizi yenye manufaa na faida.
Uko sahihi Mkuu, matumizi sahihi ya akiba yako nalo ni jambo la msingi zaidi.
 
Kuweka akiba kunahitaji commitment, yaani ujitoe kweli kweli vinginevyo unaweka leo kwenye kibubu baada ya wiki unavunja kibubu.

Mwaka huu najikaza
Kila siku naweka 100K
Kuna muda akili inaniambia “unalaza hela chini badala izunguke” ila naiambia niache nataka 50M mwisho wa Mwaka nikijumlisha mchezo wa 1M kwa mwezi
Plus Vicoba viwili
 
Back
Top Bottom