Uzi maalumu wa kufichua matapeli wa mitandaoni

Uzi maalumu wa kufichua matapeli wa mitandaoni

Mim ndo kiboko yao hao ukishajua ni tapeli ww jifanye boya zaid huku ukitafuta mbinu ya kumpiga yeye. ila usimpige zaid ya elfu 20 kwan nao wajanja hawachelew kugutuka mfano: mim nilikulaga 20 yao kizembe tu mpaka wenyewe wakacheka..! Mchongo ulikuaga hiv walinivutia waya wakanipa dili la madawa ya pale TFDA halafu wakajifanya mteja yupo landmark anasubiri mzgo , Mda kdgo akapiga mteja anaulizia mzgo umefka wapi..? Nikajisemea leo mmeumia..! Yule wa mwanzo akanipigia akanambia niende kuchukua mzgo ila nitume laki tano ya kuniandalia risit na hela ya kutolea mzigo getini. Ili nikachukue mzgo nimpelekee mteja tukachukue milion saba tugawane. Nikamwambia daah hela ninayo ila ipo benki na mim hapa nipo posta ATM Card yangu nimeisahau nyumban Bunju kma una elfu 20 nitumie nichukue boda chap niwah kutoa hela tuiwah biashara. akajichanganya akatuma mim chap nikaitoa. Bas kila mara akawa anapiga simu namwambia nakaribia kufika subiri kdgo, akasubir had jion akawa anapiga sipokei bdae ni kamtumia msg 'Bro mim nipo Dar hapa toka bahari ipo Buguruni' akanijibu kwa kucheka.
 
Habari zenu wadau.

Kutokana na kukua kwa matumizi ya Mitandao ya kijamii, kumeongezeka kwa kasi kubwa ya biashara zinazofanyika mitandaoni. Hizi biashara zina manufaa makubwa kwa watumiaji wa mitandao na uchumi kwa ujumla.

Hata hivyo ukuaji wa biashara za kimitandao, umeanbatana kwa kasi kubwa ya biashara za kitapeli. Kila kukicha watu wanakuja na mbinu mpya ya utapeli mtandaoni huku watu wakilia kuubiwa.

Hatuwezi tupia serikali( TCRA) jukumu hili peke yao. Tunatakiwa hata sisi wenyewe kufahamishana juu ya utapeli huu unaoendelea.

Hivyo basi, ningetumia nafasi hii kuwakaribisha nyote tufichue hawa matapeli wa mitandaoni kwa kupost utapeli wao humu tukiwa na ushahidi uliokamilika.

Karibuni nyote.
Screenshot_20220910-152806_Samsung Internet.jpg
 
Back
Top Bottom