Uzi maalumu wa kufichua matapeli wa mitandaoni

Zero Hours

JF-Expert Member
Apr 1, 2011
12,944
18,653
Habari zenu wadau.

Kutokana na kukua kwa matumizi ya Mitandao ya kijamii, kumeongezeka kwa kasi kubwa ya biashara zinazofanyika mitandaoni. Hizi biashara zina manufaa makubwa kwa watumiaji wa mitandao na uchumi kwa ujumla.

Hata hivyo ukuaji wa biashara za kimitandao, umeanbatana kwa kasi kubwa ya biashara za kitapeli. Kila kukicha watu wanakuja na mbinu mpya ya utapeli mtandaoni huku watu wakilia kuubiwa.

Hatuwezi tupia serikali( TCRA) jukumu hili peke yao. Tunatakiwa hata sisi wenyewe kufahamishana juu ya utapeli huu unaoendelea.

Hivyo basi, ningetumia nafasi hii kuwakaribisha nyote tufichue hawa matapeli wa mitandaoni kwa kupost utapeli wao humu tukiwa na ushahidi uliokamilika.

Karibuni nyote.
 
Tatizo watu hawaamini wala kuelimika,
Anaona au kusoma ushuhuda, haamini kesho wanamla kichwa.
 
Hivi kuna ambaye ameshafanya biashara na hawa jamaa?

Nimekuwa na mashaka nao kwa sababu zifuatazo.
1. Bei zao ni chini au sawa na bei za kiwandani.( factory price) sasa wanapataje faida ukiweka cost za usafiri na ushuru?

2. Hawana fixed adress. Wao wanatuma tu bidhaa hakuna service za kufika officini kwao.

3. Hawaoneshi sura zao.

4. Picha za bidhaa wanazopost ni za kudownload mtandaoni sio zao
Screenshot_20201213-101636_Instagram.jpg
 
Saivi wajinga wengi wanadanganywa kujiunga na Smile We care
Wazee wa Network marketing
Kwa wazee wa kubet WAUZA ODDS NI MATAPELI NAMBA 1
Wazee wa Forex kudownload mapene Wauza signal ni matapeli walewale
Nataka kuwasahau wauza Bando bei rahisi 5K unapata GB 10 sahau
Wauza dawa za nguvu za kiume
Wauza dawa za kuongeza maumbile wowowo

Na wengne wengi
View attachment 1648015
Apo kwenye Sure ODDS jamaa angu aliliwa hivhiv 160k na jamaa wa kenya! So sad
 
Huyu ni tapeli 100%. Price ya s20 inaanzia $999 hadi $1,400. Hapa Tz tigo shop bei inaanzia 2million.

Huyu jamaa anauza kwa nusu ya bei ya kiwandani.
Screenshot_20201211-184408_Instagram.jpg
 
0679022868

Hiii no mara ya pili sasa inapiga na kuniambia ni kustomer care wa Vodacom na kunamteja kaingiza pesa kimakosa.

Huna naanza kucheka na kumuuliza iyo no anayotumia ni ya mtandao gani?

Nikishamuuliza ivyo tu anakata simu
 
Bado wanaendelea kutafuta za krismas

Sms toka kwa 0734 556 916

JIUNGE NA CHAMA CHA FR EE MASON (666) BADILISHA MAISHA YAKO KWA MAELEZO ZAIDI PIGA SIMU (0624192849 0711679085) ILI KUPATA VIGEZO NA MASHARITI.
 
Kuna matapeli wanatumia jina baadhi ya details za viongozi huko Facebook kuwatapeli watu week hii mdogo wangu wa kike katapeliwa pesa kwa style hiyo na bahati mbaya alifanya siri toka mwanzo ikawa ngumu kugundua mpaka pesa zilipopigwa mala mbili ndo akastuka.
Mbaya zaidi tapeli huyo ambaye anatumia jina la MH. JOKATE MWEGELO ( MKUU WA WILAYA YA KISARAWE) alimpa namba na wakawa wanawasiliana mpaka video call akijifananisha kama JOKATE na amemtumia mpaka copy ya kitambulisho cha kura na baadhi ya picha ambazo binti aliamini kabisa ni Jokate.
Mwisho wa siku binti aliambiwa anapewa pesa yoyote anayotaka ya mtaji wa biashara akaomba apewe laki saba huyo Jokate fake akamwambia atume hela ya kujaza form pamoja na taratibu za usajiri akaambiwa atume elfu 65 na akawatumia ( ingawa nahisi alishawatumia zaidi) maana binti bado mshamba na ni msiri sana kiasi ambacho haikuwa rahisi kugundua mpaka siku ambayo nilimfuma live akiongea na simu na sauti ya kike ikimwomba atume pesa iliyobaki na yeye akilalamika kuwa wamemtapeli maana kama pesa alishawatumia lakini wanamzungusha na wanataka pesa nyingine zaidi!
Ndio tulipombana sana na kukagua simu yake tukakuta baadhi ya sms na calls walizokuwa wakiwasiliana na huyo tapeli.
0656420459
Hiyo ni namba wanayotumia whatsapp
Japo sometimes walitumia namba tofauti
Lakini hii ndo inapatikana zaidi na hata whatsapp na ameweka dp picha ya Mh. Jokate.
Na mpaka sasa inapatikana hivyo kama kuna wataalamu wanaoweza kuunda mbinu za kufuatilia wakamate hawa matapeli wa facebook wanaotumia majina ya viongozi kuibia watu wanaweza kucheck hiyo namba wakaanzia hapo.
Tulijaribu kuwashirikisha police kama unavyojua hawa police wetu walitaka hela kwanza
 
SMS kutoka kwa +255 734 557 527

( 666) jiunge na mtandao mkubwa wa matajiri duniani bila kumwaga damu kujiunga piga namba no, 0673360341 Kwama helezo zaid piga
Kuna mtu aliwahi kunichekesha sana kipindi cha nyuma, umenikumbusha baada ya kuwa umeweka hii namba hapa Jukwaani. Ni kwamba kuna tukio liliwahi kutokea Prof. Ibrahim Lipumba alitishiwa kwa simu na mtu ambaye hakuweza kumfahamu ni nani. Taarifa hizi zilitolewa na vyombo vya habari kwenye taarifa ya habari ya saa 2 usiku. Ni zamani kidogo na watu bado walikuwa hawajazoea sana haya mambo ya mitandaoni, na ni kipindi ambacho watu walikuwa wanatumia laini ambazo hazijasajiliwa, laini zilikuwa zinauzwa hadi barabarani, unanunua laini halafu unaweka moja kwa moja kwenye simu.

Sasa bwana, namba fulani ikawa iemtishia Profesa halafu ikatolewa public na vyombo vya habari. Baada ya kuwa imetolewa, mimi nikawa prompted kui-beep nione kama kweli iko online, halafu baadaye nikajishauri nikaacha kwa kuhofia kwamba unaweza ukai-beep halafu ukaonekana kwenye system ya mawasiliano kuwa umekuwa una mawasiliano nayo tangu siku nyingi, halafu ikabidi uanze kusaidia uchunguzi. Kumbe wakati ninasita kui-beep, kuna jamaa yangu mwingine naye tena wakati huo huo naye alifanya hivyo hivyo kama nilivyofanya mimi. Kesho yake tunakuja kukutana ofisini bahati nzuri tukawa tunashare naye incidence ya tukio hilo. Baadaye anakuja kuniambia kuwa alitaka kui-beep namba hiyo halafu akasita, exactly kama nilivyofanya mimi. Baada ya kubadilishana taarifa za tukio hili, tulicheka sana.

Hata hapa naamini kuna watu wengi sana watakuwa wame-beep hii namba!
 
Back
Top Bottom