Nasubiri comment ya
Kiranga hapa
Maombi na shukurani kwa nchi yenye watu wengi wenye matatizo ya kisaikolojia na wataalamu wachache sana wa matatizo hayo, yanaweza kuwa ni kitu pekee kinachokaribia therapy ya ku address mental health problems.
Ninapopinga uwepo wa Mungu kama fact, hilo halina maana napinga kila kitu kuhusu dini na imani.
Hizi dini na imani mara nyingi zina function muhimu katika jamii, hata kama kinachosemwa katika dini si factually truth.
Dini inaweza kumpa mtu moral compass hata kama Mungu hayupo, maombi yanaweza kuonesha upendo hata kama hayajibiwi. Mtu kusema anakuombea tu kakuonesha upendo wa aina fulani (kama hajasema in a condescending way)
Nitakupa mfano mmoja. Kulikuwa na kijiji, watu wake hawajasoma sana, lakini ni werevu wa mazingira yao, walikuwa an kisima kirefu. Sasa kile kisima kikaathirika na sumu kutokana na water table kuwa contaminated. Watu wakawa wanakunywa maji ya kile kisima wanaumwa. Wazee wakasema, kisima hiki kina majini, msinywe maji yake. Wazee hawajui biology wala chemistry kuelezea chemical na biologivcal makeup ya maji ya kisima kama yana sumu au bacteria, lakini wanajua habari za majini (ambayo hayapo na hayaharibu maji). Na watu wa kijijini hawaelewi Chemistry wala Biology ya kisima, ila ukiwaambia kisima kina majini hawanywi maji.
Sasa akatoka mtu wa mjini, kaelimika. Hakubali uwepo wa majini. Anaenda kisayansi zaidi. Akaambiwa na wale mababu, kisima hiki usinywe maji yake, kisima kina majini, ukinywa maji yake utaumwa.
Yule kijana wa mjini akabisha, akasema hamna majini, wazee hamna elimu. Mimi nitakunywa maji ya kisima hiki kuwahakikishia maji haya hayana majini na ni salama. Akanywa. Akanywa sumu iliyo kwenye maji. Akaumwa vibaya sana.
Watu wa kijijini wasio na elimu wakamcheka sana.
Wakasema unaona, amekunywa maji ya kisima chenye majini, ameumwa.
Sitaki kuwa huyo kijana asiyekubali majini na kunywa maji ya kisima bila kuangalia muktadha.
Maombi na imani, hata kisayansi, ni vitu muhimu. Kuna watu wanapona kwa imani tu katika tafiti za dawa za kisayansi. soma kitu kinaitwa "placebo effect" uone.
Natumai nimekupa kitu kipya na sijajibu kama ulivyotegemea nijibu.