KERO MWAUWASA na urasimu unaofikia kiwango cha juu

KERO MWAUWASA na urasimu unaofikia kiwango cha juu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

johnmashilatu

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2010
Posts
1,252
Reaction score
1,744
Wakati Dunia ikibadilika kwa kasi kwa kujali muda zaidi na kupunguza kutumia muda mwingi kufanya jambo fulani, taasisi nyingi za umma bado ziko zama za mawe.

Ndugu zangu hawa wa Mwauwasa, wanadai kwenda na teknolojia lakini, sijui wanachofanya kina makusudi au hawajui.

Ukitaka huduma ya maji " safi" unaambiwa tumia "system". Huko kwenye mtandao wao, hawakuwezeshi kutuma maombi na ili upate, wanakuelekeza nenda steshinari, ukatengane na 5000.

Ukituma, hakuna muda maalum wa maombi yako kushughulikiwa. Utasubiri kudra za mwenyezi Mungu.

Nina wiki karibu tatu nimetuma na kupewa namba 325058579, naendelea kusubiri, wahusika waje kufanya survey ya gharama za kuunga maji umbali wa mita 10 kutoka kwenye bonba linalopitisha maji!

Kama ninaweza subiri mwezi ili labda pengine " surveyor" atakuja, itachukua muda gani kuja kupata hiyo huduma?.

Mwauwasa, jifunzeni kwa Tanesco ambayo pamoja na chabgamoto zao, bado wana utaratibu mzuri wa ku- engage na wateja wao, kupitia majukwaa tofauti.
 
Back
Top Bottom