Uzi maalum: Visa vilivyowahi kukutokea ukipata tiba kwa mganga wa kienyeji

kuna jirani yangu tumemzika juzi..alikuwa anaumwa akaenda kwenye zahati zetu hizi wakampima wanachojua majibu yakatoka kuwa hana shida yoyote ....mzee akahisi kuna watu wanamtengeneza so akaitwa mganga kutoka mikoa ya kusini huko...mganga kufika akamwangalia mgonjwa wake akawaambia huyu kapigwa zongo ..na kuliondoa inabid akamuliwe ndimu kumi na kunyweshwa.....familia ikatafuta ndimu kumi zenye maji ya kutosha ..mganga akaandaa dawa ..mgonjwa akanyweshwa maji ya ndimu 10... kwani mzee alilala sasa...mzee hakuchukua hata masaa akanyooka..mganga akala kona hajulikani alipo na mzee next day kabla jua halijazama tulimpika chepe...habari ikaishia hapo...

kumywesha mzee wa watu maji ya ndimu kumi ...si mchezo
 
Wakuu habari,pasi na shaka wengi wetu tumewahi kuhudhuria kwa mganga/waganga wa kienyeji kwa shida mbalimbali za miili yetu na maisha kwa ujumla.Nishee nanyi visa/madhira niliyowahi kuvisikia toka kwa watu wangu wa karibu ktk kutafuta uzima kwa wataalamu hawa;

1. Mzee jirani alipelekwa baharini usiku wa saa8 ili kuaguliwa,huko alikutana na watu wengi wakiwa na waganga wao,hakuna aliekuwa bize kumshangaa mwenzake,gari za kifahari zilikuwepo,kila mtu alikuwa na vifaa vyake vya kazi,mwenye mbuzi,kondoo,kuku,vyungu n.k,
Tiba ya mzee ilianza,mtaalamu alichanganya dawa kwenye chungu chenye moto,ubani na madawa ya marashi yanayopalia puani,sharti alilopewa mzee ni aingie Baharini mpaka maji yafike usawa wa shingo yake ndio atupe kile chungu kwa mbele na asigeuke nyuma.

Shida mwanaharamu,mzee alijitwisha chungu,hatua moja baada ya nyingine akielekea kwenye maji ya shingo(size),huku akipaliwa na moshi wa dawa na joto kali la mvuke kutoka kwenye chungu alichojitwisha kichwani.

Hakuna masharti mepesi kwa mganga,alipofikia maji size ya kifua chake,mawimbi yalianza kumpiga usoni na kumfanya ashindwe kupumua vizuri,hivyo alikitupa chungu kilichokua na dawa kabla ya kufikia maji ya shingo na kuharibu tiba ile. Mganga alimfokea sana na kumlaumu kwa kuharibu tiba. Ilibidi ipangwe siku nyingine kwa ajili ya kutekeleza tiba ile

2. Kisa cha pili,Mzee safari hii hakurudi kule kwa awali,ila masharti hayakuwahi kuwa mepesi,mganga wa pili alimtaka mzee akaoge barabarani,barabara ya lami kwenye pilikapilika za watu na biashara. Dawa iliandaliwa kwenye beseni ikiwa kwenye hali ya kimiminika.

Sharti likijirudia la kujitwisha(rejea mganga #1),safari hii akitokea nyumbani kwake mpk barabarani,kama ujuavyo beseni likijaa maji,ile kujitwisha beseni likamwaga maji tiba ikaharibika kwani hakutakiwa kumwaga hata tone mpk afike barabarani ambapo angetakiwa kuoga akiwa uchi wa mnyama.

Mganga alirudia kutengeneza dawa nyingine,safari hii alimtwisha mwenyewe ili tiba isiharibe,mzee alijitahidi kutembea kwa umakini na hakumwaga hata tone la maji mpk akafika barabarani.

Note:hakuna raia anaemwona ila yeye anawaona kwa jinsi alivyotengenezwa na mtaalamu kishirikina)

Kufika amefika,ishu ikawa atavuaje nguo aoge na yeye anaona kama watu wote wanamuangalia,mbaya zaidi sio mbali na nyumbani kwake,baada ya tafakuri dawa hii ilimwagwa na mzee akarudi nyumbani kupumzika
Visa ni vingi,hatuwezi kuvimaliza kwa andiko moja.

Ongezea kisa chochote ulichowahi kukutana nacho au kukisikia kwenye kutafuta tiba/uzima,mali au shida yoyote iliyokupeleka au kumpeleka jamaa yako kwa mganga wa kienyeji

................
Sheikh23
Huyo ''mzee jirani'' bila shaka ni wewe ila umezunguka. Huwezi kujua details zote hizo pasi ya kuwa ni wewe.
 
Shushen nondo za kwa waganga watu wajifunze
Kuna Mganga niliwahi kwenda baada ya kunipa dawa akaniambia unatakiwa isiongee na mtu kuanzia Asubuhi Hadi jioni

Basi ikanibidi nikae pale pale kwa Mganga, nakumbuka alikuja jamaa tunaye fahamiana naye akaanza kusalimia nikavunga sikuitikia akanza kunisemesha sikumjibu akajua huenda jamaa kapewa masharti akaingia ndani kwa Mganga.
Kimtindo nilifanikiwa Lile sharti.
 
Kuna Mganga niliwahi kwenda baada ya kunipa dawa akaniambia unatakiwa isiongee na mtu kuanzia Asubuhi Hadi jioni

Basi ikanibidi nikae pale pale kwa Mganga, nakumbuka alikuja jamaa tunaye fahamiana naye akaanza kusalimia nikavunga sikuitikia akanza kunisema sikumjibu akajua huenda jamaa kapewa masharti akaingia ndani kwa Mganga.
Kimtindo nilifanikiwa Lile shar

Alikutatulia shida yako?!😅
 
Kuna mwaka mmoja 2003 nadhani, alikuja mganga mmoja toka Congo ,alifikia hotel inaitwa Triz Motel pale mbezi beach( YA MAREHEMU KIMAMBI ) Inasemekana yule mganga walimleta kina J. Kapuya kwajili ya ishu zao ,

Palikuwa na watu wengi maarufu wanaenda pale kwa huyo mganga ikiwemo wasanii,
Sasa bwana namimi kipindi hiko Kuna ishu ilikuwa inanitatiza ,kwaiyo kwa mujibu wa mganga ilipaswa nisafishwe nyota Kwanza kabla ya mambo mengine, Mi nikamkubaria mganga,

Basi akaniandikia vifaa ambavyo vinaitajika kuvileta, masufulia makubwa mawili mapya kabisa, na hela za sarafu za zamani, nikamuachia Laki moja ya vifaa na ya kazi yangu,
Basi akinipangia siku nzuri kwangu kufanyiwa kazi ni Alhamis,
Basi ikafika alhamisi saa nne nikaenda ,kufika pale ndani kulikuwa na msanii Kanumba na dada mmoja hivi nae ni maarufu Hadi leo ,na yule mama Abduli muigizaji,
Basi walivyotoka wao ikiwa zamu yangu kuingia kwa mganga ,kufika akaniambia ushafika boss,haya kaa hapo subiri niwashe moto dakika sifuri, basi bwana akawasha moto akabandika maji kwenye ile sufuria mpya ,

Baada ya dakika kadhaa maji yakachemka haswaa, akayamimina kwenye ndoo, akatumbukiza na zile sarafu za zamani mnemne,
Tukaenda sehemu maalum hili aniogeshe sasa maji Yale yenye dawa,

Kufika kule pahala pakuogea, Sasa bwana kabla yakuanza kuniogesha kwanza nikatia mkono kwenye ndoo ,maana maji pamoja nakuwa kayapooza,hila yalikuwa yanafuka moshi balaa, kutia mkono aisee nikakuta maji Ni ya moto mno,

Nikamuambia Kaka haya maji Bado Ni ya moto Sanaa yatanibabua mwili kabisa Ni hatari,
Eti akasema hakuna wewe tu muoga,haya unayaona ya moto,lakini kwa uwezo wa mizimu nikikumwagia tu hayaunguzi"

Nikamuambia hapana tuyapooze tu mkuu, Basi akayapooza lakini kiroho upande,

UNAJUA HAWA waganga ukiwaendekeza wanaweza wakakuua hivihivi aisee,

sikuile jamaa Kama angenimwagia Yale maji huenda saizi naitwa marehemu au ni mlemavu fulani!!!
nimecheka kufala
 
Me jamaa yangu ndo aliniadisia alipewa dawa ila sharti lilikuwa rahisi kwa akili za kibinadamu kwamba ahakikishe hakojoi ikiwa mfukoni japo unatakiwa kila uendapo iwe mfukoni, Yaani ukihisi haja make sure unaitoa kwanza pembeni ndipo ujisaidie, Jamaa ndani ya week tuu akachana mkeka.
 
Yuko mdada mmoja miongeaji Kama kasuku. Huyu Dada haishi kugombana na mumewe. Kila siku Ni ugomvi. Basi Dada alikwenda kwa mganga ili asije akaachika. Mganga alivyomjua Ni chiriku alichukua koa ya vile vijikonokono vya baharini. Na kuambiwa ukimuona mumeo anarudi nyumbani, chukua hiyo koa itie mdomoni halafu weka maji kinywani. Hayo maji usiyateme Wala usiyameze. Yakae mdomoni mpaka mumeo aondoke ndio ukayateme na kuihifadhi hiyo koa.
Baasi bwana, kila mume akirudi anamkuta wife Yuko kimya. (Kumbe anamaji mdomoni) mpaka jamaa akaanza kushangaa kulikoni bibi haleti maneno machafu??
Hali iliendelea ya mke kutoongea na kutoleta ugomvi Hadi ndoa ikawa ya furaha.
Mpaka leo yule Bibi anaamini yule mganga Ni kiboko.
 
Kuna waarabu walitoka Oman wakiwa na na ramani ya kahama! Wakanitafuta niwap3l3ke kahama kwa mganga fulani ambaye sasa ni marehemu.

Safari ilianza na balaa sababu tulipata seat zile za mwisho kabisa, bus najimunisa, kama mnakumbuka kuna kipande cha dodoma kilikuwa na vumbi tena kipande kirefu, basi tulipofika gairo wanauliza bado? Nikawaambia kahama tunafika kesho na tunatembea usiku na mchana wakachoka..kipindi hicho kahama mnaingia asubuhi, chombo ikifika nzega inalala.

Kufika kahama

Kahama pale tulifikia kwa mwenyeji wetu ambaye alikuwa ana hostel kabisa, yaan kama ana shule, kuna paka weusi zaidi ya 100 wateja si chini ya 50 wanakaa hapo hapo wanahudumiwa mpaka wakipata nafuu na pia ana hostel zingine nje ya mji, kifupi jamaa alijipanga

Aisee nilipapenda kwa yule jamaa maana asubui anachinja kuku20, utakunywa supu, kuku rost, kuku ya kuchoma na za kukaanga, sasa sijajua ilikuwa ni nili ya wale waarabu ama laa,

Tiba ikaanza wakawa asubuhi wanatibiwa na jioni, ila kuoga wanatakiwa wakaogee mlimani kule kuna viwanda vya pamba kule juu, ikawa hivyo , hapo mm nafanya utalii wa ndani tu maana nishavuta fungu langu tangu nikiwa dar, nakumbuka walinipatia laki 9 .2007 laki 9 si haba..kila kitu juu yao kwenye safari.

Sasa kuna siku yule mwarabu ( alikuwa ni meneja kwenye visima vya mafuta huko kwao sasa kilichomleta huku ni kwamba kuna mzungu kaletwa kuziba nafasi yake, yaani yeye anashushwa cheo anakuwa chini ya mzungu, mwarabu hilo jambo hakutaka hata kulisikia akafikia uamuzi wa kuja Africa kuroga, kaja na location kabisa anataka apelekwe kahama kwa (fulani)

Sasa wakati ameshatoka kuoga kule juu ya mlima ( hiyo siku alitakiwa aoge saa 4 asubui ) tunarudi kwa mtaalam kwa bahati mbaya sijui ama bahati nzuri mi sielewi lakini yule mjuba aligusa upupu ule uko kama ukwaju hivi, basi ulimuwasha sana mpaka ngozi ikawa nyekundu, akaniuliza hii ni nini? Nikamwambia huu ni upupu! Upupu ndio nini nikamwambia upupu ni upupu tu na kazi yake ni kama hiyo unayoiona. Ajabu akasema tafuta watu wanichumie hii kitu, itanifaa na dawa basi siogi tena na kama tunaweza kupata ndege inayoenda dar leo hii fanya taratibu tuondoke leo hii hii hii upupu itanifaa sana.

Badi tukarudi mpaka kwa mtaalam tukamwelekeza, jamaa ana connection vibaya mno, wakafanya booking, ya ndege ya kesho yake hawakutaka tena bus maana walifika kahama na vidonda mikononi.

Mimi sikuwa na mzuka na ndege, nikawaambia ppesa yangu ya tiketi nipeni mm nitarudi na bus, tukaachana hivyo,

Yule mwarabu sasa baada ya kufika huko kwao alichokifanya anakijua mwenyewe, kwa maelezo yake, likizo ilipoisha maaana alikuwa na likizo ya wiki2, aliwahi ofisini mapema sana akausambaza ule upupu ofisi nzima asema na mwingine akaweka kwenye AC! Akasepa akaenda kufanya mishe zingine,

Mzungu alipoingia ofisini, akawasha Ac akawa anakung'uta mafile mara kagusa huku mara kule, kilichomkuta yule mzungu anajua mwenyewe. Anasema alianza kuwashwa alipiga kelele akawa kama ana kichaa na kule ni jangwani, ikabidi ifanyike jitihada ya kumfunga kamba kumtia ndani ya ndege ya kumpeleka mjini, na hata alipofikishwa hospital na kupata matibabu alikataa kufanya kazi Oman kabisa, ikabidi mwarabu arudishwe kwenye ofisi yake..

Upupu ndio uliomsaidia na si tiba ya yule gagula.
 
Bila shaka hii story ina part 2
 
Back
Top Bottom