Uzi maalum: Sintosahau zilizokukumba maishani mwako

Melki the Storyteller

JF-Expert Member
May 3, 2022
5,700
9,779
Katika maisha ya kila siku, kuna matukio ambayo hutokea wakati wa kusongesha gurudumu la maisha ya hapa duniani ambayo hayawezi kusahaulika kirahisi katika kumbukumbu zako! Yanaweza kuwa ya furaha ama huzuni!

Uzi maalumu kwa ajili ya kushirikishana matukio usiyoweza kuja kuyasahau kamwe!

Sintosahau,
Wakati nikiwa kidato cha sita karibu ku graduate, iliandaliwa sherehe ya graduation ya dini ya YCS! Hivyo ukumbi wa shule uliandaliwa vyema kwa ajili ya sherehe ile! Vipaji mbalimbali vilinolewa siku chache nyuma! Kama ilivyo desturi, shule za wakina dada zilitumiwa mwaliko! Kwa kuwa mimi nilikuwa mtumikiaji, sikukosa nafasi ya ku perform katika sherehe ile, nilipita bila kupingwa wala kufanyiwa liheso yoyote, isitoshe nilikuwa msanii bora wa shule kwenye sherehe za clubs! Pia hata viongozi wa dini na watumishi walinifahamu zaidi!

Siku ya sherehe ilifika, baada ya ibada niliitwa kwenda kuperform mbele ya walimu, watumishi wa dini na wanafunzi wenzangu wakiwemo akina dada wa shule zaidi ya tatu! Niliperform nyimbo miwili, (samahanini wanajukwaa kama nitakuwa nje ya maadili ya forum, ama nitakuwa nimeeleza kitoto zaidi) Iyola na matatizo za harmonize! Baada ya performance kuisha kutoka kwa walioandaliwa, ulikuwa ni muda wa mgeni rasmi, Paroko, kuzungumza! kwa kuanzia alisema, "leo nimeona ni jindi gani vijana wangu wanavyoporomoka kimaadili na kiroho, mtu anapata ujasiri wa kuimba mapenzi mbele ya watumishi?, fulani njoo hapa mbele, mwalimu mmoja aniletee fimbo nzuri!"

Kilichofuata ni bakora kumi za nguvu mbele ya kadamnasi! na kuungamishwa mbele ya watu wote! Mbele ya watoto wa kike! Kwa upande wangu, kutokana na aibu ile, sherehe iliishia pale! Nilirudi bwenini!

Sintosahau!
 
Huu uzi uungwe na ule ' Ni jambo gani lilikufanya ujute sana' maana zinafanana
 
mim nipo chalii la 7 nikashilikiana na mwenzangu tukaingia store wakati msos wa walimu na vinywaji vimehifadhiwa tukaiba ubwabwa tukaweka kwenye mfuko wa rambo na soda kama 10 mwenzangu kaenda na mzigo huyooo ile mim natinga miguu chini nakutana na sura ngumu kumbe ni afande wa shule weee alinitoa nduki hareee
 
nilikuwa napita sehemu flani kijijini kwetu sehemu wanadai kuna majini usiku saa6 nikasikia harufu ya marashi na joto kali vinyweleo vya mwili vikasimama nilikuwa nimelewa nikapita salama kwenda kumuhadithia bibi yangu akaniambia hilo lilikuwa jini na inaonekana lilikuwa linasali bahati yako ulilewa likaona nuksi acha ipite hiyo ndio salama yako
 
nilikuwa napita sehemu flani kijijini kwetu sehemu wanadai kuna majini usiku saa6 nikasikia harufu ya marashi na joto kali vinyweleo vya mwili vikasimama nilikuwa nimelewa nikapita salama kwenda kumuhadithia bibi yangu akaniambia hilo lilikuwa jini na inaonekana lilikuwa linasali bahati yako ulilewa likaona nuksi acha ipite hiyo ndio salama yako

Kumbe Pombe na majini ni maadui!!
Mambo mengine yanafurahisha...
 
Sito sahau siku niliyonusurika kuuliwa na Police wa kizungu South Africa..
 
Back
Top Bottom