kisokolokwinyo20
JF-Expert Member
- Apr 15, 2019
- 472
- 422
Habari Wakuu,
Ni kipindi kingine tena cha mwaka ambapo kama ilivyo ada kunakuwa na Maonesho ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Sabasaba.
Kupitia maonesho haya, wafanyabiashara na watoa huduma mbalimbali kwa jamii hupata nafasi ya kujinadi kwa shughuli mbalimbali wanazozifanya.
Ni ukweli usiopingika kuwa maonesho haya yana tija sana katika kuinua uchumi wa nchi kupitia biashara zinazofanyika hasa bidhaa za viwandani. Lakini pia kwa watoa Huduma wengine hunufaika kwa kupata mirejesho mingi kutoka kwa wapokea huduma zao.
Kwa mwaka huu wa 2019, maonesho haya yameanza vizuri ikiwa ni pamoja na wanaomiliki majengo/mabanda kukamilisha maandalizi yao mapema na wachache ambao wanamalizia matayarisho kwa hatua za mwisho.
Leo ikiwa ni siku ya kwanza tayari kumechangamka na kumependeza.
Karibuni wananchi wenzangu tujionee na kuwaunga mkono wajasiriamali wadogo, wakubwa na wote wanaojihusisha na kujitangaza katika viwanja hivi.
Nawasilisha.