nimeumizwa mno kumshuhudia mzee mmoja akiachwa na magari mawili yaliyokuwa katika haraka zao za kukimbilia abiria vituo vya mbele.
'achana nae atatuchelewesha huyo'!
'unaweza kuta ametoroka tu kwao bila kuaga wanakuja kutuhangaisha sisi huku'! hayo ndo yalikuwa maneno yao.
kilichoniuma zaidi ni kuwa mzee namfahamu, ni mzima kabisa kiakili ingawa mwili hauko bara bara kutokana na uzee....huwa anatembea kwa shida kidogo! safari yake hii alikuwa anaelekea kwa mtoto wake kupata msaada wa matibabu. viti kibao vya magari vilikuwa vitupu kabisa.....walimwacha mzee wa watu kinywa wazi ameshangaa huku wao wakiendelea na safari yao kwa vicheko.
tuwatunze na kuwaheshimu wazee wetu jamani, tunaelekea huko huko kwa kasi ya ajabu kabisa! tunaweza kujikuta tunalipwa, uzeeni kwetu, haya haya tuwatendeayo sasa hivi!!