gracious86
JF-Expert Member
- Mar 25, 2011
- 437
- 54
wapendwa,hivi kama mwanamke amejifungua kwa operation,anaruhusiwa kujamiiana baada ya muda gani? Coz,kuna mshono tumboni, na hata kama mshono utakuwa umepona,kutabaki na kovu! Je,hii haitaathiri ktk kufanya mapenzi? Au mshono ukipona,inaruhusiwa? Help..
==================================================================================================================
==================================================================================================================
============================================================================================================Kimaumbile...hakuna tatizo lolote kuanza kujamiiana baada ya mama kumaliza arobaini (puerperium) ambazo kwa kawaida ni wiki 6. Ila kuna watu huwa wanachelewa zaidi kwa sababu za kimila, desturi, tamaduni etc.
Mama anapojifungua kwa operation anakuwa na kovu tumboni (hili ni kovu la nje kwenye ukuta wa tumbo/ngozi) na kovu la kwenye kizazi (kovu la ndani). Tatizo ni hili kovu la ndani, na tatizo lake huwa iwapo mama huyo atapata ujauzito tena, kizazi huwa kinatanuka, na wakati wa kujifungua kina weza kuchanika kama madaktari wake hawatakuwa makini!
Kovu hili la ndani halina tatizo lolote kwenye kujamiiana pindi inapopita aroabaini/puerperium, Uume hata uwe mkubwa vipi huwa unaishia kwenye uke tu, haungii kufikia kizazi kwani kuna shingo ya kizazi (cervix) ambayo utenganisha uke na kizazi. Kwa hiyo hamna jinsi yeyote uume ukaumiza kovu la ndani au kulichana.
NB: Kubeba uja uzito mwengine kabla mtoto hajafikisha miaka miwili kunaweza sababisha matatizo katika ukuaji wa mtoto au hata kwako wewe wakati wa uzazi. Kwa hiyo kama una mpango wa kuanza kujamiiana mapema, tumieni kinga (condom) au njia nyingine ya uzazi wa mpango ili kuepusha ujauzito wa mapema.
Bw. Liwa nimepata kusikia kuwa kama Mwanamama mjamzito akigundulika ana VVU pendekezo pekee la uzazi wake ni kwa njia ya upasuaji ili kuepusha maambukizi ya VVU kwenda kwa mtoto? unasemaje juu ya hili?
Mama mjamzito mwenye maambukizi ya VVU anaweza kujifungua kwa njia ya kawaida au kwa operation kutokana na sababu kama nilizozitaja kwenye thrad zangu zilizopita. Inajulikana kisayansi kwamba mtoto anaweza akaambukiwa VVU toka kwa mama wakati akiwa tumboni (kiasi cha 10%), wakati wa kujifungua (njia ya kawaida kiasi cha 25 - 30%), na wakati wa kunyonya.
Kwa hiyo basi, mama akijifungua kwa operation anapunguza uwezekano wa maambukizi kwa mtoto wake, ndio maana kuna kina mama/familia nyingine ambazo wameathirka huwa wanaamua kujifungua kwa operation. Lakini challenge ni kuwa hatujawa na uwezo wa kupima mtoto VVU kabla hajazaliwa, kwa hiyo waweza fanay operation wakati mtoto keshaambukizwa tumboni!
Ushauri wangu: Ni vyema mama akapima afya yake mapema (anapoanza clinic) ili kama ameathrika apewe ushauri na kujiungana huduma za kuzuia maambukizi ya VVU toka kwa mama kwenda kwa mtoto (PMTCT) ambayo yanapatikana bure katika vituo viingi tu vya kutolea huduma za afya hapa Tanzania. Huko atashauriwa jinsi ya kupunguza maambukizi wakati wa kujifungua na wakati wa kunyonysha.
Nauliza tafadhali.Je mwanamke aliyezaa kwa operation mimba ya kwanza anaweza kuzaa bila operation katika ujauzito wake wa pili?
Nilishajibu hili swali kwa kirefu humu JF..kama anvyosema dada Lizzy: inategemea na sababu ya mama huyu kujifungua kwa operation kwa mara ya kwanza. Kuna sababu zinazojirudia rudia mfano maumbile yasiyokidhi ya nyonga ya mama mara nyingi kwa kina mama wafupi (150cm or below), ulemavu unaothiri nyonga etc...na kuna sababu zisizojirudia mfano mtoto mkubwa, mtoto kuchoka, mama kuchoka, mtoto kufungwa na kitovu shingoni, kifafa cha mimba etc.
Kama mama alifanyiwa operation uzazi wa kwanza kutokana na sababu zisizojirudia, huwa anapewa nafasi ya kujifungua kawaida kwenye uzazi wa pili lakini chini ya uangalizi wa karibu wa daktari, kwani kovu la ndani linaweza chanika wakati wa uchungu na kuhatarisha maisha ya mama na mtoto. Wapo wengi tu wanajifungua kawaida baada ya operation katika uzazi wa kwanza.
Lakini kama alifanyiwa opeartion kutokana na sababu zinazojirudia, basi uzazi wake wote utakuwa wa operation, na inashauri afunge kizazi baada ya kuzaa mara tatu kwa operation!
Ni kweli wapo kimna mama kadhaa wanaoamua kujifungua kwa operation, kama unaweza mudu gharama unalipia na unajifungua kwa operation bila kuonja adha ya uchungu. Ila madhara yake ni kama niliposema hapo juu, unakuwa na kovu kwenye kizazi ambalo mara zote litahatarisha maisha yako na ya mtoto wakati wa kujifungua!