Mwana CCM.
Member
- Jan 4, 2011
- 83
- 10
Mimi na mke wangu katika suala la uzazi tulipanga kama Mungu akitujaalia tuwe na watoto wawili tu. Na miezi mitatu iliyopita tulijaariwa kupata mtoto wetu wa kwanza kwa njia ya operation hii ilitokana na njia kutokufunguka kwa wakati. Sasa tunaambiwa mtu akijifungua mtoto wa kwanza kwa operation hata wanaofuatia watapatikana kwa njia hiyohiyo hasa ukizingatia mke wangu ana umri wa miaka 33 sasa. Sasa tupo kwenye wakati mgumu wa kuamua kama tuongeze mtoto mwingine au la! na woga wetu unajikita katika uvumi unaosema mwanamke akijifungua kwa njia ya upasuaji kwa zaidi ya mara moja ni hatari sana. Naomba ushauri kama tupange kuongeza mtoto au lah?