Uzanzibari + Utanganyika = Utanzania

Uzanzibari + Utanganyika = Utanzania

Watanganyika tumekaa kimya Sana kwa muda juu ya chokochoko zenu na Sasa mnavuka redline kwanza huwa nashangaa kitu gani kinacho wafanya mjione watu special Sana enyi Wala ulojo?

Chuki zenu za wazi kwa watanganyika ni udini ulio zaa ubaguzi na mwisho mkatengeneza makundi ndani ya nchi yenu wenyewe sijui huyu mkaskazini sijui huyu mkusini ujinga tu umewajaa.

Kwanza hamchangii chochote kwenye muungano rudini kwenu.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app

Warudi kwao, waende wapi?
 
Ni walalamishi sana,
Sehemu yenye watu milioni na nusu Bunge la ina wabunge wengi kuliko Mwanza yenye watu zaidi ya milion tatu,

Na wanalipwa sawa na mbunge kawe yenye watu zaidi ya milioni,
Dah hatari mkuu imagine ukifika pale feri yao lazima uulizwe kitambulisho kama Huna basi barua ya mwenyekiti wa serikali ya mtaa au hata card ya benk kutoka kwao kuja huku bara unapita tu sasa sijui maana ya muungano ipo wapi.
 
Wana haki, asilimia zaidi ya 90 zanzibar ni waislamu, sasa unategemea asiekua muislamu ajichomeke mule! Kumbuka zanzibar ina rais wake, na ni nchi na sio mkoa ama jiji.
Sasa kama wanajua wana serikali,rais na nchi yao kwanini wasitulie kwao??Wanalalamika nini ??Kila mtu akae kwao,sasa tumewachoka wanatakiwa kulitambua hilo.
 
Hv kati ya Tabora na Zanzibar ipi ni kubwa kieneo.?
Tabora?! Hivi upo serious kabisa unafananisha ukubwa wa tairi la toroli na tairi ya nyuma ya trekta?!

Zanzibar ndio mkoa mdogo kuliko miokoa yote hapa Tanzania.

Hata Dar es salaam tu ukifananisha na Zanzibar havifikiani hata nusu. Dar inakuwa ni kubwa sana.

Zanzibar ni makelele tu ila hakuna nchi pale. Maana hata tukitengana nao watajikuta mikononi mwa taifa jingine na watageuzwa wilaya kabisa bila mamlaka yoyote.
 
Sasa kama wanajua wana serikali,rais na nchi yao kwanini wasitulie kwao??Wanalalamika nini ??Kila mtu akae kwao,sasa tumewachoka wanatakiwa kulitambua hilo.

Kumbuka huo ni muungano, na wanapoona dhulma inatendeka wana haki ya kusema. Hata wewe ungelikua ni mzanzibar usingekaa kimya.
 
Kumbuka huo ni muungano, na wanapoona dhulma inatendeka wana haki ya kusema. Hata wewe ungelikua ni mzanzibar usingekaa kimya.
Wanatendewa dhuluma gani! Kila siku ni kulalamika tu na kudeka deka kama vitoto vya miaka miwili!

Kwa nini sasa wasijitegemee kwa kila kitu? Jana nilikuwa naangalia mechi yao ya kirafiki na Uganda; eti wana mpaka wimbo wao wa Taifa!!!

Sasa wanashindwa nini kujiondoa kutoka Tanganyika kwa 100%!!! Wajitenge hata kesho halafu waone kama kuna Mtanganyika atakufa njaa kutokana na huko kujitenga kwao.
 
Huenda wapo tayari kujitenga, lakini mamlaka yenyewe ndio inatia ugumu(Tanzania bara+Zanzibar)
 
Kumbuka huo ni muungano, na wanapoona dhulma inatendeka wana haki ya kusema. Hata wewe ungelikua ni mzanzibar usingekaa kimya.
Sasa dhulma inatendeka wapi kama Zanzibar wana rais wao pia wana rais anayetawala Tanganyika hadi nafasi ndogo za Tanganyika wamezishika wanzazibar pia ardhi wanamiliki bila kizuizi wakati huo watanganyika ni wakiwa hawana serikali, rais wala kiongozi wa kuwatetea na mtanganyika hawezi kuishi Zanzibar bila uraia wa zanzibar.??Pia hawezi kumiliki ardhi zanzibar,Pia kizuri cha mtanganyika ni cha wote ila kizuri cha zanzibar ni cha wazanzibar.
 
Hapana asiejua kwamba Zanzibar inatawaliwa na inabururwa na Tanganyika. Kwa miaka sitiini yote ya Muungano, ndio kwanza Rais aliepo madarakani hivi sasa ndio mzaliwa wa Zanzibar, lakini waliomzunguka ndio walewale, wao ni wengi mmno, wameshaota mizizi minene ndani ya CCM na Serikali zake, anapotumia nguvu zake wao hutumia wingi wao na hujuma zao dhidi yake.

Wapo wenye chuki na uadui kwanini Mzanzibari awe Rais wa Tanzania! Chuki na uadui huu umo ndani na nje ya CCM! Wanasahau kwamba Zanzibar ni nchi kamili iliyoungana tu na Tanganyika ikapatikana Tanzania! Tokea Mwanzo wa Muungano, hapana Mzanzibari aliewahi kuwa kiongozi Mkuu wa Taasisi kuu yoyote ya Muungano, sio Mkuu wa Jeshi, wala Mkuu wa Polisi, wala Mkuu wa Uhamiaji, na wala usiseme hizo taasisi nyengine.

Sisi Wazanzibari kipa umbele chetu sio Muungano wala Utanzania, kwa sababu tunajua wazu kwamba hizi ni njama tu na mbinu za kuumaliza Uzanzibari. Sisi Wazanzibari kipa umbele chetu ni Zanzibar yenye mamlaka kamili.

Hapana asiejua kwamba CCM Tanganyika ni waanzilishi na ni wasimamizi dhulma na ukandamizaji kwa Wazanzibari. Na kinachosikitisha ni kuwaona CCM Zanzibar wameridhia hayo kwa sababu tu ya maslahi yao binafsi wanayoyapata ndani yake.

Wazanzibari kuishi Tanganyika sio lazima pawepo na Muungano, na Watanganyika wanaoishi Zanzibar pia sio lazima pawepo na Muungano. Watanganyika wapo kila nchi duniani wanaishi vizuri tu na wala hapana Muungano baina ya Tanganyika na nchi hizo, na kwa Wazanzibari ndio hivyohivyo. Kilicho bora zaidi na ni faida kwa pande zote mbili ni kuwa na Muungano ambao hauna upendeleo wala malalamiko.

Hata hivyo, mimi siungi mkono na wala sipendi kuona chuki na ugomvi baina ya Watanganyika na Wazanzibari. Mwenyezi Mungu atunusuru tusije tukaja kupigana na kuuwana. Kuepusha hayo, ipo haja ya kuoneshana ubinaadamu na kuwekeana heshima za mila na tamaduni za pale ulipo. Hapana haja ya kudhalilishana wala kudobogoana. Lakini tatizo ni mifumo ya kisiasa ya CCM na Serikali zake, au labda niseme kuwa wanasiasa wengi wa Tanganyika hawana nia njema na Zanzibar.

Ismail Jussa
21/08/2022
Makunduchi Unguja
Kwanza wewe ismail jussa sio mzanzibari ila muhindi tu. Sijui nia yako kuihamisha zanzibar india au uarabuni? Hadi umezeeka unalia na zanzibar huru umeshindwa kukubali wazanzibari karibu wote asili yao tanganyika. Ni wandengereko, wamakonde, wazigua, wadigo, wazaramo, wamatumbi. Wee piga kelele tu hadi mwisho. Mwenzako maalimu seif kapiga kelele hadi mwisho😆😆😂
 
Kwanza wewe ismail jussa sio mzanzibari ila muhindi tu. Sijui nia yako kuihamisha zanzibar india au uarabuni? Hadi umezeeka unalia na zanzibar huru umeshindwa kukubali wazanzibari karibu wote asili yao tanganyika. Ni wandengereko, wamakonde, wazigua, wadogo, wazaramo, wamatumbi. Wee piga kelele tu hadi mwisho. Mwenzako maalimu seif kapiga kelele hadi mwisho😆😆😂
Watu mukishindwa hoja munakimbilia kwenye Ubaguzi.
 
Kwanza wewe ismail jussa sio mzanzibari ila muhindi tu. Sijui nia yako kuihamisha zanzibar india au uarabuni? Hadi umezeeka unalia na zanzibar huru umeshindwa kukubali wazanzibari karibu wote asili yao tanganyika. Ni wandengereko, wamakonde, wazigua, wadogo, wazaramo, wamatumbi. Wee piga kelele tu hadi mwisho. Mwenzako maalimu seif kapiga kelele hadi mwisho😆😆😂

Bhebhe nang'ho!

Tangu umeanza kujitambua mpaka hii leo umepata faida gani kuwachukia/kuwabagua watu weupe!! Au uliambiwa na wapumbafu wasiojielewa kuwa ukimbagua asie mwafrika utatajirika ama kuishi milele!! Jitathmini upya!
 
Pia Jussa kumbuka haya
Mtanganyika hawezi kumiliki ardhi znz,

Ajira za serikali Znz ni za Wazanzibr pekee,

Mtanganyika hawezi kugombea nafasi yoyote ya kisiasa Znz, hata ujumbe wa mtaa, (sheha)

Ukitaka kwenda Znz lazima uwe na kitambulisho, lkn mpemba au muunguja anaweza kwenda popote Tanganyika na kumiliki ardhi na biashara yoyote bila tatizo,
Mzanzibar anaweza kuwa Rais wa JMT, lakini Mtanganyika hawezi kuwa Rais wa Zanzibar, hapa namaanisha mwenye jina kama Mapunda, John, au Mwakyoma,

Rai yangu ni muungano uboreshwe kuondoa maunguniko kama haya ya kina Jussa Ismail,

Mwinyi ni mtu wa Mkuranga, sasa unasemaje Mtanganyika hawezi kugombea Zanzibar? Acheni uwongo. Na majeshi yenu kila uchaguzi yanauwa na kutesa Wazanzibari. Hujawahi kusikia Wazanzibari wanauwa na kutesa Watanganyika.
 
Wanatendewa dhuluma gani! Kila siku ni kulalamika tu na kudeka deka kama vitoto vya miaka miwili!

Kwa nini sasa wasijitegemee kwa kila kitu? Jana nilikuwa naangalia mechi yao ya kirafiki na Uganda; eti wana mpaka wimbo wao wa Taifa!!!

Sasa wanashindwa nini kujiondoa kutoka Tanganyika kwa 100%!!! Wajitenge hata kesho halafu waone kama kuna Mtanganyika atakufa njaa kutokana na huko kujitenga kwao.

Hivi kama jambazi lenye silaha likivamia nyumbani kwako, kati yako wewe mwenye nyumba na hilo jambazi ni yupi amefanya makosa na ni yupi anatakiwa kuondoka?
 
Kila siku kelele tu simuuvunje huo muungano wenyewe sijawahi ona Hata faida yake kwanza,muondoke mtuachie nchi yetu!!! #Mungu ibariki Tanganyika!
 
Back
Top Bottom