aleesha
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 775
- 1,117
Hapana asiejua kwamba Zanzibar inatawaliwa na kuburuzwa na Tanganyika. Kwa miaka sitini yote ya muungano, ndio kwanza Rais aliepo madarakani hivi sasa ndio mzaliwa wa Zanzibar, lakini waliomzunguka ndio walewale, wao ni wengi mmno. Wameshaota mizizi minene ndani ya CCM na serikali zake, anapotumia nguvu zake wao hutumia wingi wao na hujuma zao dhidi yake.
Wapo wenye chuki na uadui kwanini mzanzibari awe Rais wa Tanzania?! Chuki na uadui huu umo ndani na nje ya CCM! Wanasahau kwamba Zanzibar ni nchi kamili iliyoungana tu na Tanganyika ikapatikana Tanzania! Tokea mwanzo wa muungano, hapana mzanzibari aliewahi kuwa kiongozi mkuu wa taasisi kuu yoyote ya muungano, sio Mkuu wa Jeshi, wala Mkuu wa Polisi, wala Mkuu wa Uhamiaji, na wala usiseme hizo taasisi nyengine.
Sisi wazanzibari kipaumbele chetu sio muungano wala utanzania, kwa sababu tunajua wazi kwamba hizi ni njama tu na mbinu za kuumaliza zuanzibari. Sisi wazanzibari kipaumbele chetu ni Zanzibar yenye mamlaka kamili.
Hapana asiejua kwamba CCM Tanganyika ni waanzilishi na ni wasimamizi wa dhulma na ukandamizaji kwa wazanzibari. Na kinachosikitisha ni kuwaona CCM Zanzibar wameridhia hayo kwa sababu tu ya maslahi yao binafsi wanayoyapata ndani yake.
Wazanzibari kuishi Tanganyika sio lazima pawepo na muungano, na watanganyika wanaoishi Zanzibar pia sio lazima pawepo na uumngano. Watanganyika wapo kila nchi duniani wanaishi vizuri tu na wala hapana muungano baina ya Tanganyika na nchi hizo, na kwa wazanzibari ndio hivyohivyo. Kilicho bora zaidi na ni faida kwa pande zote mbili ni kuwa na muungano ambao hauna upendeleo wala malalamiko.
Hata hivyo, mimi siungi mkono na wala sipendi kuona chuki na ugomvi baina ya watanganyika na wazanzibari. Mwenyezi Mungu atunusuru tusije tukaja kupigana na kuuwana. Kuepusha hayo, ipo haja ya kuoneshana ubinaadamu na kuwekeana heshima za mila na tamaduni za pale ulipo. Hapana haja ya kudhalilishana wala kudogoana. Lakini tatizo ni mifumo ya kisiasa ya CCM na serikali zake, au labda niseme kuwa wanasiasa wengi wa Tanganyika hawana nia njema na Zanzibar.
Ismail Jussa
21/08/2022
Makunduchi Unguja