JACADUOGO2.
JF-Expert Member
- Dec 13, 2010
- 930
- 217
Naamini mnakumbuka kuwa uchaguzi 2010 jimbo la Nzega H. Kigwangala alishindwa kwenye kura ya maoni lkn alipitishwa tu kwa mizengwe. Baada ya kushinda uchaguzi mkuu akaanza kazi kwa mbwembwe tukahisi kuwa tumewapata angalau wabunge vijana wawili (January na Hamisi) kutoka chama hicho dhalima ambao wangekuwa watetezi wa wanyonge na vijana kumbe hamna kitu!
Juzi tumemuona Kigwangala akiwatetea madaktari kipindi cha mgomo na hata alidiriki kujaribu kupinga ongezeko la posho ya wabunge kumbe danganya toto.
Eti leo bila aibu Hamisi anawashauri CHADEMA wasimsimamishe mgombea Arumeru Mashariki eti ni uharibifu wa fedha! Kama kweli ana uchungu na fedha za watanzania mbona hajawashauri mafisadi wakubwa wa CCM wa EPA, Richmond, Kagoda, IPTL nk?
Leo nimeamini kuwa huyu Kigwangallah ni mnafiki namba moja na hafai na ndani ya CCM hamna kiongozi hata mmoja anayeweza kusimamia maslahi ya Taifa hili, ila 2015 siyo mbali!