Uzalendo Umemshinda Dr. Hamisi Kigwangallah!

Naamini mnakumbuka kuwa uchaguzi 2010 jimbo la Nzega H. Kigwangala alishindwa kwenye kura ya maoni lkn alipitishwa tu kwa mizengwe. Baada ya kushinda uchaguzi mkuu akaanza kazi kwa mbwembwe tukahisi kuwa tumewapata angalau wabunge vijana wawili (January na Hamisi) kutoka chama hicho dhalima ambao wangekuwa watetezi wa wanyonge na vijana kumbe hamna kitu!
Juzi tumemuona Kigwangala akiwatetea madaktari kipindi cha mgomo na hata alidiriki kujaribu kupinga ongezeko la posho ya wabunge kumbe danganya toto.
Eti leo bila aibu Hamisi anawashauri CHADEMA wasimsimamishe mgombea Arumeru Mashariki eti ni uharibifu wa fedha! Kama kweli ana uchungu na fedha za watanzania mbona hajawashauri mafisadi wakubwa wa CCM wa EPA, Richmond, Kagoda, IPTL nk?
Leo nimeamini kuwa huyu Kigwangallah ni mnafiki namba moja na hafai na ndani ya CCM hamna kiongozi hata mmoja anayeweza kusimamia maslahi ya Taifa hili, ila 2015 siyo mbali!
Mimi kwa mtazamo wangu, H.E Kigwangallah as an individual can not do anything. Ningependa vijana, wazee, akina mama, wasomi na watu wengine wa fani mbalimbali wajitokeza kum back up ili aweze kuleta mabadiliko tunayoyataka. Mfano mimi naweza kuwa na wazo la kufanya Nzega iwe port of eit ya madini Tanzania kwa kuto vigezo ambavyo vitafanya iwezekane, lakini hakuna mtu ananiback up,, kwa Tanzania hiyo itakuwa ndiyo imeishia hapo.(ukifanya Nzega iwe port of exit ya madini na ikajengwa government godown za madini, ofisi za TRA, uwanja wa ndege ,Banks zioperate area hiyo, kampuni za insurance, ofisi za madini, na soko la madini kwa wachimbaji wadogo wadogo, tazama utapata ajira ngapi?, madini , TRA, hata agents wa ndege watajipatia pesa kiasigani?,taifa litajikusanyia kodi bila jasho sana. Ndugu zangu wana JF, nadhani Hamisi is the MP now, hebu tujaribu kumpa changamoto ambazo ataweza kuziwasilisha huko bungeni kutetea wananchi na kwa njia hii itakuwa kwa maslahi ya Watanzania.
 
Wewe willy J. Malecela nafikiri hata nafsi yako inakusuta unapoandika hizi habari kwani unajua wazi kuwa Kigwangallah alikuwa anapiga kelele za chura juu ya posho na mgomo wa madaktari. Sasa ameishia wapi? Mbona amefyata mkia baada ya kutishiwa nyau na mafisadi wa CCM? Kamwe ndani ya CCM hamna ukombozi amini usiamini ukweli ndo huo.

- Hapana siwezi kusutwa na ukweli niliouona na kuusikia mwenyewe, I respect Dr. Hamis kwa msimamo wake wa kusimamia anachokiamini, Mbunge mmoja hawezi kubadili anything kama hata wabunge wengine wa Upinzani wanataka posho, Dr. Hamis stood for what he believed na in the end imemucha very unpopular na wabunge wenziwe tena wa pande zote mbili, I was there with him Nje ya bunge wakati wabunge wakimshambulia and he never blinked!

- Ingawa pia una haki za kumhukumu kutokana na facts ulizonanzo ndio Demokrasia!, mimi ninamtetea baada ya kumuona na kuongea naye na kuona siasa zinazomzunguka baada ya kuonyehsa msimamo wake!
- Unless ana mapungufu mengine ambayo hayajasemwa hapa so far, lakini binafsi ninaamini Taifa letu tunahitaji Viongozi vijana na wenye msimamo kama yeye, SALUTE BRO HAMIS!

MUCH RESPECT!


William.
 
- Dr. Hamis a great human being na kiongozi pia, nimekutana naye bungeni nimeongea naye sana one on one, na pia majuzi tulikuwa wote mpirani Yanga na Zamaleck I mean a Solid Leader kwa macho yangu na masikio nimeona mbunge mmoja wa Upinzani akimshambulia kwa ajili ya kukataa kwake posho na yeye akimcheka bila ya wasi wasi kabisaa!

- Dr. Hamis much respect mkuu, sawa huenda ana mapungufu yake kama sisi wote wanadamu lakini baaada ya kuongea naye na kumsikiliza kwa makini msimamo wake on Mgomo wa madaktari na posho, ninasema Tanzania tunahitaji sana viongozi kama yeye, SALUTE BRO!


William.
Pole sana William kwa kukutana kwa muda mfupi na Kigwangala na kisha kudanganyika mara moja. Sisi tuliyekuwa naye karibu kwa muda mrefu ndiye tunaomjua kwa undani Kigwangala. Ni kijana mnafiki, mwongo ambaye siku zote ni vigumu kujua kilichopo moyoni mwake. Huongea kwa kufuata upepo. Ni aheri hao magamba wengine ambao wanajitambulisha moja kwa moja, na wanajulikana hivyo kuliko mbabaishaji Kigwangala. Jitahidi kuwa naye karibu, haitachukua muda utakapojua kuwa Kigwangala si mtu anayestahili kuwa kiongozi kwa ngazi yeyote ile. He is a great opportunist.
 
Mkuu, mbona mimi sijawahi kuwa na rafiki mwenye wajihi kama wako? Maana huwa nachagua kweli marafiki wa kuruka nao...
Pole sana William kwa kukutana kwa muda mfupi na Kigwangala na kisha kudanganyika mara moja. Sisi tuliyekuwa naye karibu kwa muda mrefu ndiye tunaomjua kwa undani Kigwangala. Ni kijana mnafiki, mwongo ambaye siku zote ni vigumu kujua kilichopo moyoni mwake. Huongea kwa kufuata upepo. Ni aheri hao magamba wengine ambao wanajitambulisha moja kwa moja, na wanajulikana hivyo kuliko mbabaishaji Kigwangala. Jitahidi kuwa naye karibu, haitachukua muda utakapojua kuwa Kigwangala si mtu anayestahili kuwa kiongozi kwa ngazi yeyote ile. He is a great opportunist.
 
Back
Top Bottom