Uyatima unanitesa kichwa kinauma kila siku

Sep 14, 2015
18
3
Jamani habarini za saizi,

Mimi naitwa Revocatus ni kijana mwenye umri wa miaka 25 bahati mbaya toka kuzaliwa nilikua nikiishi na mama nilie mjua kua ndie mama yangu mzazi kumbe sivyo jamani ninaumia sana baada ya kuujua ukweli baada ya mwezi mda mfupi ulio pita baada ya mama yangu mlezi kufariki ndipo nilipojua ukweli ilikua hivi maisha yangu yote nilijua ninae mjua ndio mama angu kumbe ndio mlezi wangu.

Baada ya mimi kuzaliwa mama angu aliaga dunia baada ya kuvuja damu sana alie nichukua alikua ni majirani zake mama angu kabla akiwa hai sasa ukweli umewekwa wazi pale tu nilipo omba kulipiwa kalo ya masomo ninayosomea kozi ya nursing certificate mara yakwanza kuingia chuoni nililipa mimi nilitafta kibarua nikafanya zaidi ya miezi 9 nikawa nimepata kama milion 1 na laki mbili ikabidi nitume maombi NACTE nikawa nimechaguliwa masomo nimeanza mwezi wa 11 nikawa nimejilipia sh laki 9 zingine nikawa nimenunua mahitaji sasa tumefunga chuo.

Sasa tukifungua inatakiwa kila mtu amalize malipo ya nusu semista sasa nikawa nimewaomba wale watoto wa yule mama ambae amenilea niliekua nikimjua kama mama angu mzazi kidogo tukawa tumepishana kimaongezi ikabidi aniambie kwa ukali sana kwamba (kwanza hata wewe sio damu moja na sisi wewe mama ako alifariki alipo kuzaa tu sasa hupaswi kutulazimisha kukusomesha we tuna kusaidia tu mpaka hapo) jamani nikajikuta dunia naiona kama mzigo ambao sasa umenielemea yaani najihisi kama vile mimi sio binadamu kama wengine kwanza mama angu sikumuona wala baba sikumuona yaan nimepata wakati mgumu sanai mpaka sasa nimeshindwa hata nianzie wapi?

Ni malizeje kwanza ada ambayo natakiwa kulipa ili niendelee na masomo pili wazazi siwajui mpaka nimejuta kuujua ukweli nibora nisingeli ujua kabisa hivo basi nawaombeni mnishauri jaman hata mawazo tu kwamba nianzie wapi japo niendelee na shule ? Na masomo na chuo tunafungua tarehe 3 mwez wa kwanza nimefanya ivi sihitaji hawa ndugu zangu wajue kua limenikera hili ndio maana nawaomben ushauri wenu jaman inauma mpaka kuvumilia moyo umeshindwa.
 
Pole sana mdogo wangu
Nakushauri umfate mama mlezi akushauri kwani inaelekea anakujali na anakupenda na ukiangalia jinsi alivyo kulea bila kuona tofauti yoyote tangia uko mdogo, very sad story
 
Miaka 25 hupaswi kuujita yatima wewe ni mtu mzima simama kama mwanaume tetea maisha yako.
 
Pole sana mdogo wangu
Nakushauri umfate mama mlezi akushauri kwani inaelekea anakujali na anakupenda na ukiangalia jinsi alivyo kulea bila kuona tofauti yoyote tangia uko mdogo, very sad story

Amesema kafariki unasomaje ww
 
Dogo dunia hii si rafiki kwa mwanadamu. Matatizo ni maisha. Piga moyo konde komaa kibingwa tafuta hela. Hela itakutafutia ndugu. Kama huna hela dunia hii hutakuwa na ndugu, hata penzi hutapata na ukipata ni lile la daraja la tatu.
USHAURI: Katisha/sitisha masomo yako rudi kwenye kibarua chako cha awali kilichokuwezesha kuvuna shs 1.2 million kwa miezi 9. Kapige kazi kwa malengo ya kurudi shule na kujilipia mwenyewe. Ukiwa kazini usioe ama kuolewa wala usiendekeze mapenzi.
 
Hao ndugu zako ni washenzi. Hawawezi kukwambia hivyo wakati huyo mlezi wako ndiye alikuwa mama yako hata kama hakukuzaa. Walitakiwa kukusaidia tu. Unasali wapi?

Nenda kamwambie mchungaji wako kanisa litakusaidia kwa kuweka sadaka ya kukutegemeza ili upate ada. Haya mambo tunayachangia sana makanisani. Usijione mpweke wala usimnung'unikie Mungu. Yeye anajua kwanini aliruhusu hili jambo litokee.

Cha msingi we piga shule tu itakusaidia sana.
 
25 yrs old orphan?!
Unajua una umri wa kuoa wewe na kutunza mtoto wa mwanaume mwenzio pamoja na watoto wako?

Dah!
 
"UGUMU WA MAISHA NI KIPIMO CHA AKILI" warudie hao watoto wa mama mlezi wapigie magoti, uwaombe muandikiane mkataba ukimaliza utalipa garama zao na riba pindi upatapo ajira, PILI ondoa dhana ya UYATIMA kichwani maana kuna watoto wa miaka 9 ndo mkubwa na wadogo zake 3, hawajui wafanye nini ni YATIMA wewe ni mtu mzima MPAKA HAPO ULIPOFIKA WAMEKUSAIDIA SANA SANA MPAKA KUPATA ELIMU YA KIDATO CHA NNE, WASHUKURU SANA "WARUDIE HAO WATOTO WA MLEZI WAKO WAPIGIE MAGOTI WAKUSOMESHE"
 
Dah pole mdogo wangu najua unauchungu kiasi gani na hao wanaokwambia umeshakuwa eti si yatima nadhani hawajapitia hii kitu. . . . ila niamini ninaelewa ni jinsi gani unaumia moyoni na ushauri wangu ni kubadili mawazo yako sasa na ujione we ni wa pekee ktk dunia hii na ujifunze kusimama peke yako kwani this world is not fair at all. . . . mwisho kabisa ntaku PM kwa msaada zaidi.
 
Amka wewe,Miaka 25 Una Mlalamikia nani?
Je sisi Ambao Hatukupata hata huyo Mama Mlezi?
Acha ujinga,wewe ni Mtu Mzima sasa.
kazi zipo nyingi Mjini.
 
jamani mmenishauri lakin kwa jinsi moyo wangu nilivo lipokea hili swala nashindwa hata kuonge japo nijielezee hali yangu coz najikuta nalia tu paspo kuongea kitu kama leo nimeenda kumueleza kiongozi mmoja wa halimashauri nimeshindwa kuongea yaan jaman achen shida hizi bas tu nibora ningeli fariki mimi ila alie nizaa abaki maake naona ninalo giza kubwa sana mpaka nakosa hamu ya kula nikulala tu jaman mungu kama kweli yupo naomba anipumzishe tu hata kwa ajali yoyote daahh
 
transporter nashukuru kwa ushauri ila kwa jinsi nijisikiavyo mpaka sasa natamani tu nipate hata ajari ya gafla ili nife niondokane na hii hali hata niwapo darasan nikikumbuka hali yangu najikuta naanza kufikilia sana jaman mungu huyu mniombeeni anipunguzie adhabu sasa hii naona imenizidi jamani
 
ndugu zangu kile kibarua ambacho nikua nafanya kilikua ni cha tobacco ilikua ni kazi ya msimu sasa ilivo isha ile pesa nilio kua nimeipata ikabidi nijipeleke shule kumbe ni bora ningeliacha tu nikafanya hata biashara yasingelinikuta haya
 
transporter nashukuru kwa ushauri ila kwa jinsi nijisikiavyo mpaka sasa natamani tu nipate hata ajari ya gafla ili nife niondokane na hii hali hata niwapo darasan nikikumbuka hali yangu najikuta naanza kufikilia sana jaman mungu huyu mniombeeni anipunguzie adhabu sasa hii naona imenizidi jamani

Dogo pole sana kwa kuujua ukweli.upokee huo ukweli japo mchungu lakini utakuweka huru na kukuimarisha.usimkufuru Mungu kwa hiyo hali kwakuwa Mungu ni Baba wa yatima.upo duniani kwa mpango wake.Pia anakuwazia mawazo mema na ya amani.kinachokuumiza ni ukosefu wa maarifa namna ya kuishi ni hii hali.jambo la kufanya washirikishe viongozi wako wa kiroho upate ushauri nasaha.majirani na viongozi wa kiroho watakupa msaada na uwezo wa kuyakabili unayoyapitia.kumbuka hakuna jambo gumu la kumzidi Bwana aliye hai.Barikiwa.
 
shukuru hata hawapi wamekuepushia zambi kuliko wapo na hawakujali wala kulipa hizo karo unaishia kuwatukana tu upate laana bureeee.

miaka 25?? umeoa? fanya chaap mda ndo huu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom