UWT: Lini Mtakuwa Taasisi [Institution] Mliokoe Taifa na Vizazi Vyake?

DSN

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
2,837
1,674
Watanzania wamekuwa wakifuatilia sana mwenendo mzima wa kisiasa na uchumi wa Taifa lao lakini wakiwa hawana majibu ya maswali mengi ambayo yamelikumba Taifa. Matatizo mengi sana yamelisibu Taifa lakini watawala wamekuwa wanamajibu kiduchu kujibu kiu kubwa ya Watanzania.

Lakini kadri siku zinavyosonga ukosefu wa majibu ya kukidhi kiu ya Wananchi, juu ya mambo mengi yanayolisibu Taifa ikiwemo WIZI WA MALI YA UMMA,UKOSEFU WA MAADILI YA VIONGOZI NA UMMA,HUJUMA DHIDI YA TAIFA NA MENGINEYO MENGI YANAYOHUSU USALAMA WA SISI KAMA TAIFA NA UMMA.

Lawama nyingi sasa hivi zinapelekwa kwa Wanausalama wa Taifa.Kwa Mtanzania wa kawaida wanaufahamu japo kidogo kujua kazi za Usalama wa Taifa. Ingawa hakuna mahari popote katika Taifa ambako Wananchi wanapata fursa ya kujifunza japo kidogo juu ya shughuri zinazofanya na IDALA hiyo mihimu kwa Taifa.

Lakini kwa mujibu wa mfumo wa idala [Department] hiyo ya UWT imekuwa ngumu kwa Idala hiyo kuonyesha matumaini na uwezo wake kwa umma na sasa kuwa ni sehemu ya baadhi ya Watanzania kuona kuwa HAITIMIZI WAJIBU WAKE kama msimamizi MKUU wa ULINZI NA AMANI YA TAIFA NA RASILIMALI ZOTE ZA TAIFA HILI.

Uongozi wa IDALA hiyo nyeti ufike sehemu utafakari na kuamua kwa DHATI kuwa ZAMA NA NYAKATI unaisukuma IDALA HIYO [DEPARTMENT] ya hiyo UMMA hiyo kubadilika kuwa TAASISI [INSTITUTIONS] KAMILI YENYE MAMLAKA NA UWAJIBIKAJI KWA UMMA.

Kwa kuwa kuna mengi yanayokuja na kutufanya kuwa TAIFA ndani ya MATAIFA [EAST AFRICA COMMUNITY] pasipo UWT iliyotimilifu kama TAASISI HURU [INDEPENDENT INSTITUTION] yenye mamlaka tosherezii kukabiliana na changamoto [Challenge] ambazo kwa uwezo wake wa ndani kwa sasa zimeonyesha kuwa Wananchi wana hofu na wasiwasi kwa yale yote yanayoendelea kuwa yameshindikana kudhibitika japokuwa kuna uwepo wa idala hiyo.

Kiutendaji Wananchi tulio Nje hatuna majibu lakini,tunatathimini kupitia mwenendo mzima ya haya yanayojili kwenye TAIFA katika hali halisi kama matatizo ya hujuma za kiuchumi wa Taifa,wizi wa fedha za umma,ukosefu wa maadili ya viongozi na Taifa na mengineyo mingi.

UWT kama walinzi wa TAIFA waje na jawabu la kuondoa sintofamu nyingi ambazo Taifa inazo,lakini majibu hayo yaje yakiwa na tiba ya kudumu na sio zima moto.Tiba hiyo ya kudumu ni kuifanya idala hiyo ya ulinzi kuwa taasisi yenye uwezo na mamlaka itakayojibika BUNGENI.

Kwa kuanzishwa kwa UWT kuwa TAASIASI itakuwa na UWEZO WA KIMAMLAKA [MANDATE] na hivyo kutoa na kupokea sera zenye uwezo usio na vikwazo vya kuwajibika chini ya ofisi fulani na badala yake iwajibike kwa UMMA [BUNGE].

Ndani ya TAASISI hiyo ndio mwanzo wa kuwa na idala kadha wa kadha kama vile:
-Idala ya Ulinzi
-Idala ya Mambo ya Kimataifa na Utandawazi [Uchunguzi]
-Idala ya Utumishi na Mahusiano [Utawala]
-Idala ya Uchumi na Fedha [Uchunguzi]
-Idala ya Technolojia na Sayansi [Uchunguzi]
-Idala ya Siasa, Ustawi wa Jamii na Utamaduni wa Taifa [Uchunguzi]
-Idala ya Afrika Mashariki na Mipaka [Uchunguzi]
-Idala ya Ualifu na Ujasusi [uchuguzi]
-Idala ya Maadili na Uzalendo [Uchunguzi]
-Idala ya Elimu na Ajira [uchunguzi]
-Idala ya Muungano [Uchunguzi]
-Idala ya Afya [Uchunguzi] nk

Kwa kuanzia hapo kila idala ikawajibika ipasavyo kwa kitengo [organ] kutengeneza kitu kizima ambacho ndio Taasisi.

Kwangu mimi huu ni Mtizamo tu

Nawasilisha
 
Wawe wanareport wapi,kwa wakati gani,dg awe appointed na nani,mamlaka yao kiutendaji yaweje,wawe wazi kiasi gani kiutendaji katika uchunguzi wao?
 
Sijui unamaanisha nini kwa kusema UWT iwe taasisi, kama unaweza wa act kama tasisi ya kweli au wawe formally institutionalized.

If you are talking about the former you may have a point, for the latter, Mkapa already institutionlized them formally.
 
Wawe wanareport wapi,kwa wakati gani,dg awe appointed na nani,mamlaka yao kiutendaji yaweje,wawe wazi kiasi gani kiutendaji katika uchunguzi wao?


Waweza kuwa chini ya Kamati maalum itakayochaguliwa na Bunge kutoka vyama vyote [National Security of United Republic of Tanznaia Commiteee].Wanawajibika kwa Bunge la jamhuri ya Muungano,Na Kwa kuwa utendaji wao wa kila siku unakuwa ni sehimu ya utendaji unaohihusu Serikali, Mkurugenzi wake [Director General] atateuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa kupitishwa na kupigiwa kura Bunge la Jamhuri ya Muungano.Rais anaweza kupeleka majina Matatu ya Wateule kisha wabunge wanapitisha jina moja katika majina matatu wabunge wakisema hapana inabidi aluidi kuteua upya mpaka watakapokubali,na hata kama wabunge wakisema kuwa hawana imani nae kwenye utendaji wake wanapiga kula ya kutokuwa na imani nae [A vote of no confidence is a vote in which members of a group are asked to indicate that they do not support the person or group in power, usually the government.]

Wanakuwa na Mamlaka wao kama wao,ili kuondoa kuwa inamtegemea nani kama msimamizi zaidi ni kuwa mambo yote ya msingi yanayoitaji ufafanuzi kwa wabunge watawajibika wao.Hata pale kiongozi yoyote atakaeingia madarakani wao wanabaki kikatiba kuwa wao nao ni taasisi inayojitegemea ndio maana ya kuwa Independent.

Mfano kama sasa hivi matatizo ya Umeme,Dowans,Mafuta na hujumu zozote za kitaifa wanaitwa Bungeni watoe taarifa yoyote kama kuna vitendo vya hujuma vimefanyika kulihujumu Taifa na wao wamechukua hatua gani.Majibu yao yanachukuliwa Independetly nje na yale majibu ya Serikali kitu ambacho itaibua utendaji ambao itabidi wawe na jukumu la dhati na si kuwa ni sehemu lasmi ya serikali kwa asilimia mia.

Kwa kuwa majibu kama leo ya kukosekana kwa mafuta,wao kama wao wanajua nini kinaendelea na ushauri wao ni muhimu sana kwa kuwa itakuwa ni taasisi yenye kila idala yenye wataaramu kama taasisi nyingine kama ilivyo TRA,EWURA,au Mamlaka yoyote ile iliyoanzishwa kwa mujibu wa sheria ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa ufasaha kajielimishe kuhusu au maana ya TAASISI [INSTITUTION].Mnake ungekuwa unajua maana yake usingeuliza Wawe wanareport wapi, kwa wakati gani, dg awe appointed na nani, mamlaka yao kiutendaji yaweje, wawe wazi kiasi gani kiutendaji katika uchunguzi wao?Ila nimeona tujuzane japo kidogo kutoa idea ya mtizamo wangu.
 
Sijui unamaanisha nini kwa kusema UWT iwe taasisi, kama unaweza wa act kama tasisi ya kweli au wawe formally institutionalized.

If you are talking about the former you may have a point, for the latter, Mkapa already institutionlized them formally.

No Waakati kama taasisi inayojitegemea [Independetly] hii kuwa institutionalized, iwe hivyo kwa vitendo na majukumu yao kama kuna majibu ya kujibiwa pale ambapo Taifa linatka kujua kupita vyombo vyake kama Bunge basi wawajibike wao kama wao na sio kuwa wako kwa niaba ya fulani.Lengo ni kuwa wawe huru kama TRA,EWURA,wenye mamlaka yao na sheria zao.Ukikwepa kodi kuna sheria zitasema na wewe.

Nao wao wafikie huko kwa kuwa taasisi yenye kujitegemea.Namaanisha kama ni walinzi basi wawe ni walinzi wenye kupambana na adui hata kama ni kungata adui ruksa mwenye nyumba ampe ruksa. Sio sawa mimlki wa nyumba kumiliki mbwa mzuri mwenye sifa zote za kujihami dhidi ya adui anashinda na mnyororo masaa 24.Ila kitisho kinabaki kuwa ni mlio wa sauti ya mbwa aliye ndani ya ukuta.Mwenye nyumba akiingiliwa usiku wa manane huku mbwa anabonge ya cheni amlaumu nani mbwa au?
 
Back
Top Bottom