Mimi nadhani mambo ya dini huwafanya watu wajisikie wakosefu muda wote na ni dhaifu. Lakini pia dini kubwa duniani (ukiondoa Ubudha) zimejengwa katika misingi ya Uhasama wa Mashariki ya Kati. Wakristo wanaamin Ibrahim alimzaa Isaka ambaye ni chimbuko la wana Israel ambao ndiyo msingi wa ukombozi wa wanadamu kupitia Yesu Kristo ambaye ni uzao wa Daudi.
Lakini Waislamu wanaamini Ibrahim alimzaa Ishmael ambaye ndiye chanzo cha sehemu kubwa ya Waarabu ambao nao wao pia wanamuona Ibrahim kama baba wa Imani kama wakristo wanavyoamini. Wakati ugomvi wa waarabu na Israel ni wa Kihistoria na wala hauhusiani na dini hizi za Kiislam na Kikristo, waumini wa dini hizi mbili wanadhani ugomvi huo ni sehemu ya dini zao. Kumbuka Wafilisti ndiyo Wapalestina!!
Leo hii muislamu wa Tanzania anaamini kwamba anapoitetea Palestina (ingawa kuna wapalestina wakristo) dhidi ya Israel (ingawa Waisrael wengi 90% hawaamini katika Ukristo) anakuwa anautetea Uislam, na Mkristo naye anasisimka anapoitetea Israel kwa kuamini kuwa ni taifa teule la mungu.
Kwa hiyo Kwenye Jukwaa la dini huwa mitusi inaporomoka hovyo hovyo kwa sababu dini hizi mbili zimejengwa juu ya msingi wa kiuhasama na wao waliozisanifu (Siyo Mtume S.A.W au Yesu Kristo) nje ya msingi uliowekwa na waasisi wa dini hizi ambao ni upendo, amani, mshikamano, nia njema. Ndiyo maana salaam ya "Asalam aleykhum" ina mantiki katika kujenga hoja ya Uislam lakini ni waislam wangapi wanaoamini kwamba hata wasio waislam nao wanatakiwa kuishi kwa Amani? Kama yesu alikuja kuwakomboa wanadamu ni ukombozi gani unaotenga sehemu ya wanadamu hao mbali?