Uwezo wa wataalamu wetu kutoka vyuoni.

Mathias Byabato

JF-Expert Member
Nov 24, 2010
1,025
705
Wakubwa ebu tujadili uwezo kitaaluma wa wajuzi wetu wanaoanza kazi wakitokea vyuoni ni kwa nini unakuwa ni mdogo sana.

Tatizo liko wapi,mitaala,mapokeo ya kidunia(kusoma kwa lengo la kutafuta ajira) au nini.

Nimejionea wataalamu kadhaa wanaotoka vyuoni wakiwa hawajui lolote hasa kwenye fani yao, wengine wakiomba attachment kwa wazoefu(ingawa si vibaya) lakini A B C hawajui.

Tufanye nini ili vyuo vyetu vizalishe wataalamu badala ya kuzalisha watumishi tu.

Jumapili njema

Byabato
 
Tatizo kubwa ni Wizi wa Mtihani ulliyo Kithiri Mwanafunzi anaiba Mitihani kuanzia Mtihani wa Taifa darasa la nne, la saba form two,form four,form six chuo kikuu wewe unategemea nini hapo. akiajiriwa mahari huyo ndugu ni hatari hasa kwa fani ya Udakitari,na atakuwa Mwizi hata kwenye fedha za umma kwasababu yeye anajua kila kitu kinakuja kwa kuiba tu ni hatari kwa nchi yetu na ndiyo wazoefu wa kutaka rushwa ili atoe huduma.sijui tunaenda wapi
 
Wakubwa ebu tujadili uwezo kitaaluma wa wajuzi wetu wanaoanza kazi wakitokea vyuoni ni kwa nini unakuwa ni mdogo sana.

Tatizo liko wapi,mitaala,mapokeo ya kidunia(kusoma kwa lengo la kutafuta ajira) au nini.

Nimejionea wataalamu kadhaa wanaotoka vyuoni wakiwa hawajui lolote hasa kwenye fani yao, wengine wakiomba attachment kwa wazoefu(ingawa si vibaya) lakini A B C hawajui.

Tufanye nini ili vyuo vyetu vizalishe wataalamu badala ya kuzalisha watumishi tu.

Jumapili njema

Byabato

Mkuu naona una-generalise sana kuna watu vipanga tu wengi na kuna wezi kama JK wengi tu. Wenye uwezo mkubwa wapo lakini hawapewi nafasi tuache hii kulialia kila siku ati wataalam na wasomi wetu hawana uwezo. Hao mnaowaita ma-expatriate wana uwezo? Mbona mnaleta vichaka ambao wanajifunza kazi tu?
 
Back
Top Bottom