Uwezo wa maji ya baraka kupambana na nguvu za giza

Nimekuwa nikisikia mara nyingi kuwa ikiwa ndani kwako unasumbuliwa na nguvu za giza suluhisho ni kuweka Maji ya Baraka! Binafsi nimeweka chupa ya lita moja lakini bado tunaandamwa na tatizo hilo, ndoto Za watu waliokufa, kufukuzwa na majoka, kupigwa risasi, na kuweweseka kila siku kati ya saa nne na nusu na saa tano na nusu usiku! Nakosea wapi maana nina imani sana na uwezo wa haya maji, lakini bado sijawakomesha hawa wasiojulikana! Naombeni mawazo yenu wana jamvi!
Maji hayana chochote Bro.Labda kwa sababu siku hizi kuna joto sana hasa hapa Dar hayo yanaweza kukusaidia kwa kukatia kiu.Damu ya YESU ndiyo kiboko ya matatizo yote ,hasa hayo mauza uza.
 
Mkuu nenda kapime malaria.Mimi nikianza kuota ndiyo za kutisha huwa napima malaria. Always nakutwa ninayo.

Malaria hapana! Hii hali ni zaidi ya Miamala miwili sasa, na hutokea saa nne na nusu hadi saa tano! Nikilala baada ya muda huo hali huwa shwari
 
Nimekuwa nikisikia mara nyingi kuwa ikiwa ndani kwako unasumbuliwa na nguvu za giza suluhisho ni kuweka Maji ya Baraka! Binafsi nimeweka chupa ya lita moja lakini bado tunaandamwa na tatizo hilo, ndoto Za watu waliokufa, kufukuzwa na majoka, kupigwa risasi, na kuweweseka kila siku kati ya saa nne na nusu na saa tano na nusu usiku! Nakosea wapi maana nina imani sana na uwezo wa haya maji, lakini bado sijawakomesha hawa wasiojulikana! Naombeni mawazo yenu wana jamvi!
Pole sana kwa matatizo
Hizo ndoto zitazama kwa upande Mwingine
Inawezekana Mungu anasema na wewe kuna ujumbe unapewa kuhus ww au family au ukoo.
Hao watu waliokufa inawezekana wanakuvuta na wewe kwenye kifo, kupelekwa kuzimu.
Chunguza vizuri hao watu waliokufu inawezekana vifo vyao siyo kwa mapenzi ya Mungu. Kuna soma 1 refu kuhus kuota watu waliokufa kwa kifupi kuna aina 4 za kifo. Kifo 1 kwa mapenzi Mungu hatuwezi kuwaota hawa watu. Aina 3 za vifo hawa watu ndio tunaowaota kwa sababu Nafsi au roho zao zipo zipo katika ulimwengu wetu wanasubiria siku za Mungu alizowapangia kuisha Nafsi au roho zao ndipo zitaondoka kwenye ulimwengu wetu huu.

Fanya sala ya Toba omba msamaha wa Dhambi, mpokee Yesu awe Bwana na mwokozi wako wa maisha.
Nguvu za Giza utashinda
Imeandikwa “Lolote nitakalo lifunga Dunia litafungwa Mbinguni, lolote nitakalo lifungua Dunia litafunguliwa Mbinguni “
“Ninayaweza mambo yote kwa yeye anatiaye nguvu”
“Kila silaha yeyote itakayofanyika juu yangu haitafanikiwa “
Tutatumia Damu ya mwana Kondoo kumshinda shetan na majeshi yake
Huwe na Amani tulia Bwana anaponya

Funga mapepo na nguvu za Giza zitupie kuzimu kwenye shimo

Kuna watu wanaota wanaendesha Tax au gari wanakuwa na furaha sana wanaamini siku 1 wataendasha Tax au Gari. Kumbe Bwana anawapa ujumbe kuwa wao ni madereva wa Safari za kichawi.
Kuota ndoto kufukuzwa na Mbwa ina maana yake,wapo wengine wanaota ndoto wanaoga mtoni ina maana yake
 
Nimekuwa nikisikia mara nyingi kuwa ikiwa ndani kwako unasumbuliwa na nguvu za giza suluhisho ni kuweka Maji ya Baraka! Binafsi nimeweka chupa ya lita moja lakini bado tunaandamwa na tatizo hilo, ndoto Za watu waliokufa, kufukuzwa na majoka, kupigwa risasi, na kuweweseka kila siku kati ya saa nne na nusu na saa tano na nusu usiku! Nakosea wapi maana nina imani sana na uwezo wa haya maji, lakini bado sijawakomesha hawa wasiojulikana! Naombeni mawazo yenu wana jamvi!
Yaani unalalaga saa nne?, Mbona mapema sana?, No wonder unapata ndoto za ajabu ajabu,
Hayo maji ni imani tu, hayana nguvu yoyote,
Pili nguvu za giza nazo ni imani tu,, usikute una tatizo la hallucinations,,,,
 
Ni. Mkatoliki halafu hujui kutumia hayo maji? Hayo maji nyunyuzia kwa kutumia mkono kila siku nje na ndani ya nyumba na hata hapo kitandani huku ukisema maneno ya Mungu yanayohusiana na hiyo hali iondoke, wengi hayo maji yametusaidia sana
 
Malaria hapana! Hii hali ni zaidi ya Miamala miwili sasa, na hutokea saa nne na nusu hadi saa tano! Nikilala baada ya muda huo hali huwa shwari
Unakula sana vyakula vizito vizito muda mfupi kabla ya kwenda kulala.
 
Achana na ujinga uo utakufa bure eti maji ya baraka si mazindiko hayo
Ila akifanya mwengine ndo kosa achana na uo ujinga fanya mfuke na maji ya bangi kwa kwa kutamka mabalaa yako yote alafu ulete majibu
Hapa
 
Ni. Mkatoliki halafu hujui kutumia hayo maji? Hayo maji nyunyuzia kwa kutumia mkono kila siku nje na ndani ya nyumba na hata hapo kitandani huku ukisema maneno ya Mungu yanayohusiana na hiyo hali iondoke, wengi hayo maji yametusaidia sana
Apo ndo analoga zaidi huu ushaur mwingine mngekuw mnakaa kimy unachek uzi then una chill mtakujaga kuua pasipo kutarajia
 
Nimekuwa nikisikia mara nyingi kuwa ikiwa ndani kwako unasumbuliwa na nguvu za giza suluhisho ni kuweka Maji ya Baraka! Binafsi nimeweka chupa ya lita moja lakini bado tunaandamwa na tatizo hilo, ndoto Za watu waliokufa, kufukuzwa na majoka, kupigwa risasi, na kuweweseka kila siku kati ya saa nne na nusu na saa tano na nusu usiku! Nakosea wapi maana nina imani sana na uwezo wa haya maji, lakini bado sijawakomesha hawa wasiojulikana! Naombeni mawazo yenu wana jamvi!
Maji ya baraka yakikatoliki huwa yanabarikiwa lakini pia huchanganywa na chumvi.Ukiacha kubarikiwa tambua chumvi kiasili ni kinga ya uchawi.Chumvi na uchawi haviendani kabisa,

Kama unandugu yako ni mganga wakienyeji na anavibuyu(tunguri) ndani mvizie hayupo chukua chumvi mimina kwenye vibuyu vyake utakua umeviua.

Tuwaachie kina mshana na fani zao lakini ni ukweli usiopingika kwamba kuna vitu huwa havikai pamoja na uchawi,inasemekana hata kina mshana,tunguri za uchawi na tunguri za kutibia huwa haziwekwi pamoja,ukiziweka pamoja huwa moja itaharibu nyingine.

Nikihitimisha kwenye isue ya maji ya baraka,ili ile hali ya ubaraka utende muujiza ni lazima muhusika awe na imani ya kweli sio ya mdomoni tu wakati rohoni hana.
 
Malaria hapana! Hii hali ni zaidi ya Miamala miwili sasa, na hutokea saa nne na nusu hadi saa tano! Nikilala baada ya muda huo hali huwa shwari
Usile usiku ukiwa unalala. Hebu pata dinner saa moja usiku. Kisha utulie kwenye TV mpaka saa 3 ndipo ukalale
 
Nimekuwa nikisikia mara nyingi kuwa ikiwa ndani kwako unasumbuliwa na nguvu za giza suluhisho ni kuweka Maji ya Baraka! Binafsi nimeweka chupa ya lita moja lakini bado tunaandamwa na tatizo hilo, ndoto Za watu waliokufa, kufukuzwa na majoka, kupigwa risasi, na kuweweseka kila siku kati ya saa nne na nusu na saa tano na nusu usiku! Nakosea wapi maana nina imani sana na uwezo wa haya maji, lakini bado sijawakomesha hawa wasiojulikana! Naombeni mawazo yenu wana jamvi!
Yani huo muda unaolala wewe ndio bia huwa inanogs, halafu unakuta sebene la Papa Mobimba liko hewani, aisee unaanzaje kulala mida hiyo?

Jaribu kupiga K-Vant uondowe ujinga na hizo elusion.
 
Back
Top Bottom