Serikali, wazazi na mashirika ya kidini kwa ujumla chagueni mwanga au giza

Mhafidhina07

JF-Expert Member
Aug 1, 2014
2,553
2,992
Salaam,

Binafsi ni kawaida kwangu kuja na bandiko za kukemea tabia na mmonyoko wa maadili kwa jamii nyingi za kiafrika na hususani Tanzania.

Jamii nyingi za kiafrika zimepoteza asili yake ya kimalezi na heshima (Tamaduni) kutokana kuvamia dude kubwa ambalo lipo imported halikuwahi kuwepo mwanzo ila ni changamoto
za muingiliano zimetufikisha katika giza hili.

Nimetembea bàadhi ya mikoa ya Tanzania nimekutana na Tabia za ajabu zikifanywa na vijna hususani rika la 17-24 wakiwa kwenye kifungo kikubwa cha uvutaji bangi na mapenzi ya jinsia moja vitu ambavyo ni moja ya kiini kikuu cha kuharibu Tamaduni zetu.

Bado serikali imeendelea kupiga kelele za mayowe kwa kuwatupia mzigo wa lawama asasi za kiraia, dini na wazazi upande mwengine nao wanawatupia lawama serikali kama muhimili mkuu wa nchi.

Binafsi, naona bado wote wanaendelea kuwa kwenye makosa makubwa na deni, shutuma pamoja na lawama kizazi kinachokuja kwani wote wanahitaji mshikamano wa nguvu kulinda nguvu kazi ya Taifa katika misingi yote. Sasa nini kifanyike ili kuondokana na hii dhuruba?

SULUHISHO

Tukimbuke nguvu kazi ni msingi kwenye kusimama kwa Taifa na kijana ndiyo jembe la Taifa tunapokubali kuharibika tabia za vijana basi inaweza kutugharimu maelfu ya miaka kwenye meza ya maamuzi na uchumi wa Taifa.

Mshikamano

Wazazi, walezi, asasi za kiraia, serikali na taasisi za kidini tujue umuhimu wa kizazi kijacho na tusipende kuangalia leo yetu kwani hata hao viongozi wa nchi macho yao yapo kwenye leo yao (indivudual interest) ndiyo maana wapo tayari kwa namna yeyote ile ili kukubalika hata kwa kuharibu kizazi (no future visio).

Masikilizano

wazazi tunatakiwa kuwasikiliza watoto ila inahitaji umakini mkubwa kwenye kuamua na kuelewana pia kuijua zaidi utandawazi kwa lengo la kuwafundisha watoto wao.

Tujifunze kusema hapana (msimamo) ila kujulikana muelekeo wetu wa itikadi na akili ya maamuzi.

SHIME TUSHIAMANE.
 
Back
Top Bottom