Uwezo wa bundi kutambua kifo cha mtu

Uwezo wa bundi kutambua kifo cha mtu

bhuha

Member
Joined
Feb 10, 2017
Posts
39
Reaction score
31
BUNDI ni aina ya ndege ambaye hula nyama; hufanya mawindo yao wakati wa usiku na kupumzika wakati wa mchana.
Pamekuwepo na imani kwa wengi kwamba bundi anaponekana nyumbani kwa mtu ni lazima kuna mtu atakufa katika nyumba hiyo.
Hivyo imewapelekea watu wengi kuwa na hofu kubwa sana juu ya kiumbe hiki cha Mungu na hivyo kukihusianisha na nguvu za giza kwamba ni lazima ametumwa na mchawi ili kuchukua roho ya mtu. UKWELI UPO HIVI:

Bundi ana uwezo mkubwa sana wa kuvuta harufu ya mzoga kutoka mbali. Uwezo huu wa kunusa harufu unapita uwezo walionao binadamu.
Hivyo inapotokea katika nyumba fulani kuna mgonjwa mahututi ambaye seli za mwili wake zimeshaanza kufa lakini mapigo ya moyo bado yanafanya kazi; Bundi huweza kunusa harufu ya seli hizo, harufu ambayo binadamu hawawezi kuihisi, na hivyo huvutiwa kuisogelea kwa ajili ya kujipatia chakula, ila hataweza kuingia ndani kwa kuhofia binadamu. Kwa kawaida binadamu hafi mara moja, bali hufa hatua kwa hatua. Zinaanza kwanza kufa seli za mwili, baadaye ogani mbalimbali za mwili.
Ogani za mwisho kufa ni moyo ikifuatiwa na ubongo. Hivyo bundi anapoonekana kwenye nyumba yenye mgonjwa mahututi ni dalili kwamba mgonjwa huyo ameshaanza hatua za kufariki, na hivyo uwezekano wa mgonjwa huyo kufariki siku za karibuni ni mkubwa sana.
Inapotokea kwamba mgonjwa amekufa baada ya bundi kuonekana, tafsiri sahihi siyo kwamba kifo kimesababishwa na bundi bali ni kwamba dalili za kifo cha mgonjwa huyo zimetambuliwa na bundi.
Hivyo cha kufanya siyo kumtafuta mchawi bali ni kuzidi kumkabidhi mgonjwa huyo katika huruma ya Mungu kwa njia ya sala.

Hofu ya bundi kama kiumbe chenye nguvu za giza ipo zaidi Afrika. Ulaya hawana hofu hiyo. Wao humtazama bundi kama kiumbe cha Mungu, kiumbe cha ajabu, na hivyo huvutika kukaribia kwa njia ya utalii, utafiti na hata ufugaji.
Zipo mbuga za wanyama zinazofuga bundi. Sifa mojawapo ya bundi inayowavutia watalii wengi kumtazama ni ule uwezo wake wa kugeuza shingo kutoka mbele mpaka nyuma pasipo kuhitaji kugeuka kwa kiwiliwili chake.

Hivyo hatupaswi kuwaogopa, kuwachukia bundi ama kuongea vibaya juu yao. Hao ni viumbe vya Mungu kama walivyo njiwa, kondoo, v n.k. Wao ni kazi ya Mungu.
Hivyo kuongea vibaya juu ya bundi ni kuongea vibaya juu ya kazi ya Mungu na hiyo kumpa shetani nafasi ili hofu izidi kutawala miongoni mwa watu.
Kwa hiyo tunapowaona bundi tuna wajibu wa kumpa Mungu SIFA NA UTUKUFU Kwa Kuwa Uwezo Huu Umetoka Kwake.

Na
_*Dr. Amani L. Mang'alila*_
_Animals Behavior & Psychology_.
Dodoma - Tanzania
 
Naombeni Mpeni Credit Yake Padre Titus Amigu!..
Ndiye aliyetoa Haya Majibu!
 
huko kuzungusha shingo huko ndio hatar..hapana kwa kweli
 
Hizi imani zilikuwepo zamani kipindi wazee wapo ila tangu wamepotea kwa kufariki naona hii hali imeisha zamani nakumbuka bundi akililia shambani kwenu kesho hamna kwenda shule babu atakuja mbuzi inapigwa chini eti ya kuombea ukoo eti asife mtu..
 
Sijui hoja hii uneitoa katika chanzo gani maana ungetuwekea chanzo ingekuwa bora zaidi. Lakini kama chanzo ni wewe mwenyewe basi ntakuambia tu kuwa bundi hali mizoga. Kwa hiyo hawezi kuvutiwa na mizoga kamwe.
 
UWEZO WA _BUNDI_ KUTAMBUA KIFO CHA MTU

BUNDI ni aina ya ndege ambaye hula nyama; hufanya mawindo yao wakati wa usiku na kupumzika wakati wa mchana.
Pamekuwepo na imani kwa wengi kwamba bundi anaponekana nyumbani kwa mtu ni lazima kuna mtu atakufa katika nyumba hiyo.
Hivyo imewapelekea watu wengi kuwa na hofu kubwa sana juu ya kiumbe hiki cha Mungu na hivyo kukihusianisha na nguvu za giza kwamba ni lazima ametumwa na mchawi ili kuchukua roho ya mtu. UKWELI UPO HIVI:

Bundi ana uwezo mkubwa sana wa kuvuta harufu ya mzoga kutoka mbali. Uwezo huu wa kunusa harufu unapita uwezo walionao binadamu.
Hivyo inapotokea katika nyumba fulani kuna mgonjwa mahututi ambaye seli za mwili wake zimeshaanza kufa lakini mapigo ya moyo bado yanafanya kazi; Bundi huweza kunusa harufu ya seli hizo, harufu ambayo binadamu hawawezi kuihisi, na hivyo huvutiwa kuisogelea kwa ajili ya kujipatia chakula, ila hataweza kuingia ndani kwa kuhofia binadamu. Kwa kawaida binadamu hafi mara moja, bali hufa hatua kwa hatua. Zinaanza kwanza kufa seli za mwili, baadaye ogani mbalimbali za mwili.
Ogani za mwisho kufa ni moyo ikifuatiwa na ubongo. Hivyo bundi anapoonekana kwenye nyumba yenye mgonjwa mahututi ni dalili kwamba mgonjwa huyo ameshaanza hatua za kufariki, na hivyo uwezekano wa mgonjwa huyo kufariki siku za karibuni ni mkubwa sana.
Inapotokea kwamba mgonjwa amekufa baada ya bundi kuonekana, tafsiri sahihi siyo kwamba kifo kimesababishwa na bundi bali ni kwamba dalili za kifo cha mgonjwa huyo zimetambuliwa na bundi.
Hivyo cha kufanya siyo kumtafuta mchawi bali ni kuzidi kumkabidhi mgonjwa huyo katika huruma ya Mungu kwa njia ya sala.

Hofu ya bundi kama kiumbe chenye nguvu za giza ipo zaidi Afrika. Ulaya hawana hofu hiyo. Wao humtazama bundi kama kiumbe cha Mungu, kiumbe cha ajabu, na hivyo huvutika kukaribia kwa njia ya utalii, utafiti na hata ufugaji.
Zipo mbuga za wanyama zinazofuga bundi. Sifa mojawapo ya bundi inayowavutia watalii wengi kumtazama ni ule uwezo wake wa kugeuza shingo kutoka mbele mpaka nyuma pasipo kuhitaji kugeuka kwa kiwiliwili chake.

Hivyo hatupaswi kuwaogopa, kuwachukia bundi ama kuongea vibaya juu yao. Hao ni viumbe vya Mungu kama walivyo njiwa, kondoo, v n.k. Wao ni kazi ya Mungu.
Hivyo kuongea vibaya juu ya bundi ni kuongea vibaya juu ya kazi ya Mungu na hiyo kumpa shetani nafasi ili hofu izidi kutawala miongoni mwa watu.
Kwa hiyo tunapowaona bundi tuna wajibu wa kumpa Mungu SIFA NA UTUKUFU Kwa Kuwa Uwezo Huu wa bundi
Hanna kitu kama hicho! Mimi msiba unatokea kijijini bundi analia juu ya paa language siku mbili kabla! Kwa hio hiyo harufu inatoka kijijini mpaka kwangu ndio bundi anainusa?
 
Acha sayansi zako za kubuni sikubaliani nawe hata chembe
 
Una hoja kwa kiasi fulani, wa afrika imani za kishirikina zimetawala
 
Hakuna ukweli wowote wa uwezo usio wa kawaida wa bundi kupata harufu ya seli zlizoanza kufa za binadamu ndani ya nyumba, hivyo eti huisogelea! Bundi, kwa silika tu, husogelea nyumba yoyote ili kujipatia mawindo, hususani panya. Katika mawindo yake huweza kuifuata nyumba yoyote. Kifo kutokea ni coincidence tu. Kinachomponza ni kule kutoka kwake usiku na muundo wa uso wake ulio tofauti na ndege wengine. Macho yake yamekaa yote mbele kama ya nwanadamu. Hata Ulaya zamani enzi za ujima walimchukulia kama ndege mleta nuksi. Wakamwita ' a bird of bad omen.' Lakini baada ya 'enlightenment' ushirikina huo waliuacha. Bundi ni ndege wa kawaida tu kama walivyo wengine, ila tu yeye ni ' nocturnal'
 
UWEZO WA _BUNDI_ KUTAMBUA KIFO CHA MTU

BUNDI ni aina ya ndege ambaye hula nyama; hufanya mawindo yao wakati wa usiku na kupumzika wakati wa mchana.
Pamekuwepo na imani kwa wengi kwamba bundi anaponekana nyumbani kwa mtu ni lazima kuna mtu atakufa katika nyumba hiyo.
Hivyo imewapelekea watu wengi kuwa na hofu kubwa sana juu ya kiumbe hiki cha Mungu na hivyo kukihusianisha na nguvu za giza kwamba ni lazima ametumwa na mchawi ili kuchukua roho ya mtu. UKWELI UPO HIVI:

Bundi ana uwezo mkubwa sana wa kuvuta harufu ya mzoga kutoka mbali. Uwezo huu wa kunusa harufu unapita uwezo walionao binadamu.
Hivyo inapotokea katika nyumba fulani kuna mgonjwa mahututi ambaye seli za mwili wake zimeshaanza kufa lakini mapigo ya moyo bado yanafanya kazi; Bundi huweza kunusa harufu ya seli hizo, harufu ambayo binadamu hawawezi kuihisi, na hivyo huvutiwa kuisogelea kwa ajili ya kujipatia chakula, ila hataweza kuingia ndani kwa kuhofia binadamu. Kwa kawaida binadamu hafi mara moja, bali hufa hatua kwa hatua. Zinaanza kwanza kufa seli za mwili, baadaye ogani mbalimbali za mwili.
Ogani za mwisho kufa ni moyo ikifuatiwa na ubongo. Hivyo bundi anapoonekana kwenye nyumba yenye mgonjwa mahututi ni dalili kwamba mgonjwa huyo ameshaanza hatua za kufariki, na hivyo uwezekano wa mgonjwa huyo kufariki siku za karibuni ni mkubwa sana.
Inapotokea kwamba mgonjwa amekufa baada ya bundi kuonekana, tafsiri sahihi siyo kwamba kifo kimesababishwa na bundi bali ni kwamba dalili za kifo cha mgonjwa huyo zimetambuliwa na bundi.
Hivyo cha kufanya siyo kumtafuta mchawi bali ni kuzidi kumkabidhi mgonjwa huyo katika huruma ya Mungu kwa njia ya sala.

Hofu ya bundi kama kiumbe chenye nguvu za giza ipo zaidi Afrika. Ulaya hawana hofu hiyo. Wao humtazama bundi kama kiumbe cha Mungu, kiumbe cha ajabu, na hivyo huvutika kukaribia kwa njia ya utalii, utafiti na hata ufugaji.
Zipo mbuga za wanyama zinazofuga bundi. Sifa mojawapo ya bundi inayowavutia watalii wengi kumtazama ni ule uwezo wake wa kugeuza shingo kutoka mbele mpaka nyuma pasipo kuhitaji kugeuka kwa kiwiliwili chake.

Hivyo hatupaswi kuwaogopa, kuwachukia bundi ama kuongea vibaya juu yao. Hao ni viumbe vya Mungu kama walivyo njiwa, kondoo, v n.k. Wao ni kazi ya Mungu.
Hivyo kuongea vibaya juu ya bundi ni kuongea vibaya juu ya kazi ya Mungu na hiyo kumpa shetani nafasi ili hofu izidi kutawala miongoni mwa watu.
Kwa hiyo tunapowaona bundi tuna wajibu wa kumpa Mungu SIFA NA UTUKUFU Kwa Kuwa Uwezo Huu wa bundi
Kaka uki copy kaz wa watu weka Acknowledgment.....sio vzr watu tuandike makala tuumize kichwa na ktafta source hlf ww una copy2 na kupest
 
intersting lakini wabongo tunapinga hoja sisi tunaamini zaidi mambo ya art bin zuruza MKUU...all in all uandishi mzuri pia uchambuzi mzuri imetulia
 
Ndege karibia wote wana vipawa vya asili vya kuona hatari isiyoonekana kwa macho, ndio maana usiku ukisikia kuku anatoa milio kama anaguna ujue mchawi anapita, ndio maana hata waganga wa kienyeji huwatumia kuku
 
nakubaliana na wewe asilimia mia moja
 
Back
Top Bottom