Uwezo wa bundi kutambua kifo cha mtu

Uwezo wa bundi kutambua kifo cha mtu

Sijui hoja hii uneitoa katika chanzo gani maana ungetuwekea chanzo ingekuwa bora zaidi. Lakini kama chanzo ni wewe mwenyewe basi ntakuambia tu kuwa bundi hali mizoga. Kwa hiyo hawezi kuvutiwa na mizoga kamwe.
nilipata sehemu nikasema bora ni share wa ma greater thinker wa JF, nao watoe maoni yao
 
Sijui hoja hii uneitoa katika chanzo gani maana ungetuwekea chanzo ingekuwa bora zaidi. Lakini kama chanzo ni wewe mwenyewe basi ntakuambia tu kuwa bundi hali mizoga. Kwa hiyo hawezi kuvutiwa na mizoga kamwe.

Sijabahatika kupata jina la mtafiti ila inasemekana na kutoka UDOM. Bado naendelea kufuatilia Jina la mtafiti
 
Mbona hakuna thread mpya nakutana na za jana leo hakuna jipya
 
mi ninacho jua ni mnyama anaye winda kwa kusikiliza sauti za chini mno, anauwezo wakisikia kilicho chini ardhini...huenda kwenye misiba anasikia bargain kati ya marehemu na wanaotaka kumchukua roho yake ...tuendelee kumfanyia utafiti tunaweza pata faida kubwa
 
Mi nimewahi kuonana na bundi maeneo flan ya hospitali..niliogopa mwili mzima ulitetemeka....daaah afu akanikazia macho
 
bundi ndo alivyo,sio anakukazia ila mchana kuona ni shida sasa na sura yake ile akijitahidi kukutazama ndo shida inapoanzia..plus story za mtaa
 
UWEZO WA _BUNDI_ KUTAMBUA KIFO CHA MTU

BUNDI ni aina ya ndege ambaye hula nyama; hufanya mawindo yao wakati wa usiku na kupumzika wakati wa mchana.
Pamekuwepo na imani kwa wengi kwamba bundi anaponekana nyumbani kwa mtu ni lazima kuna mtu atakufa katika nyumba hiyo.
Hivyo imewapelekea watu wengi kuwa na hofu kubwa sana juu ya kiumbe hiki cha Mungu na hivyo kukihusianisha na nguvu za giza kwamba ni lazima ametumwa na mchawi ili kuchukua roho ya mtu. UKWELI UPO HIVI:

Bundi ana uwezo mkubwa sana wa kuvuta harufu ya mzoga kutoka mbali. Uwezo huu wa kunusa harufu unapita uwezo walionao binadamu.
Hivyo inapotokea katika nyumba fulani kuna mgonjwa mahututi ambaye seli za mwili wake zimeshaanza kufa lakini mapigo ya moyo bado yanafanya kazi; Bundi huweza kunusa harufu ya seli hizo, harufu ambayo binadamu hawawezi kuihisi, na hivyo huvutiwa kuisogelea kwa ajili ya kujipatia chakula, ila hataweza kuingia ndani kwa kuhofia binadamu. Kwa kawaida binadamu hafi mara moja, bali hufa hatua kwa hatua. Zinaanza kwanza kufa seli za mwili, baadaye ogani mbalimbali za mwili.
Ogani za mwisho kufa ni moyo ikifuatiwa na ubongo. Hivyo bundi anapoonekana kwenye nyumba yenye mgonjwa mahututi ni dalili kwamba mgonjwa huyo ameshaanza hatua za kufariki, na hivyo uwezekano wa mgonjwa huyo kufariki siku za karibuni ni mkubwa sana.
Inapotokea kwamba mgonjwa amekufa baada ya bundi kuonekana, tafsiri sahihi siyo kwamba kifo kimesababishwa na bundi bali ni kwamba dalili za kifo cha mgonjwa huyo zimetambuliwa na bundi.
Hivyo cha kufanya siyo kumtafuta mchawi bali ni kuzidi kumkabidhi mgonjwa huyo katika huruma ya Mungu kwa njia ya sala.

Hofu ya bundi kama kiumbe chenye nguvu za giza ipo zaidi Afrika. Ulaya hawana hofu hiyo. Wao humtazama bundi kama kiumbe cha Mungu, kiumbe cha ajabu, na hivyo huvutika kukaribia kwa njia ya utalii, utafiti na hata ufugaji.
Zipo mbuga za wanyama zinazofuga bundi. Sifa mojawapo ya bundi inayowavutia watalii wengi kumtazama ni ule uwezo wake wa kugeuza shingo kutoka mbele mpaka nyuma pasipo kuhitaji kugeuka kwa kiwiliwili chake.

Hivyo hatupaswi kuwaogopa, kuwachukia bundi ama kuongea vibaya juu yao. Hao ni viumbe vya Mungu kama walivyo njiwa, kondoo, v n.k. Wao ni kazi ya Mungu.
Hivyo kuongea vibaya juu ya bundi ni kuongea vibaya juu ya kazi ya Mungu na hiyo kumpa shetani nafasi ili hofu izidi kutawala miongoni mwa watu.
Kwa hiyo tunapowaona bundi tuna wajibu wa kumpa Mungu SIFA NA UTUKUFU Kwa Kuwa Uwezo Huu wa bundi

Source: Sijabahatika kupata jina la mtafiti ila inasemekana na kutoka UDOM. Bado naendelea kufuatilia Jina la mtafiti
Hata kwenye makala za wanyama na ndege NatGeo wameeleza hivyohivyo,bundi ana uwezo mkubwa wa kunusa mtu anapokuwa mgonjwa mahututi baadhi ya viungo vyake huwa vimeoza au huanza kuoza ,na kutoa harufu ambayo mwanadamu haisikii bali bundi hata angekuwa wapi anaisikia,kwa kawaida bundi ni ndege mzuri sana kwa haiba ana aibu pia huua panya na nyoka,ilifaa bundi awe ni ndege rafiki badala ya ndege adui,nilitaka kumfuga lakini naogopa kuchomewa nyumba yangu kwa imani zisiz.o na mshiko
 
mi ninacho jua ni mnyama anaye winda kwa kusikiliza sauti za chini mno, anauwezo wakisikia kilicho chini ardhini...huenda kwenye misiba anasikia bargain kati ya marehemu na wanaotaka kumchukua roho yake ...tuendelee kumfanyia utafiti tunaweza pata faida kubwa
Haaa..."anasikia bargain kati ya marehemu na mtoa roho"....hiii kali
 
Hata kwenye makala za wanyama na ndege NatGeo wameeleza hivyohivyo,bundi ana uwezo mkubwa wa kunusa mtu anapokuwa mgonjwa mahututi baadhi ya viungo vyake huwa vimeoza au huanza kuoza ,na kutoa harufu ambayo mwanadamu haisikii bali bundi hata angekuwa wapi anaisikia,kwa kawaida bundi ni ndege mzuri sana kwa haiba ana aibu pia huua panya na nyoka,ilifaa bundi awe ni ndege rafiki badala ya ndege adui,nilitaka kumfuga lakini naogopa kuchomewa nyumba yangu kwa imani zisiz.o na mshiko

Hapa jf tu watu walishanza kumsema vibaya...ukimfuga unatengwa na jamii kabisa..watu wrngi wana imani potofu juu ya bundi
 
Sasa kwa nini ukichoma chumvi anakimbia?
 
Inawezekana harufu ya chumvi inamkera ndio maana anakimbia sawa na wewe ukisikia harufu usiyopenda sidhani kama utakaa mahala hapo,chumvi ni madini na ukichoma hutoa harufu ambayo inaweza isiwe rafiki kwa fundi,je wewe ukichomewa kwa mfano mpira au tairi utakaa hilo eneo?
 
mi ninacho jua ni mnyama anaye winda kwa kusikiliza sauti za chini mno, anauwezo wakisikia kilicho chini ardhini...huenda kwenye misiba anasikia bargain kati ya marehemu na wanaotaka kumchukua roho yake ...tuendelee kumfanyia utafiti tunaweza pata faida kubwa
True! ana uwezo mkubwa wa kusikia, hasa kutokana na uso wake ni kama dishi na anaweza kugeuza dishi hilo likatazama mgongo wake.

Jambo la pili ana uwezo wa kupaa bila kutoa sauti kutoka katika mabawa yake

Ila kwenye uwezo wa kutambua mtu anayekufa sijui, ila tu huwa najiuliza kwa nini bundi wasiwe wengi hospitali.kwenye vifo vingi kama lengo lao ni kututonya.
 
M/mng kaumba viumbe vingi sn.na kira kiumbe kakipa uwezo binafsi.
Bundi ni ndege kama ndenge wengine,ana sifa ya kipekee,ikiwepo ya kuzungusha Shingo.uwezo wa kukaa sehemu moja ata Kwa masaa 2/8 bira kutingishika.ana uwezo wa kuangali mbali bira kupepesa macho nk.pia m/mng kawapa uwezo viumbe wote kuona visivyo onekana na binadamu ima usiku au mchana.hivyo bundi,njiwa,njoka,paka,nawangine inapo tokea swala la kuona wao huona.
KUHUSU USHIRIKINA HIKO KITU HAMNA.
BINAFSI NISHA FUGA BUNDI NIKIWA KIJIJINI. CHOCHOTE ANAKULA.
 
Kazi ya Bundi ni kutoa ishara ya Balaa Na Matatizo kwa Mujibu wa imani zetu

Cha kushangaza wanamchukia Bundi utadhan ndio analeta Tatizo hiLo Kumbe kaz yake Ni kuashiria tu Na kukujulisha 'in advance'
 
UWEZO WA _BUNDI_ KUTAMBUA KIFO CHA MTU

BUNDI ni aina ya ndege ambaye hula nyama; hufanya mawindo yao wakati wa usiku na kupumzika wakati wa mchana.
Pamekuwepo na imani kwa wengi kwamba bundi anaponekana nyumbani kwa mtu ni lazima kuna mtu atakufa katika nyumba hiyo.
Hivyo imewapelekea watu wengi kuwa na hofu kubwa sana juu ya kiumbe hiki cha Mungu na hivyo kukihusianisha na nguvu za giza kwamba ni lazima ametumwa na mchawi ili kuchukua roho ya mtu. UKWELI UPO HIVI:

Bundi ana uwezo mkubwa sana wa kuvuta harufu ya mzoga kutoka mbali. Uwezo huu wa kunusa harufu unapita uwezo walionao binadamu.
Hivyo inapotokea katika nyumba fulani kuna mgonjwa mahututi ambaye seli za mwili wake zimeshaanza kufa lakini mapigo ya moyo bado yanafanya kazi; Bundi huweza kunusa harufu ya seli hizo, harufu ambayo binadamu hawawezi kuihisi, na hivyo huvutiwa kuisogelea kwa ajili ya kujipatia chakula, ila hataweza kuingia ndani kwa kuhofia binadamu. Kwa kawaida binadamu hafi mara moja, bali hufa hatua kwa hatua. Zinaanza kwanza kufa seli za mwili, baadaye ogani mbalimbali za mwili.
Ogani za mwisho kufa ni moyo ikifuatiwa na ubongo. Hivyo bundi anapoonekana kwenye nyumba yenye mgonjwa mahututi ni dalili kwamba mgonjwa huyo ameshaanza hatua za kufariki, na hivyo uwezekano wa mgonjwa huyo kufariki siku za karibuni ni mkubwa sana.
Inapotokea kwamba mgonjwa amekufa baada ya bundi kuonekana, tafsiri sahihi siyo kwamba kifo kimesababishwa na bundi bali ni kwamba dalili za kifo cha mgonjwa huyo zimetambuliwa na bundi.
Hivyo cha kufanya siyo kumtafuta mchawi bali ni kuzidi kumkabidhi mgonjwa huyo katika huruma ya Mungu kwa njia ya sala.

Hofu ya bundi kama kiumbe chenye nguvu za giza ipo zaidi Afrika. Ulaya hawana hofu hiyo. Wao humtazama bundi kama kiumbe cha Mungu, kiumbe cha ajabu, na hivyo huvutika kukaribia kwa njia ya utalii, utafiti na hata ufugaji.
Zipo mbuga za wanyama zinazofuga bundi. Sifa mojawapo ya bundi inayowavutia watalii wengi kumtazama ni ule uwezo wake wa kugeuza shingo kutoka mbele mpaka nyuma pasipo kuhitaji kugeuka kwa kiwiliwili chake.

Na
_Dr. Amani L. Mang'alila
_Animals Behavior & Psychology_.
Dodoma - Tanzania
Huku Africa Huyo ni uchuro.kule ulaya ni mafanikio,hujaona mabango mengi ya shule /vyuo vya huko hunakishiwa na picha ya kisirani huyu.
 
Back
Top Bottom