Uwezo nyuma ya sayansi ya ulimwengu

Nov 24, 2019
11
18
Una amini juu ya huu usemi "kila mtu anakula kwa urefu wa kamba yake" Na je, una amini kuenda darasani ndio mafanikio au talanta "talent " uliyo nayo ndio mafanikio?

Basi mtambue ARCHERFISH, Mfizikia "physicist " ambae hakuenda darasani.

Huyu ni samaki (jamii ya samaki wadogo katika kundi LA TOXOTIDAE) Aina hii ya samaki wana maajabu ya peke
Samaki Hawa huwa wana winda windo lao wakiwa majini huku windo likiwa nchi kavu unaweza jiuliza ana wezaje!?

Huwa wanafanya hivi, pale wanaona windo lao lipo karibu hasa kwenye tawi karibu na maji au kwenye majani Karibu na maji huwa wana puliza maji mithiri ya bomba linavyotoa maji na kulinasa windo lake.

Kwanini anaitwa Mfizikia "physicist "? Ingalikuwa yeye ni mnyama? Kumbuka turudi shule kidogo na wataalamu watusaidie. Kuna kitu kinaitwa LAWS OF REFRACTION, fizikia ni sayansi "science" na sayansi ina sheria zikivunjwa utata unakuja.

Law of refraction inasema "mwanga huwa una pinda pale unapo pita Kutoka kwenye hewa kwenda kwenye maji au kioo" ina maana Kuwa unacho kiona kwenye maji hakipo sehemu sahihi "location" kitaalamu wanasema ni "vitual image " location sahihi ya hiko kitu kipo mbele au nyuma ya hiko unacho kiona.

Swali sasa ARCHERFISH anawezaje kumdungua mdudu akiwa ndani ya maji na law of refraction ina eleza tofauti na mafanikio yake Ambayo yana zaa matunda mazuri!? Je, huyu samaki katuzidi nini sisi binadamu juu ya hii law?

REF: "spit decision :how archerfish decide 19 November 2013
Archerfish, 2016.

Additional :facebook @ ZOO learning.
IMG_20200413_202630_037.jpg
IMG_20200413_201712_494.JPG

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hajatuzidi hata kidogo ila huyo maisha yake ndo yanategemea huo ujanja ili aishi na mazingira yamemlazimu kukomaa na hali mpaka akabaini hiyo reflection, kwani akizubaa anajua ndoano inamhusu.
 
ni nature tu
Kumbuka we are living in nature guided with science, Mfano experiment ilifanyika na kuonesha Kuwa matokeo tofauti na huyo samaki ,slope ya graph experimentally inaonesha sio rahisi
Na ukilazimisha unapata kitu kinaitwa "VISUAL DISTORTION" na technically na majaribio yaliyo Fanywa huyu samaki anakuwa accurate Kati ya angle 74° na anakuwa accurate zaidi Kati ya angle 110° na 45° kitu ambacho, kina Leta matokeo tofauti kwetu sisi binadamu na experiment zetu
IMG_20200414_165510_252.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Swali sasa ARCHERFISH anawezaje kumdungua mdudu akiwa ndani ya maji na law of refraction ina eleza tofauti na mafanikio yake Ambayo yana zaa matunda mazuri!? Je, huyu samaki katuzidi nini sisi binadamu juu ya hii law?

Sent using Jamii Forums mobile app
Naomba nijaribu kujibu swali lako, japo linahitaji pia mtu awe mtaalamu wa mambo ya elimu ya viumbe, kwa sababu linamhusisha kiumbe samaki. Physics is the study of matter in relation to energy. Sasa matter na energy hapa sivioni sana uhusiano wake, japo kuna mwili wa samaki unaorusha maji juu, una-release energy, labda sasa na mwili wake tuchukulie ndiyo matter.

Sikumbuki vizuri lakini nadhani samaki ana uwezo wa kuona kwa nyuzi 180 (180 field of view). Kwa maana hiyo yeye ndani ya nyuzi 180, ana uwezo wa kuona kawaida bila kujali kitu kiko wapi ili mradi tu kiwe ndani tu ya hizo nyuzi 180. Na kwa sababu refractive index ya maji ni ndogo kuliko nyuzi 180 (ukiangalia kwenye mchoro wako hapo juu), na ni pembe kali, ina maana pembe hiyo iko ndani ya field of view ya samaki, eneo lake la kujidai ambalo anaweza kuona kitu pale kilipo pasipo matatizo yoyote. Still, refractive index hata ingekuwa pembe butu, bado angeweza kukamata prey wake kama kawaida kwa sababu pembe hiyo bado ingekuwa ndogo kuliko nyuzi 180. Ni kitu kile tu ambacho kiko nje ya nyuzi 180 za uono wa samaki ndicho ana uwezekano wa kukosea kukikamata, kama akikihitaji.

Zaidi tu ni kwamba mwanga huwa unapindishwa kuelekea mbali na reference vertical line inayoitwa NORMAL, (vertical axis) kama utasafiri kuingia kwenye mada yoyote ya kitu ambacho kina tungamo (density) ndogo kuliko ile ya mwanga, na vilevile huwa unapindishwa kwa kusogea karibu na mstari huu, kama utaingia kwenye mada ya kitu chenye tungamo kubwa kuliko ile ya mwanga. Normally, any angle of refraction is necessarily less than 90 degrees and; at 90 degrees angle of refraction , we get what a phenomenon which is popularly known as TOTAL INTERNAL REFRACTION, scenerio ambayo huwa inasababisha tunaona kama maji yanayomeremeta bararbani kwa mbali, tunapokuwa tunatembea kwenye barabara ya lami wakati wa jua kali (mirage)
Kujibu hili swali, inabidi pia uwe unajua namna ambavyo samaki huwa anaona. Kwa hiyo swali hili labda tuseme linahitaji sana sana wataalamu wa Bio-physics, kama discipline hiyo huwa ipo. Ubarikiwe kwa kulete changamoto hii
 
Back
Top Bottom