Uwezo mdogo kuzinyima kampuni za ndani fursa ya kunufaika na mnyororo wa usambazaji mafuta na gesi

Daniel Mbega

JF-Expert Member
Mar 20, 2013
338
180
Uwezo wa kampuni za Tanzania kumudu ubora unaohitajika katika sekta ya gesi bado ni mdogo pamoja na kwamba sekta yenyewe bado ni changa pia.

Aidha, uzoefu unaonyesha kwamba faida itokanayo na uzalishaji wa rasilimali kama gesi ni nadra sana kufaidisha jamii na eneo husika ambako rasilimali hiyo inachimbwa, hata katika nchi zenye utajiri wa rasilimali Afrika. Hii ni sawa pia kwa nchi zinazojitokeza kama Tanzania.

Changamoto nyingine ni kwamba, kampuni za kimataifa zinazotoa huduma kwenye sekta ya gesi zina uhusiano mzuri na kampuni za kimataifa za mafuta na gesi, jambo ambalo linafanya kampuni hizo kuziondoa kampuni za wazawa kwenye mnyororo wa thamani katika shughuli ya mafuta na gesi.

Soma zaidi hapa => Uwezo mdogo kuzinyima kampuni za ndani fursa ya kunufaika na mnyororo wa usambazaji mafuta na gesi | Fikra Pevu
 
Back
Top Bottom