Uwezo Duni TBS Unaligharimu Taifa


Ukifika k/koo kutaka kununua vitu vingi unaulizwa unataka fake au genuine? Ukishafikia sehemu unaenda dukani unaulizwa hivyo ujue hakuna TBS wala nini ni ujinga tu unaoendelea.
 
ukitafakari mambo kwa kina sana unaweza kufikia hitimisho kwamba HATUNA serikakti!.
tuna kagenge fulani tu kanajiita watawala/viongozi ambako bahati mbaya sana kamehodhi kila kitu kuhusu maisha yetu wananchi.
Huo ndio ukweli...tena kama sasa Wafanyakazi Wote Serikalini ni kama wamefunguliwa kutoka jela, kila mtu anawaza kupiga kufidia miaka mitano ya Jiwe....semina, makongamano, rushwa kama zote.
 
Hili swala la Vitu fake au havina ubora ni swala la msingi sn serikali inahitaji iongeze umakini vitu fake au havina ubora sababu kuna vitu sio kabisa vya kuvifumbia macho
Kama vitu vya ujenzi nk kwamfano angalia NYUMBA zinavyo waka moto ukichunguza utakuta hitilafu ya umeme inayotokana mara nyingi na vifaa vya umeme havina ubora kabisa inaweza kuwa wire au sockets nk.
 
Wachina wa enzi ya tazara hawapo tena wamekuja wachina wapya wapiga dili
 
Achana na hayo, kuna CHANJO eti tume ya wataalamu wa bongo wamesema ni salama, sijui wameitest kwenye maabara gani, mimi huwa nawaangalia halafu nasema hiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
Hiyo chanjo iko Soko gani? Kariakoo au machinga complex?
 
Ongeza hawa ndugu zangu wa TMDA, wizara ya Afya na wizara ya mifugo wote wanahatarisha afya za watanzania zamani ilikuwa vigumu kwa vijana kufa na magonjwa ya ini na figo ila nimekuja gundua hawa ndugu zetu hawafanyi kazi zao vizuri wameridhika huko maofisini ili hali watanzania wanaangamia kwa kubugia vyakula vya sumu kila siku.

Nakuja na andiko langu.
 
Kuna jiran yangu anakiwanda kidogo cha kuchana mbao,, kila siku analia na mikanda ya mashine ya kichina,, kampuni la mikanda linaitwa MITSUBA yan mikanda kila baada ya siku mbili ananunua mikanda mingine. Mchina hana maana
 
Unamlaumu victim na kuwaacha waliopewa kazi ya kuthibiti ubora na wanalipwa kwa kodi yako. Huku ni kutokuwajibika.
 
Ongeza hapo pia ni wala rushwa wakubwa wengi wao huzibwa midomo kwa kupewa fungu ndio maana unaona bidhaa feki zimejaa sana huku mtaani.
 
tunapenda sana vitu vya chini, vilivyopangawa chini
saa za mafungu,
viatu vya mafungu.
tanaenda kwa mafungu tu
buku buku pa pa
toa buku pa pa pa
Tuanze kidogo kidogo kuwa wenyewe tbs hawataketa tena
mbona kwenye mchele tunachagua wa Mbeya?
 
Hongera mleta mada kwa kuiibua hii mada upya, ipo humu imeletwa kama mara mbili na imejadiliwa sana, jambo la kubwa hapa ni kwamba hatuna serikali iliyopo kwa ajili ya watu badala yake iko kwa ajili "watawala". Ndio maana unaona vyombo ambavyo viko active ni vile vinavyowalinda watawala, matokeo yake wanakimbizana hadi na wachora katuni. Lakini vyombo vinavyogusa maslahi ya wananchi moja kwa moja ni either butu au havina meno kabisa.

Tatizo sio umaskini wa nchi, tatizo ni uwajibikaji wa waliopewa dhamana, kuna bidhaa zinazoingizwa hapa kwetu huwezi kuzilinganisha kwa ubora hata na bidhaa zinazoingizwa pale kwa mzee Museveni.
 
U
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Yote tisa,

Kumi hujauziwa kadet nzuri ya kung'aa alafu ukiweka kwenye maji tu inageuka rangi, kama ilikuwa ya kijivu inakuwa nyeupe au njano
nachosema ni sahihi kabisa mkuu.juzi nimenunua suruali mpya dukani lkn baada ya kuivaa nikafua.Duhh maji yote yaligeuka kuwa meusi ni kama vile iliwekwa kwenye rangi na kutolewa.ni balaa tupu mpaka leo sina hamu ya kuivaa tena nahisi nikivua mara tatu basi rangi yote ya suruali itapotea.
 
Kuna jiran yangu anakiwanda kidogo cha kuchana mbao,, kila siku analia na mikanda ya mashine ya kichina,, kampuni la mikanda linaitwa MITSUBA yan mikanda kila baada ya siku mbili ananunua mikanda mingine. Mchina hana maana
Na bahati mbaya sasa hivi, hata ukiwa na nia ya kupata bidhaa nzuri, hupati. Maduka karibu yote yamejaza hizo bidhaa zisizo na ubora toka China.
 
Halafu taasisi hizi zimejaa wazee wa kaunda ama ndio tuseme nao wanahujumu nchi kwa kuzibwa midomo kwa kupokea rushwa.

Hatuwezi kuwa na taifa ambalo viongozi wakuu wa nchi hawajali afya na uhai wa watanzania, na kwa kukazia ni kwamba nchi haiwezi kupiga hatua yoyote kama wananchi hawajahakikishiwa afya bora.
 
wahusika kama watakuelewa watatuokoa sana na taifa letu pengine litasonga mbele
 
Na hii ndo shida aliyoleta mwalimu nchi hii 'siasa kupewa kipaumbele' mara utasikia siasa ya ujamaa na kujitegemea, siasa ni kilimo, chama kushika hatamu, ukirudi huku lugha ya uswahili swahili. Haya mambo yalidumaza watanzania kifikra sana sana, na hadi leo hii unakuta mwanasiasa mwenye elimu ya hapa na pale na mwingine kaishia la saba naye anatoa maelekezo kwa wataalamu na wanamsikiliza kabisa.....​
 
Ongeza hapo pia ni wala rushwa wakubwa wengi wao huzibwa midomo kwa kupewa fungu ndio maana unaona bidhaa feki zimejaa sana huku mtaani.
Kabisa mkuu, kimsingi tunakubaliana kwamba issue sio vifaa vya kazi au sifa za wafanyakazi, vyote hivyo vipo vizuri kabisa, tatizo ni WATU, tatizo ni sisi na wao yaani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…